Mashabiki wa Urusi wanavyoswitch habari ziende wanavyotaka wao na wasikilize wanachotaka wao (walidharau Mwiba mguu waanza kuoza)

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Habari za wanandugu hapa!

Wakiwa wamekufa wanajeshi zaidi ya 10,000 wa Urusi na 2600 wa Ukraine na raia 5200 wa Ukraine, Hakuna aliyeamini Kama Kuna Kifaru cha Urusi kitaguswa wala hakuna aliyeamini kama Urusi ataruhusu hata majeshi wake mmoja kuuwawa huko vitani, maana wengi walilibeka kiushabiki na kujipa scale ya 72 hours kufika Kiev na kuangusha Serikali, wakati tunaongea Hapa kuna watu walisema bwana mkubwa Putin kashaweza zana on high alert na mbaya zaidi yeyote atakayeingilia vita ataona cha mtema kuni Hahaha sasa hakuna cha mtema kuni wala nyasi, Leo hii hata Poland anaingilia vita anatoa msaada UKRAINE , hata Estonia kanchi kadogo kanatia msaada wa vifaa na majeshi, sasa Mbona hasemi tena

Okay ndo maana tunasema

Maisha yapo katika kasi yake inayotuacha kila siku.
Wakati vita inaanza tulikua tunasikia Russia hivi, Russia vile. Yaani ilikuwa kama vile wameenda Ukraine kwenye matembezi ya Mshikamano au mbio za mwenge au kwenye Goba Marathon...ilikuwa kama vile Ukraine wote wameikumbia nchi baada ya kusikia Russia wanakuja.

Baada ya wiki moja kupita na kibao kugeuka, taarifa zikabadilika, mara Russia anashinikiza kufanyika kwa mazungumzo ya kumaliza vita, mara wameanza kufa, mara kile.

Watu walewale waliokua wakiwacheka Ukraine, wakaanza kuzishambulia medias zilezile kuwa zinapotosha.

Sasa hivi hawataki tena kusikia habari za vita hadi iwahakikishia kwanza habari hiyo itaelezea mafanikio ya Russia

Britanicca
 
Unaweza nieleza unaelimu gani kuhusu vita. Kama sio vita diplomasia ya nje.

Unaweza nieleza ulishawai kuandikia ripoti vita gani kati ya vita zilizotokea.

Kijana huko tandale ujuaji na porojo za urusi na ukraine
Dogo umjui britanicca ndo maana unaongea tu bila kujua whom you are talking to
 
Hizo takwimu umepata wapi wakati official figure raia waliokufa 1,437 wewe unatoa 5000+ lakini pia hujatoa vyanzo vya taafifa zako ni kipi. Acheni propaganda ya vita visivyokuhusu.

badala yake Fikiria namna ya kupambana na gharama za maisha zilizopanda namna gani utasaidia familia na jamii yako.
 
Familia yangu haipo huko Nangurukuru ipo huku katika mikono salama usinilinganishe nawe kukaa kujadili mambo ya harmonize na kajala Au stive NYERERE na usemaji, ninaizungumzia hii vita Nina maslahi pana nayo
 
Pambana na garama za gesi na chakula zilizopanda huko uliko.

A person livining in Europe or Amercia should be well informed na mwenye kujua kuandika vema sio kwa utumbo huu ulioandika hapa bora hata na mtu wa matombo anaweza kuandika vizuri kuliko unaejinasibu kukaa huko ulipo.

Tatu nilifikiri kukaa huko ulipo ungeelimika zaidi but unaonekana sawa na wacheza vigodoro wa kule ngamiani Tanga. Andiko halina reference ni sawa na waimba taarabu za kuchambana wakwe wenza
 
Ili habari ya CCN na BBC iwe ya kweli kwao iandike Drone ya Ukraine yadunguliwa na Askri wa Urusi", hapo meno 34 yote nje kwa KICHEKO na watajaza katika hiyo thread kama kumbikumbi😂😂.
ila ikiandika", vifaru vya Urusi vime-towed kwa KUKOSA mafuta!!!, wewe ulieleta habari utashambuliwa na chanzo chako habari.
 
Urusi kwa ujuha walioufanya wametuacha pabaya sana dunia hii, siku zote tuliwategemea uwepo wao kama wababe wa Marekani, ili kuwe na balance of power duniani, wangeendelea kuficha udhaifu wao tuendelee kuwaogopa, sasa wameshonyesha walivyo hovyo, Marekani ameachwa pekee yake kama mmiliki wa dunia, hata Waarabu waliokua wanamtegemea Urusi, kwenye hili wamepiga kimya kwa mshtuko.
 
Wakati Russia inashinda vita kwenye uwanja wa Mapambano,Ukraine inashinda vita kwenye vyombo vya Habari vya Magharibi!
Asikwambie mtu Ukraine imeharibiwa vibaya sana kiasi kwamba itachukua muda mrefu kurudi katika hali yake ya kawaida! Tusidanganywe na habari za Uongo za Vyombo vya Nchi za Magharibi.
 
Habari za wanandugu hapa!

Wakiwa wamekufa wanajeshi zaidi ya 10,000 wa Urusi na 2600 wa Ukraine na raia 5200 wa Ukraine, Hakuna aliyeamini Kama Kuna Kifaru cha Urusi kitaguswa wala hakuna aliyeamini kama Urusi ataruhusu hata majeshi wake mmoja kuuwawa huko vitani, maana wengi walilibeka kiushabiki na kujipa scale ya 72 hours kufika Kiev na kuangusha Serikali, wakati tunaongea Hapa kuna watu walisema bwana mkubwa Putin kashaweza zana on high alert na mbaya zaidi yeyote atakayeingilia vita ataona cha mtema kuni Hahaha sasa hakuna cha mtema kuni wala nyasi, Leo hii hata Poland anaingilia vita anatoa msaada UKRAINE , hata Estonia kanchi kadogo kanatia msaada wa vifaa na majeshi, sasa Mbona hasemi tena

Okay ndo maana tunasema

Maisha yapo katika kasi yake inayotuacha kila siku.
Wakati vita inaanza tulikua tunasikia Russia hivi, Russia vile. Yaani ilikuwa kama vile wameenda Ukraine kwenye matembezi ya Mshikamano au mbio za mwenge au kwenye Goba Marathon...ilikuwa kama vile Ukraine wote wameikumbia nchi baada ya kusikia Russia wanakuja.

Baada ya wiki moja kupita na kibao kugeuka, taarifa zikabadilika, mara Russia anashinikiza kufanyika kwa mazungumzo ya kumaliza vita, mara wameanza kufa, mara kile.

Watu walewale waliokua wakiwacheka Ukraine, wakaanza kuzishambulia medias zilezile kuwa zinapotosha.

Sasa hivi hawataki tena kusikia habari za vita hadi iwahakikishia kwanza habari hiyo itaelezea mafanikio ya Russia

Britanicca
Wewe ni mtoto wa ngapi wa mchungaji Zumaridi?
 
Kati ya Ukraine anayetembezewa kichapo mwanzo mwisho na Urusi ambaye hajapoteza raia hata mmoja nani analia kama mama mwenye uchungu? [emoji16]
Mwanajeshi sio raia?
Screenshot_2022-03-25-20-35-20-861_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
 
Back
Top Bottom