Mashabiki tuwasapoti wachezaji wetu pamoja na viongozi na benchi la ufundi pamoja na matokeo ya leo

Lakini tunashinda ambayo ndo maana halisi ya mpira.
 
Reactions: Tui
Hata wa simba ana nafasi, japo ana ukuta imara sana.
 
Timu moja kubwa na bora ilikuwa ikicheza na timu ya kawaida iliyokamia na kufundwa vyema, Hatimaye mkubwa akajulikana.
 
Hata wa simba ana nafasi, japo ana ukuta imara sana.
Ishu ya ukuta kwa timu zote mbili ni zote hazijaruhusu goli, ila kwenye kucheza kitimu Yanga wameonekana wapo kitimu zaidi. Kuna maelewano kwanzia kwa goli kipa, mabeki, viungo hadi kwenye safu ya ushambuliaji. Mechi ya Yanga vs Azam mashabiki wengi waliina Azam ni mbovu kutokana na mpira mbovu wanaocheza na hao hao mashabiki wakatoa maoni kuwa Singida ni timu bora kuliko Azam. Hii analysis imefanywa kwavile Singida kamsumbua Simba huku Azam akionekana kuzidiwa kwa kila kitu na Yanga. Lakini mwisho wa siku huyo Singida kafungwa, na pia aina ya mpira waliokutana nao Simba mbele ya Yanga ndio vile vile kama ilivyokuwa kwa Azam, Simba ikashindwa kutandaza mpira zaidi ya kubutua butua uende mbele. Ligi ni mbio ndefu inayohitaji muendelezo wa ubora, kikosi imara kinachofanya uweze kufanya rotation, na mwisho ni kukusanya point kwa kila mechi ni tofauti na ilivyo kwenye ngao ya jamii.
 
Manula mgonjwa
Enock mgonjwa
Luis hajarud ktk pick yake
Phiri bado hajarud ktk ubora wake
Niishie hapa,

Simba baada ya mechi kadhaa

Kuna mtu atakula 5
 
Kujiamini kupita kiasi kumewaponza[emoji1787]

Wacha wajifariji mana watasema nini tena?
 
Ndio wachambuzi wenu hao [emoji1787]

Mtu kaingia dk za mwisho alafu kamficha aliyeanza kipindi cha pili,
Labda tu niambie ni muda gani Simba walicheza mpira hata kwa dakika 8 tu. Kama Mkude hakuweza kumzidi Ngoma inamaana baada ya kutoka Mudathir na kuingia Mkude, Simba walitakiwa wauchukue mchezo. Sasa kama hilo halikutokea hilo maanake bado tatizo lilikuwa pale pale.
 
Manula mgonjwa
Enock mgonjwa
Luis hajarud ktk pick yake
Phiri bado hajarud ktk ubora wake
Niishie hapa,

Simba baada ya mechi kadhaa

Kuna mtu atakula 5
Hilo factor umeona upande mmoja pekee? Je umejiuliza swali kuwa ule mpira umechezwa na wachezaji waliofundishwa na kocha ambaye hata miezi mitatu hajafikisha tokea apewe timu.
Timu haijacheza mechi kubwa ya kirafiki hivyo bado kocha hajapata kile alichokitaka tofauti na timu yenu imeenda uturuki na imecheza mechi zaidi ya mbili ya kirafiki.
Yanga imeuza mchezaji muhimu Simba haijauza mchezaji muhimu na kocha ndio yule yule lakini mpira unaochezwa ni kama vile ni watu wasiojuana kabisa.
Kwahiyo kama ishu ya kuimarika basi wachezaji wa Yanga wataimarika zaidi kwasababu kocha ndio kwanza mgeni japo performance ilikuwa ni ya juu.
 
Hakika, ila katika kujirekebisha timu zote na makocha zinaweza jirekebisha.Simba ina wachezaji wazuri tu labda wawe na kocha wa hovyo.
 
Mpira matokea hayo mambo ya control sijui stamina huwezi kuyapata ukiwa avic town.
 
Mpira matokea hayo mambo ya control sijui stamina huwezi kuyapata ukiwa avic town.
Sijui hata ulitaka kusema nini? Yaani stamina na control unasema huwezi kupata ukiwa Avic town lakini hao waliokuwa Avic town ndio walikuwa na stamina na control kuliko waliokuwa Uturuki na Tunisia. Timu haibutui mpira hata kama mpira upo golini kwao wanaanza moja moja hadi golini kwa mpinzani. Wee mpira utakuwa unasimuliwaga hauanglii
 
Huyo huyo Robertinho ameshaiumiza yanga 2 kavu Mayele akimaliza zote 90. Kila mechi ina plan yake
Acha dharau
 
Reactions: Tui
umeongea kiuwanamichezo, mpira una matokeo matatu kushindwa, kufungwa na kutoa draw. Kwa sababu hii ilikuwa fainali mshindi ilikuwa lazima apatikane. Hata kukubali matokeo pia ni ushindi mkubwa.
 
Reactions: Tui
Nyota njema huonekaa asubuhi, pongezi kwa wachezaji, mashabiki, uongozi na benchi la ufundi tunakoeelekea ni pazuri zaidi.
 
Nilikuonya tokea mechi ya ngao ya jamii ulikuwa mbishi ila mwisho wa siku mkatulizwa na mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…