Mashauri sita yaliyosababishwa na Serikali ya John Pombe Magufuli: Kugharimu mabilioni ya kodi za Watanzania

Bado tu mnamwandama marehemu? Mwacheni apumzike zake!
Hakuna anayemuandama bali watu wapo na documents zake alizo zitengeneza kwa kujua au kutokujua.
 
Hivi karibuni imezuka tabia ya kukwepa majukumu ambayo inapaswa kupingwa kwa hali na mali ndani ya nchi yetu.

Vyama vya upinzani hasa Chadema kila wanapopata matatizo kisingizio chao ni hayati rais Magufuli,!

Chadema wamesambaza mitandaoni vijana wa kumtetea Mbowe.

Kazi yao ni kuwapumbaza wanachama na wananchi kwa ujumla waone tatizo la chadema ni Magufuli wakati Magufuli hayupo na hakuwahi kuongoza chadema . Kila uzi humu Jamii forum lazima vijana wa Mbowe wataje na kutukana mwendazake!

Mwenyekiti na aliyekabidhiwa usukani wa kuiongoza Chadema ni Mbowe lakini hawataki aulizwe chochote.!!!

Kutokana na Chadema kufa kila mahali kwa kupoteza mvuto na kukimbiwa na madiwani na wabunge ,viongozi wamebuni mbinu ya kukwepa aibu hii kwa kujificha kwa hayati rais Magufuli!

Viongozi wa Chadema wakihojiwa kwa nini chama hakina ofisi watakujibu tatizo ni Magufuli.

Tundu Lisu akiulizwa kuwa yeye ni makamu mwenyekiti wa Chadema lakini kwa nini hafanyi kazi za Chadema? Bavichaa watakujibu chanzo ni Magufuli!

Bavicha ukiwauliza kwa nini kamati kuu ya Chadema wanafanyia vikao vyao kwenye hoteli za kitalii na kuacha ukumbi wa ufipa ? Utajibiwa tatizo ni hayati Magufuli!

Chadema wakiulizwa kwa nini kwenye uchaguzi mliwatosa makada wenu waliokipigania chama ,mkabadili gia angani na kutuletea mgombea urais ambaye yupo kwenye list of shame(orodha ya chadema ya mafisadi wakuu wa nchi )?
Utajibiwa tatizo ni mwendazake!

Bavicha na vijana wote mliosambazwa mitandaoni kumtetea Mbowe ,tambueni anayepaswa kuulizwa kuhusiana na mabaya na mazuri ya Chadema ni Mbowe na Tundu Lisu hao ndio viongozi wenu mliowapa ridhaa ya kuwaongoza kwa sasa.

Hayati Rais Magufuli hakuwahi kuwa kiongozi wa chadema ,hivyo kukaa mnamhusisha na kuporomoka kwa chama chenu ni kupoteza muda na kuonyesha uzwazwa wa hali ya juu.
Kuporomoka kwa Ccm wataulizwa SAMIA na Dr Nchongolo na lazima watoe majibu kwa sababu wao ndiyo viongozi wa ccm kwa sasa.
Kwa nini nyinyi hamtaki kupata majibu kwa Mbowe badala yake mnataka majibu yatoke kwa Magufuli
 
Jiwe amelitendea taifa maafa makubwa
 
Bado tu mnamwandama marehemu? Mwacheni apumzike zake!
Hawezi akaachwa tu kwani hii hasara atailipa nani?ndio maana mliambiwa kuwa legacy ya mtu inajisimamia yenyewe tu na sio kulazimishana!!kweli kwa mauozo haya hiyo legacy itasimamia wapi?na ndio maana kwa aibu walikuwa wanalipa ma bilioni yetu kimya kimya tu!!eti mwana MAPINDUZI WA AFRIKA"daaa!!
 
Jikite kwenye mada. Mbowe hapa anahusika vp??
 
Unalinasua taifa bila kufuata sheria ? Mikataba na sheria za kimataifa ? Huu sio upumbafu ?
 
Sawa inawezekana kwa upande fulani ukawa sahihi, lakini bunge si lilikuwepo walikuwa wapi kuzuia hayo?kosa la meko kubwa alifikiria zaidi kutumia nguvu bila kujua haya mambo yana utaratibu wake, na hata akiwa waziri mikataba mingi, nayo alivunja ikaigharimu/itaigharimu nchi, mfano meli ya wachina, kuna barabara ya bagamoyo!!huwezi sema unalitakia mema taifa ndio ukurupuke kuvunja mikataba tena ya kimataifa, sio yakina INGOMBAKULE, wa uvinza, kuwa utamtisha na ataufyata!!ambayo taifa lako limeingia kwa utashi wake, sio kwa kulazimishwa, kama ni ya kifisadi laumu serikali yako!Lawama zote hizi ni kwa CCM.
 
Yeye mwenye alikuwa katika serikali zote na hakuwahi kupinga wala kujiuzulu, hivyo ni wale wale tu.
unadhani kupinga na kujiuzulu ndo suluhu ya mikataba mibovu? mara ngapi wapinzani walipiga kelele bt mikataba mibovu iliendelea, ajabu anapatikana mtu wakulipigania taifa kwenye mikataba ya kinyonyaji na kifisadi eti anaonekana hafai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…