Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Inasikitisha Askari kumtishia Raia inasikitisha tunako kwenda siyo kuzuri, kama wanaopaswa kutulinda ndo wanao tutisha na siraha nasikitika sana, Dar es salaam si salama kwa kweli, MUNGU ibariki Tanzania.

Sent from my itel it1507 using JamiiForums mobile app
 
Yet, kuna watu wanasifia ujinga huu. Nchi yetu ina shida sana.
Nimetishika sana na hii!
yule askari yuko totally blinded na hasira ,bado wenzie hawakupata akili ya kuona nini kingeweza kutokea?
mtu anafoka kwa hasira ya kimaumbile kabisa,hakuna aliyeona kuwa huyu hayuko sawa kiasi anyang'anywe silaha?
like serious hii ndio namna ya kukamata wahalifu?
(sikubaliani na kitendo cha malima kukaa ndani ya gari akiwa ameegesha mahali kusikotakiwa na kugoma kushuka)
LAKINI askari kwa nidhamu ipi ya chombo cha moto aliruhusiwa kuendelea kuwa nacho?
wenzie hawakuona?
anaenda anarudi anafyatua anashusha anapandisha anafyatua tena? nini kilikuwa kinaenda kutokea hapa?
SIELEWI!
 
Achana na maelezi, je kwa ulichokiona unadhani kulikua na ulazima gani wa kupiga risasi?

Kwa ulichokiona, kulikuwa na ulazima gani kwa hao jamaa kupaki gari mahala siyo ruhusa kupaki!?

Kwa ulichokiona, kwa nini waongee hivyo kuwadharau polisi!?

Kwa ulichokiona, kwa nini wasitii Sheri na kuwa waadilifu!?

Polisi alifanya hivyo kukomesha midomo na wanaopenda kufata gari lao kwenda kituo cha polisi.

Ila polisi wetu wasilaumiwe
kwa sababu, nchi zingine huwa watu wanatii sheria bila shuruti mfano, kama ni no parking ( No ) wenzetu hawapaki kabisaa sasa sisi huko Tanzania inakuwaje!?

Tuache kutetea wavunja sheria kwa sababu ya vyeo, fedha au sababu zingine zingine tunazozijua.

Mfano, Barabara nyingi hapo Dar zimewekewa uzio wa kukataza kukatisha zile bustani sasa angalia barabara ya Mandela, Nyerere, kijitonyama kwenda city centre kila bustani hizo waenda kwa miguu wanakatiza na wenye magari wanazigonga.

Swali, mbona pale Mwenge mkono wa kushoto pana hizo bustani lakini watu hawakatishi na Magari hayagongi zile bustani!?

Jibu lake pale bustani ya Mwenge pana kakibao kadogo sana kameandikwa ONYO kukatisha bustani (JWTZ) na hakuna kweli anayegusa wala gari halijawahi kugusa wala kugonga ile bustani.

Sasa kwa nini, hao wasitii Sheria!?

Hili jambo, ukiliangalia kwa chuki zako kwa polisi utaona kuwa polisi kakosea ila hekima ya Malina ilipungua pale yeye Kama kiongozi tena mkubwa alipaswa kuonesha weredi na uwezo wa kuchambua mambo na hekima.

Acha , nisiseme sana ila haya mambo yanahitaji hekima na kutii sheria au amri bila shuruti.
 
Hao wapumbavu wa chama cha magamba acha wavune walicho panda "wafu wazikane tu akuna namna"
 
Kwa Matumizi Haya Ya Hovyo Hovyo Ya Silaha
Ni Hatari Sana Kwa Askari Lakini Pia Wananchi Tujitahidi Kujua Nguvu Ya Umma Ni Kubwa Kuliko Silaha.
Utemi Haufai Popote Pale!!!!
huyu askari zuzu sana yaani kitu cha kutumia busara n akili yeye anafytua risasi.
 
Unaandika mambo meengi halafu mashudu tupu. .

Ungeandika mambo yako machache bila kutukana ungeonesha hekima ila Kwa lugha yako hiyo chafu tarajia polisi kukukamata na kukufyatulia risasi.

Maana haya maneno ya kukashifu wengine hasa polisi wetu ndiyo yanayopelekea mfyatuliwe risasi baadye mnalialia bila kuangalia lugha zenu.

Asante sana, kwa kunitukana. Ila omba usikutwe na polisi kisha ukajisahau kuwa uko JF kumbe upo na polisi ukatukana mrejesho wake utaujua mwenyewe.
 
Hiyo clip ikifika Ikulu aliyekua anamzuia mwenzaje ni lazima awajibishwe kwa kitwndo cha yeye kama afisa wa serikali kumpinga afisa mwenzake hadharani badala ya kuonyesha uwajibikaji wa pamoja na Hugo aliyekua amepanic na kupiga risasi hovyo, IGP ataagizwa ampandishe cheo.
Kweni interahamwe walianzishwaje nadhani ni hivihivi.
 
Mawazo ya kipuuuzi nimeanza kufahamu kwa nini raisi anasema sipangiwi ,maana akiwasikiliza ninyi roho zenu zimejaaa chuki na ushabiki usio kua na maana.Unafahamu ni sheria gani inampa mamlaka askari kutumia risasi za moto?? Au unabwabwaja tu.
Nenda CCP utaoneshwa
 
Aliye na cheti feki hata umpe mafunzo ya kupika Chai, kesho yake mwambie aipike mwenyewe lazima uone maajabu tu.
[emoji81] [emoji81] [emoji81] [emoji81] [emoji81] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Sitagusia sababu za kilicho sababisha gari ya Mtoto wa Malima kukamatwa. Ntajikita kwenye matumizi sahihi ya silaha ya moto.
Tatizo pia kwani lazima majembe auction mart lazima watembee na askari wenye silaha?! Kama majembe wakihatarishiwa maisha yao si polisi wapo?! Kuna biashara gani kati ya majembe auction mart na polisi?! Kwani majembe auction mart hawawezi tu kupiga faini za EFD mtu akalipe mbele kwa mbele kama trafiki baada ya kuchukuwa picha za gari lilipopakiwa time na siku?! Hapa kuna maswali na majibu mengi ambayo ni rahisi sana, kulikuwa hakuna haja ya kutumia chombo cha moto kipuuzi kama vile, yaani imefika wakati askari anajiona hayuko kamili bila silaha?!
Sasa hapa ndipo tunaporudi mitaa ya Kibiti na MKuranga, mie nina uhakika kabisa kama raia kule wangekuwa na uhusiano mzuri na wanausalama, wale wauaji majambazi wangeshakamtwa siku nyingi, ila kutokana na haya matukio tuyaonayo DAR kidogo nakuwa na mashaka, imagine raia wa Kibiti MKuranga mitaani kule wanavyopurukushana na askari?!
Polisi yahitaji marekebisho makubwa sana kati yao na raia, isiwe sisi vs polisi Bali sisi na polisi dhidi ya uhalifu...
 
K

Kikawaida/kitaratibu/kiitifaki mbunge ni mtu mwenye heshima katika jamii , askari alipaswa kutoa salamu ya saluti , askari wetu hawajui mipaka yao!
Mimi ninavyojua mbunge anapigiwa salute akiwa kwenye eneo la jimbo lake tu.
 
Back
Top Bottom