Mashauri sita yaliyosababishwa na Serikali ya John Pombe Magufuli: Kugharimu mabilioni ya kodi za Watanzania

Mashauri sita yaliyosababishwa na Serikali ya John Pombe Magufuli: Kugharimu mabilioni ya kodi za Watanzania

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
855
Reaction score
1,224
Habari Wana JF,

Bila shaka wengi mnafahamu kuwa Serikali ya Tanzania maarufu kama Serikali ya Magufuli ilitenda kwa kutanguliza nguvu, vitisho na weledi duni hasa katika kudeal na majadiliano ya kibiashara na wawekezaji mbalimbali.

Matumizi ya nguvu yalichagizwa zaidi na kutungwa kwa sheria maarufu mbili, ile ya Uhujumu Uchumi na Maliasili, ambapo Rais na watendaji wa Serikali walijipa mamlaka ya kutatua migogoro ya usuluhishi nje ya sheria za kimataifa zinazolinda mitaji ya uwekezaji na wawekezaji.

Mashauri takribani sita yalifunguliwa na bado yapo katika hatua mbalimbali za usuluhishi, ambazo kwa kiasi kikubwa zitaweza kutafuna mabilioni ya shilingi za kitanzania.

Mashauri yaliyopo katika hatua za usuluhishi ni:
1. Sunlodges v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub.
2. Agro EcoEnergy and others v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub
3. Symbion Power and others v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub
4. Saab v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub
5. Winshear v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub
6. Nachingwea and others v. Tanzania | Investment Dispute Settlement Navigator | UNCTAD Investment Policy Hub

Kutokana na hali hii, Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria inapaswa kutoa taarifa kwa Watanzania kupitia Bunge ili kueleza hatua mbalimbali za mashauri haya, na sababu za kushitakiwa na pengine kiasi cha fidia ambacho tunaweza kulipa endapo tutashindwa.

Tanzania pays treaty award to avoid aircraft seizure​

Jack Ballantyne
30 April 2021
 
kama kuna watu wanapaswa kulaumiwa sana katika taifa hili ni kikwete na kapa, hawa waliingia mamiikataba mengi ya mabovu yatakayoligharimu taifa hili hadi kesho, kosa kubwa la magufuli ni kule kutaka kulinasua taifa katika haya mamikataba mabovu yaloingiwa na watangulizi wake na hapa ndo wasojua mambo hushabikia upumbavu
 
Ungetupa undani wa kila shauri hakika ungeitendea haki mada yako. Labda ungejiuliza ni kwa kiasi gani hayo makampuni yalisaidia kukua kwa uchumi wa nchi?

Ila kwa kukumbusha tu nyingi ya kesi hizo ni za makampuni ambayo yalitengeneza mikataba ya kifisadi nasi tukaingia kichwakichwa kwa kuwa sheria zetu ziliruhusu hali hiyo.
 
kama kuna watu wanapaswa kulaumiwa sana katika taifa hili ni kikwete na kapa, hawa waliingia mamiikataba mengi ya mabovu yatakayoligharimu taifa hili hadi kesho, kosa kubwa la magufuli ni kule kutaka kulinasua taifa katika haya mamikataba mabovu yaloingiwa na watangulizi wake na hapa ndo wasojua mambo hushabikia upumbavu
Yeye mwenye alikuwa katika serikali zote na hakuwahi kupinga wala kujiuzulu, hivyo ni wale wale tu.
 
Tatizo ni matumizi ya nguvu katika masuala yenye utaratibu wa kisheria. Ni kulikosea taifa na watanzania kuwalipisha gharama kwa matendo ya Viongozi yasiyofuata sheria na taratibu.
Rasilimali zetu lazma tuzitengenezee sheria na kuzisimamia sisi wenyewe.
 
Kwa Bunge liliopo sidhani kama wataelewa yaliyomo
Kwani hakuna njia mbadala Bunge lililopo hapana bora kuacha tu
Bunge lipi ambalo uliamini ni sahihi!
Kwa maana miaka yote linaongozwa na CCM na nyie hakuna kitu mliwahi kupitisha ila vyote huwa mnapinga na maisha yanaendelea

Sasani lipi una aminia?
 
Back
Top Bottom