Mashauri sita yaliyosababishwa na Serikali ya John Pombe Magufuli: Kugharimu mabilioni ya kodi za Watanzania

Unalinasua taifa bila kufuata sheria ? Mikataba na sheria za kimataifa ? Huu sio upumbafu ?
Hata tundu lisu alisema hivi hivi wakati JPM akipambana na mabeberu waliokuwa wanatuibia madini yetu kupitia mikataba ya kifisadi, mwisho wa siku sheria zikabadilishwa na Acacia wakafungasha. JPM ameonyesha njia ya kutoogopa kudai haki kwa kisingizio Cha sheria za kimataifa.
 
..hawajafungasha.

..acacia ni mtoto wa barrick.

..na barrick bado yuko anadunda.

..Magu alitakiwa awafukuze hata barrick.

..pia awatemeshe usd 191 billion alizosema wametuibia.
 
Kama nimekulewa, hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano hazitoshi kusimamia madini yetu. Serikali iliyoko madarakani inaandaa mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji, je, ndio mwelekeo sahihi ambao unashangiliwa na wengi, hasa upinzani?
 
..hawajafungasha.

..acacia ni mtoto wa barrick.

..na barrick bado yuko anadunda.

..Magu alitakiwa awafukuze hata barrick.

..pia awatemeshe usd 191 billion alizosema wametuibia.
Whatever the case lakini hatuna kampuni inaitwa Accacia na Barrick aliingilia kati ili kuokoa jahazi. Kizuri tuna sheria mpya za madini ambazo Barrick na makampuni mengine yanazifuata, sheria zinazolinda maslahi ya nchi yetu. JPM angesikiliza kelele za Tundu lisu kuwa tutashitakiwa MIGA asingefanikiwa.
 
Jamani mumuache mwendazake apumzike, km kumsema na kumzogoa mmefanya sana, imetosha lol.
 
Tatizo ubongo wako ulisha gandishwa na mawazo ya jiwe
Kwa kuwa unafikiri ndani ya kisanduku kamwe hutotofautisha kati ya mbivu na mbichi au pumba na mchele.
√ Akina mama waliotuliwa ndoo kichwani hawatakuelewa
√ Madereva wa magari yaliyokuwa yanaharibika kwa barabara mbovu watakushangaa
√ Wazazi waliokuwa wanashindwa kuwapeleka watoto shule watakulaani
√ Wanachuo waliokuwa wanacheleweshwa mikopo yao, watakuponda kwa mayai viza
√ Wachaga na Wameru waliokuwa wanabamizwa gharama za usafirishaji kwa njia ya barabara watakutoa macho
√ Na kadhalika kadhaika bila kusahau uboreshwaji wa huduma ya afya
 
Kama alikuwa anatoa fedha za kufanyia hiyo mieadi sawa lkn kama ni fedha za walipa kodi nakuona bado upo utumwani.
 
Kama alikuwa anatoa fedha za kufanyia hiyo mieadi sawa lkn kama ni fedha za walipa kodi nakuona bado upo utumwani.
Kwamba miradi hiyo ni ya yeye na familia yake! Hakika akili ni nywele kila mtu ana zake.

Kwa kuwa unafikiri kipinzani, niulize tu ruzuku walizokuwa wanalipwa wamezifanyia nini Kitaifa ili hoja yako ya kubeza yaliyofanyika na Serikali iwe na nguvu.
 
Hakuna kilicjofanyika,
Namuombea mama Samia atufanyie kula khali
 
Tutashinda yote na kulipwa fidia, labda wanasheria watuhujumu kwakuwa Boss wao hayupo. Ulitaka tuendelee kunyonywa na makampuni ya kibeberu wakati tunao uwezo wa kuzalisha umeme?.
 
Hakika, inasikitisha sana.
Tatizo ni matumizi ya nguvu katika masuala yenye utaratibu wa kisheria. Ni kulikosea taifa na watanzania kuwalipisha gharama kwa matendo ya Viongozi yasiyofuata sheria na taratibu.
 
Alitukosea ndio..ila mwacheni apumzike kwa amani
 
Duuh
 
Tatizo ni matumizi ya nguvu katika masuala yenye utaratibu wa kisheria. Ni kulikosea taifa na watanzania kuwalipisha gharama kwa matendo ya Viongozi yasiyofuata sheria na taratibu.
Aliju atawaburuza kama alivyoburuza wanyonge
 
Hakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…