illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Hapo lile tukio limeangukia kwny kifungu gani..?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo lile tukio limeangukia kwny kifungu gani..?
Ni kodi zenu sawa ndo mvunje sheria??kwa vile ni kodi zenu shuleni si mlikuwa mnapeleka rimu kwa ajili ya matumizi ya mitihani kuna siku ulipewa alama 100%kuwa mwalimu amekupa baada ya kuwa mpeleka rimu bora???Unajua iyo risasi ni kodi yetu sisi? Bei ya risasi unaijua?
Wangelipaki wapi na barabara zimejengwa kama corridor za guest house.Kwa ulichokiona, kulikuwa na ulazima gani kwa hao jamaa kupaki gari mahala siyo ruhusa kupaki!?
Kwa ulichokiona, kwa nini waongee hivyo kuwadharau polisi!?
Kwa ulichokiona, kwa nini wasitii Sheri na kuwa waadilifu!?
Polisi alifanya hivyo kukomesha midomo na wanaopenda kufata gari lao kwenda kituo cha polisi.
Ila polisi wetu wasilaumiwe
kwa sababu, nchi zingine huwa watu wanatii sheria bila shuruti mfano, kama ni no parking ( No ) wenzetu hawapaki kabisaa sasa sisi huko Tanzania inakuwaje!?
Tuache kutetea wavunja sheria kwa sababu ya vyeo, fedha au sababu zingine zingine tunazozijua.
Mfano, Barabara nyingi hapo Dar zimewekewa uzio wa kukataza kukatisha zile bustani sasa angalia barabara ya Mandela, Nyerere, kijitonyama kwenda city centre kila bustani hizo waenda kwa miguu wanakatiza na wenye magari wanazigonga.
Swali, mbona pale Mwenge mkono wa kushoto pana hizo bustani lakini watu hawakatishi na Magari hayagongi zile bustani!?
Jibu lake pale bustani ya Mwenge pana kakibao kadogo sana kameandikwa ONYO kukatisha bustani (JWTZ) na hakuna kweli anayegusa wala gari halijawahi kugusa wala kugonga ile bustani.
Sasa kwa nini, hao wasitii Sheria!?
Hili jambo, ukiliangalia kwa chuki zako kwa polisi utaona kuwa polisi kakosea ila hekima ya Malina ilipungua pale yeye Kama kiongozi tena mkubwa alipaswa kuonesha weredi na uwezo wa kuchambua mambo na hekima.
Acha , nisiseme sana ila haya mambo yanahitaji hekima na kutii sheria au amri bila shuruti.
Tanzania haieleweki mlinzi halisi ni nani.Leo hii viongozi wa madereva bodaboda walishajigeuza nao trafic wanakamata na kutoza watu faini barabarani bila utaratibu.mkuu ile gari ndio wameichukua hao polisi au vipi, na hao majembe siku hizi wamekuwa walinzi
Wangelipaki wapi na barabara zimejengwa kama corridor za guest house.
Umenena. Hii ndo inayotakiwa.Binafsi nachukizwa sana na hii operation liyoibuka hivi karibuni hapa Dar es salaam inayoitwa wrong parking.
Wahanga wa hii operation ni wa wamiliki wa vyombo vya moto hasa magari.
Kampuni za udalali zinaenda vtuo vya polisi na kuwachukua askari wenye silaha na kuanza kutembetea mitaani kutafuta magari yaliyoegeshwa vbaya,wanasumbua sana watu barabarani kisa wako na polisi na matokeo yake ndo kama hayo.Inafanyika kati ya saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni na kila askari anashiriki katika operation hiyo hupewa kifuta jasho cha sh elfu 20.
Rai yangu ni kuwaomba viongozi wa wa manispaa zetu kuona namana mbadala ya kuliondoa tatizo hili na kuifuta operation hii maana ni kero kubwa sana,,kibaya zaidi ni kwamba sehemu kubwa ya pesa zinazotozwa zinawanufaisha hawa jamaa wanaokamata na sio serikali,,wanakamata magari 20 wanaandikia 5,,,iliyobaki ni halali yao.
Wanayakamata sana wengine hawapendi kudai haki zao wanaona bora wanyamaze. Kelele zililetwa na wenye maduka yao na migahawa barabara ile maana wao ndio wahanga, wateja wao wakija kununua vitu lazima wawasumbue mpaka imepelekea wengine wasiwe wanaenda maeneo hayoAcha mawazo finyu.
Yeye tu ndiye ana gari au yeye pekee ndiye aliyepita barabara hiyo!?
Mbona hawajakamata wote watumiaji wa eneo hilo!?
Binafsi, huwa sitetei wavunja sheria hata wawe kwenye familia yangu!
