Masharti mapya ya NASA kwamba waruhusiwe kuingia kwenye server za IEBC

Masharti mapya ya NASA kwamba waruhusiwe kuingia kwenye server za IEBC

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Hili wamesema kwamba wakiruhusiwa kuingia na kufungua server za IEBC, basi watakubali kushindwa.
Mimi binafsi naona kama washauri wa Raila watakua wanamdanganya na kumzungusha zungusha mzee wa watu.

Kwanza alisimama juzi na kutuonyesha stakabadhi alizoita logs za kuonyesha kwamba mfumo umedukuliwa, wataalam tulioangalia kwa makini hayo makaratasi ilikua aibu tupu maana zilionyesha ni bootlogs za server aina ya MS SQL 2008 ambayo ni mfumo uliopitwa na wakati, wengi tunajua kwamba IEBC wanatumia Oracle.

Wamekua wakituhumu mambo mengi mara udukuzi mara kile mara hiki, hii imepelekea IEBC kuwaomba waje na makarani na mawakala wao na wana habari na wachunguzi wa kimataifa wakague dodoso/fomu zote moja baada ya nyingine lakini bado haitoshi.

Kwa wao kwenda kwenye server sidhani kama patakua na jipya. Maana hata takwimu walizotuonyesha kwamba wamepewa na jasusi aliye ndani ya IEBC, ukitumia kikotozi/calculator humo kuna makosa mengi kwenye kujumuisha, itakua aliyewapa labda hata naye kapewa na ili awaanike, maana hawakukawia kwanza wahakikiki, walielekea moja kwa moja kwenye vyombo vya habari.



NASA sets term for conceding, asks for access to IEBC servers
 
Kama IEBC wamezijumlisha form 34A na 34B mbele ya kila mtu na matokeo bado yanaonyesha wamepigwa chini .... kwa kweli NASA inabidi wasalimu amri!! Otherwise, huo utakuwa ni uvunjaji wa amani!!

Ngoja tusubiri mkutano wa makamishna wa IEBC na wasimamizi wakuu wa wagombea wamalize mkutano tujue mbichi na mbivu .... by saa 1:30 usiku!!
 
Odinga's party NASA may have lost most seats and also the presidency but they should not give up on this country because the opposition plays a critical role in Kenya's development...hatutaki Kenya iwe rais anashinda 99% of the vote kama Rwanda..a backward decomcracy....ushindani ni kitu nzuri...how do you win 99% if u are not a dictator? bila shaka huyu jamaa nikama hataki opposition kule Rwanda...
 
Vipi wakiingia kwenye server wakabadilisha matokeo?

Huku Tanzania Ukawa hatukuruhusiwa hata kutoa sharti lolote,yaani matokeo yaliyopikwa na mafebruari manyuzi ndo yakatumika na hakuna kuandamana.

Hii ni demokrasia au uwoga wa vurugu za Odinga na mashabiki wake?
 
Back
Top Bottom