Mashabiki wa mikoani sapotini timu zenu na punguzeni unyonge na kuwa vibaraka wa timu kubwa

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Mimi ni mpenzi wa mpira wa ushindani. Sipendi timu ninayoshabikia ishindeshinde kwa kubebwa au kwa njia za mkato. Ushindi mtamu ni ule wa kutolea jasho.

Ningependa sana ligi kuu ya Tanzania iwe na timu imara za mikoani zinazotoa ushindani wa kweli kwa timu kubwa. Huwa sipendi ninapoangalia msimamo wa ligi kila msimu, unakuta baada ya mechi 10 hadi mwisho wa ligi, msimamo unagawanyika vipande vitatu. Timu 2 au mara moja moja 3 za juu zinagombania ubingwa na kila msimu ni zile zile tu, timu 4 zinagombania nafasi ya 3 na ya 4 halafu zilizobaki zooote zinapambana zisishuke daraja. Hapa ni dalili kuwa ushindani katika ligi una shida.

Mimi nadhani watu wa kwanza wanaoziangusha hizi timu ni mashabiki walioko huko mikoani. Tujenge utamaduni mpya, kama uko mkoa fulani na ndiyo asili yako hapo au umeamua kujenga makazi yako ya kudumu hapo, jenga utamaduni wa kushabikia timu ya hapo. Nunua jezi, nenda kiwanjani kila inapocheza na achana na haya matimu makubwa hata kama ulirithishwa. Ukiona viongozi wako wanajiwekaweka karibu na timu fulani kubwa, paza sauti na kemea au isusieni kabisa hiyo timu hadi viongozi wajifunze.

Taasisi na makampuni yaliyoko mikoani pia yapewe hamasa na kuwe na utaratibu wa kuchangia na kusapoti timu za mikoa walipo (in exchange wapewe fursa rahisi za kujitangaza) na hizi hamasa zisisubiri tu wanapocheza na Simba au Yanga ila iwe ni zoezi endelevu.
 
Kuna msemo mmoja unasema Mpira Pesa.

Je huko mikoani ambako mlishindwa kumpeleka Biashara United kule Libya akacheze Na al ahly tripoly mtaweza kupambana na miamba kama Azam na Simba kwenye harakati za kujiweka juu?
 
Simba na yanga wamekuwa wakoloni kwenye ligi yetu! Watu wa mikoani ni ushamba unawasumbua huwaambii kitu kwa iz timu za kkoo
 
Kuwa wa mkoani haimaanishi hutaki amani ya moyo. Penda kipendacho moyo hata kama kipo Mwezini.
 
Watu tunashangiliana team iko ulaya na bado maisha yanaenda.
Mpira Hauna mipaka kama wameamua kushabikia team za kariakoo hakuna shida ndio mpira
 
Mfano wako ndiyo msingi wa hoja yangu. Inakuwaje timu inapata nafasi ya kuwakilisha kimataifa halafu inakosa sapoti ya kueleweka kifedha hadi inashindwa kusafiri?

Makampuni ya migodi na mengine yaliyopo kanda ya ziwa ukiachilia mbali wenyeji wa kanda hiyo walio na pesa zao wakiunganisha nguvu kukawa na utaratibu endelevu ulio na faida kwa pande zote, hayo ya Biashara United hayatakiwi kutokea.
 
Simba na yanga wamekuwa wakoloni kwenye ligi yetu! Watu wa mikoani ni ushamba unawasumbua huwaambii kitu kwa iz timu za kkoo
Sahihi kabisa ila hili tunaweza kulibadili.
Kuwa wa mkoani haimaanishi hutaki amani ya moyo. Penda kipendacho moyo hata kama kipo Mwezini.

Watu tunashangiliana team iko ulaya na bado maisha yanaenda.
Mpira Hauna mipaka kama wameamua kushabikia team za kariakoo hakuna shida ndio mpira
Jasiri Haachi Asili uhurumoja Mambo mengine tunafanya kwa mazoea ila ukishaelimishwa ukaona hasara za kile unachokifanya unabadilika.

Waarabu wako tayari kufanya mafigisu yote tunayoyashuhudia kila siku kwa sababu kuna faida nyingi za kiuchumi wanazopata moja kwa moja zinazotokana na timu zao kufanya vizuri.

Nafikiri nyie mnaangalia tu katika angle ya ushabiki wa mpira. Ukiweka angle ya uchumi na faida zake za moja kwa moja kwa wakazi wa mikoani utakaotokana na timu zao kufanikiwa mtanielewa.
 
Ungeanza kwanza wewe kuisapoti, kuipenda na pia kushabikia timu yako ya Mkoani, badala ya simba! Ili wengine nao wakufuate. Nje hapo, ni unafiki tu.
 
Utashangaa watu wa Bukoba wanainyanyasa Kagera sugar kils ikicheza na Yanga au Simba. Fedha ya kumuonga refa inachangishwa ili atoe penati au abinye kuotea. Watu wa Kagera hawajui kwamba bila Kagera Sugar hawataiona Simba wala Yanga.
 
Mimi ni mpenzi wa mpira wa ushindani. Sipendi timu ninayoshabikia ishindeshinde kwa kubebwa au kwa njia za mkato. Ushindi mtamu ni ule wa kutolea jasho.

Ningependa sana ligi kuu ya Tanzania iwe na timu imara za mikoani zinazotoa ushindani wa kweli kwa timu kubwa. Huwa sipendi ninapoangalia msimamo wa ligi kila msimu, unakuta baada ya mechi 10 hadi mwisho wa ligi, msimamo unagawanyika vipande vitatu. Timu 2 au mara moja moja 3 za juu zinagombania ubingwa na kila msimu ni zile zile tu, timu 4 zinagombania nafasi ya 3 na ya 4 halafu zilizobaki zooote zinapambana zisishuke daraja. Hapa ni dalili kuwa ushindani katika ligi una shida.

Mimi nadhani watu wa kwanza wanaoziangusha hizi timu ni mashabiki walioko huko mikoani. Tujenge utamaduni mpya, kama uko mkoa fulani na ndiyo asili yako hapo au umeamua kujenga makazi yako ya kudumu hapo, jenga utamaduni wa kushabikia timu ya hapo. Nunua jezi, nenda kiwanjani kila inapocheza na achana na haya matimu makubwa hata kama ulirithishwa. Ukiona viongozi wako wanajiwekaweka karibu na timu fulani kubwa, paza sauti na kemea au isusieni kabisa hiyo timu hadi viongozi wajifunze.

Taasisi na makampuni yaliyoko mikoani pia yapewe hamasa na kuwe na utaratibu wa kuchangia na kusapoti timu za mikoa walipo (in exchange wapewe fursa rahisi za kujitangaza) na hizi hamasa zisisubiri tu wanapocheza na Simba au Yanga ila iwe ni zoezi endelevu.
Timu kubwa itabaki kuwa timu kubwa
 
Simba na yanga wamekuwa wakoloni kwenye ligi yetu! Watu wa mikoani ni ushamba unawasumbua huwaambii kitu kwa iz timu za kkoo
Wewe hushabikii timu za ulaya? ,Kutoka mikoani mpaka dar nakutoka Tz mpaka ulaya wapi mbali
 
Akili kubwa sana ila kwa bongo hatua ya kwanza ni kuziua Simba na Yanga tuanze upya.
 
Back
Top Bottom