Mashaka Marura: Mzaliwa wa 1933 ambaye bado yuko fiti, awathibitishia waandishi Dodoma

Mashaka Marura: Mzaliwa wa 1933 ambaye bado yuko fiti, awathibitishia waandishi Dodoma

Kabla hujawalaumu waandishi wewe ushawahi jitokeza kusemea yale unayoyaona sio sawa? Waandishi ni binadamu kama wewe wenye kulinda maisha yao kwa wivu mkubwa. Au mnataka wajitoe mhanga ili nyie waoga mseme walikufa kishujaa?
We sijui wa wapi wewe! Nijitokeze nisemee wapi ni visemeo mimi? Mimi sikusomea uandishi wa habari kwa hiyo jukumu langu la awali sio kuwasemea wananchi ila ni kutenda niliyoajiriwa/kujiajiri nayo. Waandishi wamesomea na wanajukumu la kimsingi kufanya hayo.
 
We sijui wa wapi wewe! Nijitokeze nisemee wapi ni visemeo mimi? Mimi sikusomea uandishi wa habari kwa hiyo jukumu langu la awali sio kuwasemea wananchi ila ni kutenda niliyoajiriwa/kujiajiri nayo. Waandishi wamesomea na wanajukumu la kimsingi kufanya hayo.
Basi tuliza kinyeo hicho kama huwezi kuongea chochote.
 
Katika kuelekea World Press Freedom Day, ambayo huadhimishwa kila tarehe 3 Mei, waandishi waliandaa marathon ya kilomita 10. Mbio hizo zilifanyika Dodoma ambao wanatasnia wa habari wamekusanyika kwa ajili ya kuipamba siku ya uhuru wa habari duniani.

Mbio hizo zimefanyika Mei Mesi, na zilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma. Hata hivyo Mzee Mashaka Marura, ameonesha umwamba kwa kuwa mbele ya msafara katika marathon hiyo tangu mwanzo hadi mwisho na bado alikuwa anaonesha ana nguvu na shauku ya kuendelea kukimbia.

Mashaka aliwataarifu wanahabari kuwa yeye hukimbia walau kilomita kumi na moja, kwa siku. Na yuko vizuri kiafya mbali na umri wake mkubwa wa takriban miaka 91 maana amezaliwa mwaka 1933. Mzee Mashaka amesema yeye mara yake ya mwisho kwenda hositali ilikuwa ni miaka sita iliyopita.

Mzee huyu ambaye sasa anaishi kwa kukimbia tu, maana aliacha biashara ndogondogo alizokuwa anafanya awali. Kupitia riadha mzee Mashaka amekuwa akiwahamasisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi kwa kushiriki kwenye marathon zao.

Tanzania, inayokabiliwa na magonjwa mengi yasiyoambukiza wana mengi ya kujifunza kutoka kwa mzee Mashaka, aidha kufanya watu wengi waone mazoezi ni moja kati ya tiba adhimu ambaye inabidi iwe njia ya maisha

View attachment 2978238
Picha 1: Mzee Mashaka akiwa na mmoja wa waandishi walishiriki marathon Dodoma


View attachment 2978248
Mzee Mashaka akiwa kwenye finish line ya marathon baada ya kumaliza mbio​
Safi umri namba tu.
 
Daa, ngoja nianze kutafuta mashine ya kukimbia, maana huku mtaani unaweza ukaitwa chizi
 
Atakuwa hajaowa ndiyo maana anaishi kwa Amani hadi kuweza kufukisha miaka hiyo.
 
Anaweza kufikisha hiyo miaka Maana mwaka 1998 alikuwa anatuuzia uzia pipi na karanga shuleni hapo Dodoma na kwa kumkadiria umri wake kwa miaka hiyo alikuwa na miaka zaidi ya 50
 
Back
Top Bottom