Masanja akutana na Majeruhi wa Lucky Vicent nchini Marekani

Kuna kiongozi mmoja mteule wa mkoa wa kaskazini akiwaona hao watoto wanatabasamu wakiwa Marekani anaumia sana. Maana ilikuwa ni kitega uchumi chake endapo wangeendelea kuwa Mt. Meru. Kama alivyofaidika kwa wale wenzao waliotangulia mbele ya haki.
 
Wanapendeza sana. Mungu awasaidie zaidi na zaidi
 
Hiyo nguo sheria haimuhusu? Au ni ruhusa kuvaa ukiwa nje ya nchi.
Sheria za tz hazi apply huko. Bila berret, mkanda, namba(kitambulisho) na filimbi, hilo ni vazi la kawaida tuu. Kwanza nchi za wenzetu huwa hawa mind vitu vidogo namna hiyo. Kuna nchi raia anaweza kuvaa jezi ya jeshi la nchi hiyo na akakatiza katikati ya kambi ya jeshi. Ilimradi tuu isiwe full. Pia hatakama ipo full lakini ina fananafanana tuu, hakuna shida. Wenyewe wanaona ni kama uzalendo fulani na mapenzi kwa jeshi lao. Nimeyaona hayo katika nchi 3 miongoni mwa nchi kadhaa nilizowahi kufika.
 
Mungu ni mwema sana, naona wadogo zetu wana siha na afya njema sasa! Pongezi nyingi kwa waliojitoa kwenda kuwahudumia huko US.

Sent from Moto G
 
Sitashangaa jeshi likitoa taarifa kuhusu suruali aliyivaa Masanja. Inaweza kuambatana na onyo kali pia. Kosa likifanyika Marekani sheria za wapi zinatumika? Ikumbukwe hilo vazi ni la jeshi letu.
 
Hao watoto wamshukuru Mungu kwa hao Wazungu kupita hiyo njia na kuwasaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…