Mashambulizi dhidi ya Magufuli: Michezo au upepo wa kisiasa?

Hivi wewe umetoroka lindo la kulinda kaburi Chato?

Saa hizi ni saa 10 midnight bado unamlilia mtu keshaoza kwenye hilo kaburi unalolinda?

Hivi mtajiliza mpaka lini? wakati mwenzenu Janeth kashukuru yule Ibilisi kuondoka sasa hivi ananawiri.
Hoja yako nn bwashekhe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona mtu anamtukuza dikteta Magu jua ni msukule. Unawezaje kuacha kuona uovu wa Magufuli kama wewe siyo msukule? Kiongozi ambaye hakuficha uovu wake kwa kauli na kwa matendo!
Kama mtu haoni mazuri na makubwa aliyofanya JPM ingawa kuna mabaya ambayo yalifanyika ili mazuri yatamalaki, Huyo ni mpuuzi wa kupuuzwa. Wezi walitwaliwa walizoiba, waliomtukana walitandikwa 30! Hiyo ni katika kufanya hayo makubwa unayoyashuhudia. Hata Yezu alisulibiwa msalabani ili wanadamu (walio wengi) waokolewe. Upo Mpaka hapo
 
Mama anamalizia miradi iliyoachwa na mtangulizi wake ambaye aliiacha ikiwa chini ya asilimia 10 kiuendelezo,unaposema eti ndani ya mwaka mmoja ajafanya kitu ni KICHEKESHO,kumbuka miradi ni MINGI na nimiradi mikubwa yenye uhitaji wa fedha nyingi sana,mlitaka aiache aanzishe mipya?, kumbukeni baadhi ya miradi iliyoachwa baadhi imekamilishwa na mingi imefikia katika hatua nzuri sana kwa kuifikisha juu ya asilimia 50%.
MNAPOSEMA HAJAFANYA KITU MNATUSHANGAZA SANA WENYE AKILI TIMAMU.
 
Miradi ipi ilikuwa chini ya 10%?
 
Vituo vyote, mpaka vituo hewa. Jiwe aliwaondoa akili za kufikiri, mme bakiwa na mafuvu tu. Hizo forehead mmeachiwa za kupasulia nazi. Ndiyo sababu mnaunga mkono kupita bila kupingwa.
Tuwekee hapa vituo vitano na matokeo yake.
 
Zitto naye yupo kwenye kundi la wanaolamba asali, lazima ajipendekeze zaidi kwa wenye mzinga.
 
Hivi wewe umetoroka lindo la kulinda kaburi Chato?

Saa hizi ni saa 10 midnight bado unamlilia mtu keshaoza kwenye hilo kaburi unalolinda?

Hivi mtajiliza mpaka lini? wakati mwenzenu Janeth kashukuru yule Ibilisi kuondoka sasa hivi ananawiri.
Sijatoroka, nipo ninalinda mkuu.

Halafu nani alikuambia kunenepa ni kunawiri?
 
Wapigaji na waovu wote hakuna jema wanaloweza kuliona kwa JPM.
 
Walikuwa wameshatengenezewa mitaji kitambo wao walisimamia yale yote ambayo watangulizi wao walishayapanga halafu kule kwa wenzetu sheria zinaheshimiwa sana hata mtoto wa miaka kumi anaweza kuongoza kwa ujasiri mkubwa kwa sababu taasisi zao zinafanya kazi barabara.
 
Amefanya vibaya wakati wa utawala wake sasa watu wanafunguka.
 
Ndugu,
Hoja duni za waliokuwa waimba mapambio hazina uwezo wa kufunika na kuficha udhalimu wa mungu wa Burigi.
Ili nchi hii isafike lazima madhambi yake yawekwe hadharani, ili hata wale/wananchi waliokuwa wanaimbishwa nyimbo za kusifu ushetani wafumbuke macho na kuujua tena maana ya kuwa na uhuru wa kweli pamoja na kupata haki zao.
 
Samia hajatengenezewa mitaji na anaongoza vizuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…