Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Katika kuelekea World Press Freedom Day, ambayo huadhimishwa kila tarehe 3 Mei, waandishi waliandaa marathon ya kilomita 10. Mbio hizo zilifanyika Dodoma ambao wanatasnia wa habari wamekusanyika kwa ajili ya kuipamba siku ya uhuru wa habari duniani.
Mbio hizo zimefanyika Mei Mesi, na zilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma. Hata hivyo Mzee Mashaka Marura, ameonesha umwamba kwa kuwa mbele ya msafara katika marathon hiyo tangu mwanzo hadi mwisho na bado alikuwa anaonesha ana nguvu na shauku ya kuendelea kukimbia.
Mashaka aliwataarifu wanahabari kuwa yeye hukimbia walau kilomita kumi na moja, kwa siku. Na yuko vizuri kiafya mbali na umri wake mkubwa wa takriban miaka 91 maana amezaliwa mwaka 1933. Mzee Mashaka amesema yeye mara yake ya mwisho kwenda hositali ilikuwa ni miaka sita iliyopita.
Mzee huyu ambaye sasa anaishi kwa kukimbia tu, maana aliacha biashara ndogondogo alizokuwa anafanya awali. Kupitia riadha mzee Mashaka amekuwa akiwahamasisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi kwa kushiriki kwenye marathon zao.
Tanzania, inayokabiliwa na magonjwa mengi yasiyoambukiza wana mengi ya kujifunza kutoka kwa mzee Mashaka, aidha kufanya watu wengi waone mazoezi ni moja kati ya tiba adhimu ambaye inabidi iwe njia ya maisha
Picha 1: Mzee Mashaka akiwa na mmoja wa waandishi walishiriki marathon Dodoma
Mzee Mashaka akiwa kwenye finish line ya marathon baada ya kumaliza mbio