Mashehe wana hoja kuhusu umri wa kuolewa

Mashehe wana hoja kuhusu umri wa kuolewa

Hao mabinti Sasa hivi wanakuwa shule kwahiyo mnataka muwaoe kwanza ndio waende shule?? Ili tu mpate mabikira?? Basi na vijana waoe umr huo huo ili waoane wote wakiwa mabikira
 
Mkuu hili ni jambo kubwa sana kwangu niliweza kuleta maada humu juu ya suala hili na nimefurahi kwamba elimu imeweza kuwagusa wengine ukiwamo wewe ambae kwa sasa ni nguvu ya ziada kuelimisha wengine, nashukuru sana kwa hilo.

Ni kweli kabisa binti akifika miaka 12 na siku moja huyo aliweza kutolewa posa, kwa kipindi cha miezi sita anabaki kwao ama ukweni kuanza kufundwa majukumu ya ndoa na jinsi ya kuishi na mme wake mtarajiwa na pindi afikishapo miaka 12 na nusu anahamia rasmi kwa mwanaume aliemtolea posa na kuanza maisha ya ndoa, na ndio maana hata bikira maria alishatolewa posa kwa miezi kadhaa bila kuingiliwa na yusufu ndipo ilipozuka taharuki ni vipi kapata mimba, ni hadi yussufu alipooteshwa ndoto ndio akaelewa. haikuwa wote ni miaka 12 na nusu kuolewa wengine waliolewa wakiwa 13 hadi 15, lakini point kuu ni kwamba tamaduni ziliruhusu mwanamke kuolewa pindi anapokuwa amevunja ungo.

Kwa sheria ya kuoa binti akiwa na miaka 15 wala sioni tatizo maana wengi kama sio wote katika umri huo wanakuwa wameshapevuka, kama binti yupo nyumbani shule imemshinda, yeye anataka kuolewa, n.k. sioni sababu yoyote ya yeye kutoolewa kuliko kubaki mtaani kujihusisha na mapenzi nje ya ndoa maana kwa umri huo tayari kuna wanaume watapita nae tu.


Binti wa miaka 15 ukimuoa anaweza kuzaa na kulea wakati mwanaume anapambana kuitunza familia.

Naona umepunguza makali hapo kwenye "binti aliolewa akiwa na miaka 14 na kuendelea" ukweli ni kwamba binti akiwa na miaka 12 na nusu tu huyo anahamia kwa mwanaume ila wengine walifika hadi 14...ilikuwa ngumu sana binti mbichi aliepevuka kukosa mwanaume kipindi hicho hasa ukizingatia kuoa hata wake watatu ilikuwa kawaida
Mmmmmmhmn miaka 12 huyo ujue ni mtoto kabisa hata kama kavunja ungo.
 
Kuvunja ungo na uwezo wa kuhimili mikimiki ya uzazi ni vitu viwili tofauti Kuna maternal death mchungaji acheni ujinga wenu wakuozesha mabinti wadogo wa 12 13 afu usisahau kuwah kuvunja ungo mapema sio kua maturity
Kuvunja ungo ni hatua ya awali kabisa ya mwili kudevelop kuelekea utu uzima ila haimaanishi mtu ameshakomaa na yupo tayari kwa majukumu ya ndoa kama kusimamia bajeti za familia, kupanga matumizi, kusimamia ratiba za usafi, kushauri mume na kumliwaza, kubeba ujauzito na kulea mtoto au watoto, kushiriki shughuli za koo na familia.

Nadhani kuna elimu inahitajika hapa ili hili swala lisipotoshwe. Waarabu wanalifanya ila ni familia zenye uwezo ndizo zinakuja na matokeo mazuri ila za kimasikini ndipo shida huanza.

Zee la miaka 50 kumvulia binti wa miaka 14 nguo haijakaa sawa. Kwanza haitamuacha huyu binti salama kiakili.
 