Wanjusanya kodi, hujusikia bosi sao alivosema?Binafsi nachukizwa sana na hii operation liyoibuka hivi karibuni hapa Dar es salaam inayoitwa wrong parking.
Wahanga wa hii operation ni wa wamiliki wa vyombo vya moto hasa magari.
Kampuni za udalali zinaenda vtuo vya polisi na kuwachukua askari wenye silaha na kuanza kutembetea mitaani kutafuta magari yaliyoegeshwa vbaya,wanasumbua sana watu barabarani kisa wako na polisi na matokeo yake ndo kama hayo.Inafanyika kati ya saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni na kila askari anashiriki katika operation hiyo hupewa kifuta jasho cha sh elfu 20.
Rai yangu ni kuwaomba viongozi wa wa manispaa zetu kuona namana mbadala ya kuliondoa tatizo hili na kuifuta operation hii maana ni kero kubwa sana,,kibaya zaidi ni kwamba sehemu kubwa ya pesa zinazotozwa zinawanufaisha hawa jamaa wanaokamata na sio serikali,,wanakamata magari 20 wanaandikia 5,,,iliyobaki ni halali yao.
mimi nimeapa!!!
umeapa kufanya nini??
Kwahyo ww hujaona hapo?Hapo lile tukio limeangukia kwny kifungu gani..?
Shabiki ni wewe unayedhani kuwa wengine wote ni wageni hapa nchini. Ikiwa scenario ile ndio imeleta kadhia yote hiyo, basi kusingekuwa na salio la risasi huko maghalani. Ubishi mdogo ule risasi zinapigwa, je huko masokoni na kwenye stendi za dala dala si risasi zingekuwa zinarindima kila uchao?Kwahyo ww ulitakaje?
Hebu jivishe uhusika wa askari halafu Malima kapaki gari wrong packing wanashuka watu unaowasindikiza kwaajili ya kazi hyo ya kukamata wanaoegesha magari ovyo anawaita kuwa ni majambazi mpaka watu wanajaa kwaajili ya kuwadhuru.. Je ungefanyeje?
Acheni ishabiki![]()
Lakini tambua kuwa hata yule askar mwingine aliyekuwa anamzuia ilifika wakati naye akalazimika kukoki silaha yake,maana yake ni kuwa hali haikuwa nzuri hapoAskari wa pili anaonekana kumzuia mwenzake asipige risasi juu.
Kama kweli alikuwa hatarini kwanini mwenzake amzuie na kumsihi aache?
Concentration na macho ya askari wote wawili ilikuwa kwa mtuhumiwa.
Hivyo ni wazi hapakuwepo na hatari yeyote kwa askari hao na kwa ushahidi mwingine yule askari aliwasogelea wale wananchi huku akiongea mbona hakuogopa kuwasogelea wale watu waliokuwa wengi kiasi kile.
*Malima ana makosa pia alipoambiwa mzee ondoka Mara mbili alibakia bado huku akilalamika kwa tendo hilo lazima askari wangekasirika ,Malima pia analo la kujibu.
![]()
Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.
Yalikuwa ni majibizano kati ya PRE SCAN AUCTION MATT waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.
Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.
Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.
Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.
Adam Kighoma Malima alikuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, aliwahi kuwa pia Naibu Waziri wa Fedha enzi za Kikwete. Anatokea katika chama cha CCM.
====
UPDATES:
Adam Malima afikishwa Mahakamani kwa Kumzuia Askari kufanya kazi yake. Habari zaidi soma=>News Alert: - Adam Malima afikishwa Mahakama ya Kisutu na kusomewa shtaka la 'Kumzuia askari kufanya kazi yake'
Inaonesha kijana uwezo wako wa kufikiri bado ni mdogo! Kuna msemo unasema; TII SHERIA BILA SHURUTI. Malima angetii amri na kumwambia dereva wake aondoa gari pale alipo park unadhani haya yaliyotokea yangejitokea? Mbona tunakuwa wepesi wa kulaumu tena upande mmoja?Mimi maneno yangu ni yale yale.
Watanzania tuamke na tujue sharia zetu hasa waandishi . wawo ndio wanaweza kuziandika na watu wote kujua.
Tukio lililotokea ingekuwa kama hivi ingekuwaje.
Mzee umepaki gari sipo naomba uondoshe gari yako hapa . nakupa dakika tano .
Dereva kakaidi hataki kuondoka, askari achukuwe plate number halafu aombe leseni ya Dereva, aombe insurance ya Gari. ili ufunguwe mashtaka. Katoa andika kila kitu na kumpa karatasi ya kuja mahakamani.
Kama Dereva hataki kutoa vyote hivyo Askari ita polisi wengine waje kusaidia na kumkamta .
Haina haja ya kutupiana maneno wala kupiga risasi juu.
Safari ndefu tunayo watanzania