Masharti gani ya ajabu umewahi kupewa na Mwenye Nyumba wako?

Masharti gani ya ajabu umewahi kupewa na Mwenye Nyumba wako?

Kuja usiku mwisho saa kumi na mbili jioni geti linafungwa, kupiga muziki kinyume na dini ya mwenye nyumba, chooni kwenda na maji tu marufuku tishu na karatasi.

Mipiko yenye harufu nzuri kama pilau na mikarangizo mingine ni marufuku. Ndio maana sikupenda kupanga nyumba ambayo mwenye nyumba anaishi humo ni kero tupu
 
Kwamba mipiko mitamu hapana
 
Yaan tulikua dini tofauti wakawa wanakuja kupondea dini yangu sijui ya uongo na hapa na pale, afu pale home palikuwa na mabinti wakawa wanaleta ngenga mingi mingi na ujinga flan [emoji16][emoji16]nkapiga tukio baada ya pale hadi familia ile ikajua mm ni mpangaji sio mwanafamilia
Wao ni manabii au mitume? [emoji848]
 
Miaka iyo nipo mwanza chuo nikapanga nje mashart hakuna kupika kitimoto yule mama kutokea uko ukerewe sijui alikuwa mshirikina, anajikuta mswali sana alafu anauza pombe za kienyeji pale kwake, mara usiku anakwambi msitoke nje anakuja na watu wake wanamwaga dawa nyumba nzima sijui wanakuaga uchi,

Si tukawa tunapika kama kawa tena afuta ya kupikia mboga ni ya kitimoto , tukikosa hata utumbo wa kitimoto tunarost tunakula mi na wanangu tunapika kilo nnee nzima ugali mkuubwa kila wikiend tunachuja mafuta lita nzima aliongea adi akachoka
 
Nilipokuwa nimepanga Mkoani Mwanza Baba mwenye nyumba alinipa sharti la kuoa kabla kodi ya mwezi mmoja haijakamilika maana nililipia miezi sita, basi mwezi ulipokamilika nikawa bado sina mke akataka kunitimua nikamwambia anirudishie kodi nikatafute chumba sehemu nyingine pia anipe siku tatu za kujiandaa kuhama akakubali ila alinikata hela ya mwezi mmoja.

Nilipopata chumba tu nikahama kabla hata ya siku tatu hazijakamilika tena nilihama na binti yake,

Alinitafuta mitaa yote mpaka akanipata nikamkaribisha kama baba mkwe naye hakuwa na jinsi ikabidi anipe baraka zote Kama mkwe wake kishingo upande mpaka sasa napeta na mwanae lydia

ILA KUPANGA RAHA..
 
Back
Top Bottom