Hii ilianza pale duniani ilipotaka mwanamke apewe nafasi ya kusoma kwanza, lakini huo SIO MPANGO WA MUNGU, tena huwezi kuwa na hoja kupinga
Ila mkuu dini yenu huwa mahubiri hayaishi bila kuzungumzia, Ngono, fuatilia mahubiri ya Shehe Kioozeo, na mashehe wengine Yaani tendo mnalipa uzito mkubwa mno. hadi leo hamuelezi kuwa Mwanamke atapewa nini huko peponi. Maana nyie mnajinasibu na mabikira 72. clips za mashehe mitandaoni ni kuhusu ngono tu
 
Ila mkuu dini yenu huwa mahubiri hayaishi bila kuzungumzia, Ngono, fuatilia mahubiri ya Shehe Kioozeo, na mashehe wengine Yaani tendo mnalipa uzito mkubwa mno. hadi leo hamuelezi kuwa Mwanamke atapewa nini huko peponi. Maana nyie mnajinasibu na mabikira 72. clips za mashehe mitandaoni ni kuhusu ngono tu
Mimi sio Muislamu ndugu yangu.
 
Ukijenga hoja kwa Biblia hata utumwa unaruhusiwa.

Wewe unakubali utumwa?
Ni kweli kabisa - hata Korani inakubali utumwa. Kwa hiyo turejeshe utumwa? Na kukatwa mkono je? Upuuzi mtupu!
Mbona mkiwa huko Ulaya hamleti hoja zenu za kidini? Mwislamu gani anaoa wake wawili au watatu huko Marekani na Canada? Thubutu
 
Wewe ndio jieleze vizuri, usiseme tu Biblia inaruhusu utumwa, toa na vifungu.
Ahaa, ulikuwa hujajieleza vizuri kwamba nijieleze kuhusu nini.


In Paul's letters to the Ephesians, Paul motivates early Christian slaves to remain loyal and obedient to their masters like they are to Christ. Ephesians 6:5-8 Paul states, “Slaves, be obedient to your human masters with fear and trembling, in sincerity of heart, as to Christ” which is Paul instructing slaves to obey their master.
 
Ni kweli kabisa - hata Korani inakubali utumwa. Kwa hiyo turejeshe utumwa? Na kukatwa mkono je? Upuuzi mtupu!
Mbona mkiwa huko Ulaya hamleti hoja zenu za kidini? Mwislamu gani anaoa wake wawili au watatu huko Marekani na Canada? Thubutu
Masheikh kibao wapo wameoa wake wanne tena wazungu walioslimu

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu amani kwenu, leo nami nimewiwa na haja ya kutoa mchango wangu kuhusu umri sahihi umpasao binti kuolewa. Mada hii imezua mijadala mingi nchini kwa sasa hasa baada ya viongozi wa kiimani wa Waislamu kupeleka hoja kuhusu umri wa binti kuolewa. Mimi nitalizungumzia hili kwa kuzingatia maandiko matakatifu (Biblia) hivyo ulinganifu wowote wa kihoja ni vema unazingatia hilo.

Kimsingi kabisa hoja ya hawa mashehe sio ya kupuuzwa tu pasipo kujenga hoja za msingi. Wanazuoni hawa wa Kiislamu wamejenga hoja yao kupitia kitabu chao cha imani, Qur'an lakini majibu yanayotolewa yanahusiana na sheria za kiserikali.

Mimi binafsi nakubaliana na hoja yao kuhusu kutazamwa upya umri wa binti kuolewa lakini ninatofautiana nao kwenye umri waliopendekeza. Hoja yangu nitaijenga kupitia Biblia ili kuleta ulinganifu wa hoja na pia kuwafumbua macho Wakristo wengi walioandika sheria za kidunia mioyoni mwao wakiikaidi sheria ya Mungu.

Nianze kwa kutazama hoja ambayo iliibuliwa na mdau mmoja NetMaster kwamba mfalme Daudi alioa binti wa umri chini ya miaka kumi. Kifungu alichorejea ni hiki:

1 Wafalme 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Mfalme Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto.
² Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe
kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto.
³ Basi wakatafuta
kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.

Maandiko hayataji umri wa binti aliyetafutwa bali yanataja SIFA zake, kijana mwanamwali. Neno lililotumika hapo ni naʿărâ ambalo lina maana hii:

Transliteration: naʿărâ
Usage:

girl, damsel, female servant

girl, damsel, little girl

of young woman, marriageable young woman, concubine, prostitute

maid, female attendant, female servant

Huyu binti kwanza ni bikra halafu mwenye umri umpasao kuolewa (marriageable young woman). Sasa umri umpasao binti kuolewa ni miaka mingapi kwa mujibu wa maandiko? Tutazame wana wa Israeli zamani za Agano la Kale, mabinti katika nyakati hizo waliolewa baaada tu ya kuvunja ungo. Huo ndio ukweli wa kimaandiko na ndio haswa Mungu alivyomuumba mwanamke.

