Nimeangalia vizuri, polisi amefyatua risasi
Ukweli usipingika ni kwamba huyo jamaa amewajibu nyodo kwa kua baba yake alikua mtu mkubwa kwenye system, kumbuka inauma sana mtu kukufanyia dharau uwapo katika eneo lako la kazi, mambo haya haya ndiyo yalipelekea Ditopile akampiga mtu risasi kisa anajua yeye ni mtu kutoka kwenye system na wengine anawaona kama vikaragosi, na watu wengi tumekua tukiwadharau polisi kwa kua vipato vyetu vinatupa kiburi.
Tusiegemee upande mmoja wa polisi, tujiulize chanzo cha polisi kukasirika ni nini? Kama yale majibizano yao tungeyasikia yote basi tungejua yule jamaa kamjibu nini polisi mpaka polisi kuchukia kiasi kile.
Hata wewe ungekua KK security ukijibiwa nyodo hata geti utagoma kufungua