Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Unajua iyo risasi ni kodi yetu sisi? Bei ya risasi unaijua?
Ni kodi zenu sawa ndo mvunje sheria??kwa vile ni kodi zenu shuleni si mlikuwa mnapeleka rimu kwa ajili ya matumizi ya mitihani kuna siku ulipewa alama 100%kuwa mwalimu amekupa baada ya kuwa mpeleka rimu bora???
 
Askari hovyo sana huyu eti ameapa. Kiapo chako hakizui Mwananchi kuhoji uhalali wa vitendo vyako hasa unapoenda kinyume na haki za raia. Askari mpuuzi kweli.
 
Binafsi nachukizwa sana na hii operation liyoibuka hivi karibuni hapa Dar es salaam inayoitwa wrong parking.
Wahanga wa hii operation ni wa wamiliki wa vyombo vya moto hasa magari.
Kampuni za udalali zinaenda vtuo vya polisi na kuwachukua askari wenye silaha na kuanza kutembetea mitaani kutafuta magari yaliyoegeshwa vbaya,wanasumbua sana watu barabarani kisa wako na polisi na matokeo yake ndo kama hayo.Inafanyika kati ya saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni na kila askari anashiriki katika operation hiyo hupewa kifuta jasho cha sh elfu 20.
Rai yangu ni kuwaomba viongozi wa wa manispaa zetu kuona namana mbadala ya kuliondoa tatizo hili na kuifuta operation hii maana ni kero kubwa sana,,kibaya zaidi ni kwamba sehemu kubwa ya pesa zinazotozwa zinawanufaisha hawa jamaa wanaokamata na sio serikali,,wanakamata magari 20 wanaandikia 5,,,iliyobaki ni halali yao.
 
Wangelipaki wapi na barabara zimejengwa kama corridor za guest house.
 
mkuu ile gari ndio wameichukua hao polisi au vipi, na hao majembe siku hizi wamekuwa walinzi
Tanzania haieleweki mlinzi halisi ni nani.Leo hii viongozi wa madereva bodaboda walishajigeuza nao trafic wanakamata na kutoza watu faini barabarani bila utaratibu.
Makampuni ya maegesho nao vivyo hivyo ni full kusumbua watu.Mbona majuzi ilitolewa taarifa kuwa hata kama ni wrong packing mtu akamatwe tu ikiwa kapaki zaidi ya saa moja.
In short kuna mapungufu mazito ktk sheria zetu(by laws).Imebaki udhalilishaji tu.
 
Wangelipaki wapi na barabara zimejengwa kama corridor za guest house.

Acha mawazo finyu.

Yeye tu ndiye ana gari au yeye pekee ndiye aliyepita barabara hiyo!?

Mbona hawajakamata wote watumiaji wa eneo hilo!?

Binafsi, huwa sitetei wavunja sheria hata wawe kwenye familia yangu!
 
Umenena. Hii ndo inayotakiwa.
 
Acha mawazo finyu.

Yeye tu ndiye ana gari au yeye pekee ndiye aliyepita barabara hiyo!?

Mbona hawajakamata wote watumiaji wa eneo hilo!?

Binafsi, huwa sitetei wavunja sheria hata wawe kwenye familia yangu!
Wanayakamata sana wengine hawapendi kudai haki zao wanaona bora wanyamaze. Kelele zililetwa na wenye maduka yao na migahawa barabara ile maana wao ndio wahanga, wateja wao wakija kununua vitu lazima wawasumbue mpaka imepelekea wengine wasiwe wanaenda maeneo hayo
 
Wanjusanya kodi, hujusikia bosi sao alivosema?
 
mimi nimeapa!!!

umeapa kufanya nini??

Swali zuri kweli kweli.Kuna huyu askari mwenzake aliyekuwa anajaribu kumtuliza huyu mwenzake,kwangu mm ningekuwa amiri jeshi huyu aliyekuwa anayemtuliza mwenzake ndiye anastahili kupandishwa cheo.Unapokuwa na silaha kama hiyo ya SMG hutakiwi kuwa na jazba.Askari ali-over react.Sitashangaa kama huyu aliyefyatua risasi atachukuliwa hatua.Malima alikuwa hana silaha ametulia,unafyatua risasi hewani ya nini?Tukio kidogo linafanana na Bw.Nape.Anyway,it could be doctored,who knows.
 
Shabiki ni wewe unayedhani kuwa wengine wote ni wageni hapa nchini. Ikiwa scenario ile ndio imeleta kadhia yote hiyo, basi kusingekuwa na salio la risasi huko maghalani. Ubishi mdogo ule risasi zinapigwa, je huko masokoni na kwenye stendi za dala dala si risasi zingekuwa zinarindima kila uchao?

Endeleeni kujitoa fahamu, lkn najua kuwa ndani ya mioyo yenu mnafahamu kuwa SI SAWA. Hata huku kuzomewa ni matokeo ya kuishi vibaya na watu.
 
Lakini tambua kuwa hata yule askar mwingine aliyekuwa anamzuia ilifika wakati naye akalazimika kukoki silaha yake,maana yake ni kuwa hali haikuwa nzuri hapo
 
Mimi maneno yangu ni yale yale.
Watanzania tuamke na tujue sharia zetu hasa waandishi . wawo ndio wanaweza kuziandika na watu wote kujua.

Tukio lililotokea ingekuwa kama hivi ingekuwaje.
Mzee umepaki gari sipo naomba uondoshe gari yako hapa . nakupa dakika tano .
Dereva kakaidi hataki kuondoka, askari achukuwe plate number halafu aombe leseni ya Dereva, aombe insurance ya Gari. ili ufunguwe mashtaka. Katoa andika kila kitu na kumpa karatasi ya kuja mahakamani.

Kama Dereva hataki kutoa vyote hivyo Askari ita polisi wengine waje kusaidia na kumkamta .

Haina haja ya kutupiana maneno wala kupiga risasi juu.

Safari ndefu tunayo watanzania
 
Inaonesha kijana uwezo wako wa kufikiri bado ni mdogo! Kuna msemo unasema; TII SHERIA BILA SHURUTI. Malima angetii amri na kumwambia dereva wake aondoa gari pale alipo park unadhani haya yaliyotokea yangejitokea? Mbona tunakuwa wepesi wa kulaumu tena upande mmoja?
Pindi walivyouawa wale askari wa 8 kuna wajinga baahdi humuhumu kwenye mitandao walikuwa wanafurahia, Ila waungwana wakawa wanawauliza; wangekuwa ndugu zenu Ungefurahia!?..
Enzi ya kubembelezana ya Mzee bure ilishaisha. Vijana mjitambue, sio kuishia kulaumu tu, mnapoteza muda wa fikra chanya. Sisemi kwamba askari polisi eti wapo perfect kwa 100%, 100% hapana. Ila kwa hili mh. Malina kachemka.

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…