Kumbe umri sahihi kabisa wa binti kuingia kwenye ndoa ni baada tu ya kuanza kuyaona majira yake, hiyo ikiwa ni dalili ya wazi kuwa sasa njia yake ya uzazi iko tayari. Hivyo basi kimaumbile katika zama hizo binti aliolewa akiwa na umri wa kati ya miaka 14 na kuendelea.

Hili linaweza kuleta ukakasi hii leo kwa sababu majira yamebadilika kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha, hasa vyakula. Leo hii binti anaweza kuona majira yake hata akiwa na umri chini ya miaka 11, lakini ifahamike kwamba zamani zile binti aliona majira yake kuanzia miaka 13 katika hali ya kawaida.

Kwa mujibu wa tamaduni za Kiyahudi binti alihesabiwa kuwa tayari kuolewa baada ya miaka 13 na miezi sita (twelve and one half years). Hapo posa ingepelekwa na taratibu za ndoa kuanza.

Tuone maandiko juu ya hili:

Ezekieli 16:

7 Nalikufanya kuwa maelfu-elfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, huna nguo.

7 I made you thrive like a plant in the field; and
you grew, matured, and became very beautiful. Your breasts were formed, your hair grew, but you were naked and bare.

8 Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama,
wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nalikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.

8 When I passed by you again and looked upon you,
indeed your time was the time of love; so I spread My wing over you and covered your nakedness. Yes, I swore an oath to you and entered into a covenant with you, and you became Mine," says the Lord God.

Kwenye andiko hilo Mungu mwenyewe anaonesha ni wakati gani wa kuingia kwenye agano la ndoa. Baada ya binti kuwa mkubwa (matured) pale sehemu zake za kike zinapochukua sura yake halisi na hivyo kuonesha wazi uzuri wake (baada ya kuvunja ungo) ndipo hapo binti anaweza kuolewa. Huu ndio wakati sahihi kabisa kibiblia.

Katika waraka kwa wakorintho Paulo anagusia jambo hilo:

1 Wakorintho 7:

36 Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.

36 But if any man thinks he is behaving improperly toward his virgin, if she is past the flower of youth, and thus it must be, let him do what he wishes. He does not sin; let them marry.


Kama binti amepita kipindi cha maua (she is past the flower of youth), yaani sasa amekuwa tunda, tayari kuzaa mbegu anaweza kuolewa. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyoumba. Mwanamke anaposubiri muda mrefu (miaka 18 na zaidi) huingia majaribuni na wengi huanguka dhambini.

Leo hii asilimia kubwa ya wanawake wanaoolewa tukisema ukweli kwa mujibu wa maandiko ni retired prostitutes! Najua neno hili ni gumu lakini maandiko yako wazi, mwanamke siku anapofunga ndoa zisipoonekana alama za ubikira, alikuwa akifanya ukahaba nyumbani kwa baba yake. Sasa ili kuhakikisha mabinti wanaolewa katika ubikira wao walipaswa kuolewa katika umri mdogo.

Wamarekani wameiwekea dunia umri wa kijana kufikia utu uzima kuwa ni miaka 18, lakini jambo hili halipo kimaandiko. Wakristo wengi pasipo kujua wamejikuta wakinasa kwenye huu mtego ambao chanzo chake ni feminism. Habari ya elimu kwa mtoto wa kike ni matokeo feminism, kudai haki sawa, lakini hili halipo kimaandiko kabisa. Kama yuko mwenye ushahidi wa maandiko atufungue macho.

Utaratibu wa mabinti kuolewa baada ya kuhitimu vyuo wala sio wa kibiblia, haya ni matakwa ya kidunia lakini Mungu hakuwahi kuelekeza hayo. Najua hoja hii ni ngumu kueleweka hasa kufuatia mfumo waliolelewa kizazi hiki ambao ni kinyume na neno la Mungu.

Tazama kizazi kimoja tu nyuma, utabaini hata kwenye jamii zetu umri wa binti kuolewa ilikuwa baada tu ya kuvunja ungo. Mwanamke amepaswa kuolewa katika ubikira wake, huo ndio ukweli mchungu.

