Kocha Robertinho atimuliwe Sasa, mnasubiri hadi Yanga iongoze ligi tofauti ya points kumi? Hatupendi makelele huko mbele fanyeni maamuzi magumu si mmeona Kwa macho yenu timu hamna! Simba inacheza kama ndondo cup!
Ligi inaanza timu ya Simba Haina fomesheni Wala possession, na usijidanganye kuwa itabidilika pale ndio uwezo wa Robertinho ulipoishua, Yani dkk moja tu Simba hawawezi kukaa na mpira, sio derby tu hata walipocheza na Singapore Big Stars ulimi nje!
Beki na midfielders wa Simba Kila mmoja anacheza kivyake timu nzima wanakimbia kimbia na kukaba tu, hadi Mkude kaonekana Bado ni Gold!!Kila mchezaji anacheza kivyake timu nzima, hujui mpira Unatoka Kwa nani unaenda Kwa nani ni kujipigia pigia tu aibu sana!
Kibu D anakimbia kimbia na kukukuruka tu kama chizi yuko alone, akijaribu juhudi binafsi aifunge Yanga asifiwe, ila Beki line ya Yanga Kali usipime!
ukweli Simba wameingia mtumbi wa vibwengo , Kwa Robertinho kocha hamna! Huu ni ukweli mchungu, nadhani Kuna fitna Yanga wamefanya kuingilia mchakato wa kocha Simba ili Simba iendelee kuwa mbovu mno kama Jana roho mkononi dkk 90 ni Yanga tu wameshindwa wenyewe no Mayele Jana angekuwepo Simba wangekufa hata nne bila!