Nadharia pandikizi
Baada ya ndoa nagundua wife bado ana mawasiliano na x wake lakini kwa viapo vya kiimani anakana katakata tena kwa kushika msahafu na kujiapiza malipizi mabaya
Katikati ya mishe za maisha x wa wife kwa hali ya utatanifu mkubwa anakuja kuwa msaidizi wangu kwenye mishe zangu .. CV yake inapewa backup kubwa na mkewangu ambaye ni x wake!
Yanatokea mengi machache yenye viashiria vya mwendelezo wa mahusiano lakini kwa taswira yangu mbele ya jamii inabidi nilitatue hili kwa umakini wa hali ya juu.
Kutokana na majukumu ya msaidizi wangu kuna nyakati inabidi awe karibu na mkewangu ambaye ni x wake! Napambana kwa hali na mali ili msaidizi wangu apate mke halali wa ndoa na hilo nalifanikisha kwa weledi mkubwa
Mimi na mke wangu tunapata watoto wawili wa haraka haraka.. Lakini badala ya furaha kuongezeka ndani ya familia.. Malaika hawa wanazua balaa jipya! Zinaanza kuenea tetesi za kwamba hawa si damu yangu, lakini vilevile kukiwa na viashiria vya mwendelezo wa mahusiano kati ya wawili hawa.. Hali ni tete mno na inabidi nifanye jambo la haraka lakini kwa umakini mkubwa sana
Nakesha nikitafuta njia sahihi ya kutatua hili tatizo moja kwa moja, niliposhindwa kabisa nawatafuta wasiri wangu na kunipa mkakati wenye kuogofya lakini ukiwa ndio bora zaidi
Napewa ramani nzima na gharama zake na uhakika wa kazi! Watenda kazi husika wananihakikishia hiyo sio kazi yao ya kwanza na wananitajia mifano kadhaa.. Nashawishika kuwaamini kwakuwa wana connection mpaka kwenye sifongo.
Nawalipa kinachowahusu, huwa hawapokei nusu maana wana hakika na kazi yao! Mimi sitakiwi kuwepo wakati kazi ikifanyika hivyo natafutiwa ziara kuepusha mengi, yangu na ya jamii
Kazi inafanyika kwa ukamilifu napata taarifa nikiwa ziarani na natumiwa ujumbe wa mwendazake kwanini akaamua kufanya aliyofanya.
Kwa haraka kabisa bila kuwaza mara mbili napost mitandaoni kumtangazia msamaha mkewangu mpenzi
Halafu baada tu ya mazishi narejea kutoka ziarani na kuwasuta wambea juu ya mkewangu na ndoa yangu! Najizuia kabisa kuwataja 'wanangu'
Namna ishu ilivyopelekwa kuanzia kifo mpaka mazishi naamini kweli wale walikuwa watu wa kazi! Nawapongeza kimoyomoyo.. Halafu katikati ya pongezi natumiwa picha za malaika wawiki copyright na mwendazake!
Napata kizunguzungu kibaya
Nahisi mapigo ya moyo yakipiga kwa nguvu sana.
Nahisi koo likikauka kabisa huku meno yakitoa jasho la moto.. Masikioni kuna mivumo ya sauti za kutisha.
Natamani nipige kelele na kukimbia huku nikisema sio mimi..
Ufahamu unanirejea na kujikuta nakodolea macho zile sura.. Kwa sekunde unapita mkanda kama wa cinema mwanzo wa matukio mpaka hapo...kumbe kuna hawa walisahaulika...
Kumbe huu sio mwisho basi ni mwanzo mwingine wenye kutisha mno...ninachowaza ni future yangu hasa ile siku nitakapotiwa pingu na kupelekwa jengo la serikali.. Breaking news na nderemo za haters,🥱