Ukiangalia kiundani kabisa hata utoaji wa mahari unakuwa na maana kama binti ataolewa hivi, kuonesha kwamba kijana tukio tayari na ana uwezo kumtunza binti, sio kuoa mtu ambaye amekwisha kujitegemea kitambo kimawazo au ana uwezo wa kuishi maisha yake binafsi halafu unakwenda kwa wazazi kuonyesha eti una uwezo wa kumtunza.

Matokeo yake ndio unakutana na mtihani kwamba umeshindwa kufikia viwango vyake, mfano kumpeleka saluni za gharama, maisha ya anasa, kumridhisha kitandani nk. Hatuoi ili kupata mpambanaji mwenza kwenye kusaka mali, tunaoa kupata msaidizi hasa kwenye eneo la nyumbani (uzazi na malezi) wakati sisi tunapambana kuitunza familia.

Unapooa binti maana yake unatafuta mke wa kuanza naye maisha, maana yake mnaanza pamoja maisha ya ndoa, hivyo amepaswa kuwa fresh kichwani mwake, asiwe na picha yake tofauti kuhusu maisha. Hii ina maana kubwa sana kwenye ndoa kwani mume ndiye mwenye dira, hivyo atamwekea picha halisi aitakayo yeye na watasonga mbele wakiifukuzia hiyo. Katika hilo wana nafasi kubwa ya kutoboa.

Sasa fikiria mume aliyeoa mwanamke ambaye naye anajiona anayo picha ya maisha, akijaribu kumpa maono yake mara nyingi watapishana tu na kuleta misuguano. katika hali hii ndoa nyingi zimekuwa uwanja wa mapambano kwa sababu mke na mume kila mmoja anatazama maisha katika namna tofauti.

Lakini kwa binti ambaye ndio kwanza amevunja ungo akaolewa, bado hana picha halisi ya maisha hivyo mwanamume ana wajibu wa kuandaa ramani zote. Huyu ana nafasi nzuri ya kuwa mke bora na ndoa kudumu.

Ikumbukwe tu kuwa Mungu sio Mmarekani kwamba kila wanachosema hao waliojifanya kuwa taifa la shetani ni haki mbele ya Mungu. Mabinti wengi wamepotea kwa sababu ya kukiuka neno la Mungu na kukimbilia maisha ya kuigiza, matokeo yake wamegeuka wafanyabiashara wa miili yao wenyewe. Ndoa sio maigizo ya Hollywood.

Hoja nyingine ipasayo kuzungumzwa ni wakati sahihi wa kijana wa kiume kuoa. Hili nalo limekuwa tatizo kubwa sana katika kizazi hiki.
Hakuna ambae anasemakuolewa kwa mtoto alie vunja ungo kama ni dhambi kiimani... Ila tunazungumzia utu kwanza...

Huyo mtoto ni mdogo anahitaji elimu kwanza na kukomaa
 
Ahaa, ulikuwa hujajieleza vizuri kwamba nijieleze kuhusu nini.


In Paul's letters to the Ephesians, Paul motivates early Christian slaves to remain loyal and obedient to their masters like they are to Christ. Ephesians 6:5-8 Paul states, “Slaves, be obedient to your human masters with fear and trembling, in sincerity of heart, as to Christ” which is Paul instructing slaves to obey their master.
Naomba uwe unaandika mtazamo wako mwenyewe sio copy and paste. Haya, nitakujibu muda kidogo, ngoja nitulie kwanza.
 
Hakuna ambae anasemakuolewa kwa mtoto alie vunja ungo kama ni dhambi kiimani... Ila tunazungumzia utu kwanza...

Huyo mtoto ni mdogo anahitaji elimu kwanza na kukomaa
Hapo ninekuele6vema mkuu, ndipo hasa hoja yangu ilipo. Hoja ni kwamba tunafuata huu utaratibu MPYA sio kwa sababu ya umri bali kutimiza matakwa ya kidunia, ELIMU KWA MTOTO WA KIKE. Halafu kwa kiasi kikubwa wakishenda huko wanakuwa hawafai tena kwa maisha ya ndoa. Hili ni ukweli uliokataliwa na kizazi kipya. Mojawapo ya sababu KUU za ndoa nyingi kuvunjika hivi sasa ni wanawake kujiingiza mwenye elimu ambayo haikukusudiwa kwa ajili yao tangu mwanzo. Kwa sasa kuongea hivi utaonekana ounguani, ni sawa na mtu atakayejaribu kuupinga ushoga miaka 20 baadaye.
 
Naomba uwe unaandika mtazamo wako mwenyewe sio copy and paste. Haya, nitakujibu muda kidogo, ngoja nitulie kwanza.
Nikiipinga Biblia kwa maneno yangu, unaniambia niweke vifungu vya Biblia, maana yake nisitumie maneno yangu tu.

Nikiweka vifungu vya Biblia, unaniambia niweke maneno yangu mwenyewe.

Hivi, hata wewe mwenyewe unajua unataka nini?
 
Nikiipinga Biblia kwa maneno yangu, unaniambia niweke vifungu vya Biblia, maana yake nisitumie maneno yangu tu.

Nikiweka vifungu vya Biblia, unaniambia niweke maneno yangu mwenyewe.

Hivi, hata wewe mwenyewe unajua unataka nini?
SITAKI COPY AND PASTE. Ikiwa hivyo hata mimi nitakujibu kwa mwendo huo. Weka kifungu ambacho ufafanuzi kwa namna ulivyoelwwa. Google kila mtu anaweza kuitumia, lakini ukipata hoja ielezee kwa jinsi ulivyoielewa WEWE.
 
SITAKI COPY AND PASTE. Ikiwa hivyo hata mimi nitakujibu kwa mwendo huo. Weka kifungu ambacho ufafanuzi kwa namna ulivyoelwwa. Google kila mtu anaweza kuitumia, lakini ukipata hoja ielezee kwa jinsi ulivyoielewa WEWE.
Kwanza kabisa, kwa nini hutaki copy and paste?

Hoja ni hoja tu, pinga hoja, usipinge kitu kwa sababu ni copy and paste.

Hata hiyo Biblia unayoiamini hujaiandika wewe.

Sasa na mimi nikitumia mfumo wako wa "sitaki copy and paste" na kusema kifungu chochote cha Biblia utakachoniletea ni batili, kwa sababu kimsingi ni "copy and paste", nataka unipe hoja wewe mwenyewe, utasemaje?

Huoni kwamba ukikataa copy and paste umeikataa Biblia hapo?

Huoni kwamba hoja hii inatuambia tukatae vitabu, tulete hoja za kutoka vichwani mwetu tu?
 
Kwanza kabisa, kwa nini hutaki copy and paste?

Hoja ni hoja tu, pinga hoja, usipinge kitu kwa sababu ni copy and paste.

Hata hiyo Biblia unayoiamini hujaiandika wewe.

Sasa na mimi nikitumia mfumo wako wa "sitaki copy and paste" na kusema kifungu chochote cha Biblia utakachoniletea ni batili, kwa sababu kimsingi ni "copy and paste", nataka unipe hoja wewe mwenyewe, utasemaje?

Huoni kwamba ukikataa copy and paste umeikataa Biblia hapo?

Huoni kwamba hoja hii inatuambia tukatae vitabu, tulete hoja za kutoka vichwani mwetu tu?
Basi wewe hauko kujifunza, siwezi kujadili na mtu adiyeshughulisha ubongo wake. Nenda google utapata majibu yote
 
Basi wewe hauko kujifunza, siwezi kujadili na mtu adiyeshughulisha ubongo wake. Nenda google utapata majibu yote
Wapi sijashughulisha ubongo wangu?

Wewe unaji contradict. Hutaki copy and paste, halafu unataka kutumia maandiko ya vitabu kwa copy and paste.

Hujui hata unataka nini.

Nimekwambia Biblia ina makosa, kwa sababu ina support utumwa. Hayo maneno yangu, si copy and paste.

Ukataka nikupe vifungu vya Biblia, ambavyo siwezi kuandika vyangu, inanibidi ni copy and paste kama vilivyo katika Biblia.

Kisha unanilaumu kuwa na copy and paste.

Nikiandika maneno yangu hutaki, unataka nilete vifungu vya Biblia.

Nikileta vifungu vya Biblia hutaki, unasema nina copy and paste.

Hujui hata unataka nini zaidi ya ubishi tu.
 
Back
Top Bottom