Mashehe wana hoja kuhusu umri wa kuolewa

Hao mabinti Sasa hivi wanakuwa shule kwahiyo mnataka muwaoe kwanza ndio waende shule?? Ili tu mpate mabikira?? Basi na vijana waoe umr huo huo ili waoane wote wakiwa mabikira
 
Mmmmmmhmn miaka 12 huyo ujue ni mtoto kabisa hata kama kavunja ungo.
 
Kuvunja ungo na uwezo wa kuhimili mikimiki ya uzazi ni vitu viwili tofauti Kuna maternal death mchungaji acheni ujinga wenu wakuozesha mabinti wadogo wa 12 13 afu usisahau kuwah kuvunja ungo mapema sio kua maturity
Kuvunja ungo ni hatua ya awali kabisa ya mwili kudevelop kuelekea utu uzima ila haimaanishi mtu ameshakomaa na yupo tayari kwa majukumu ya ndoa kama kusimamia bajeti za familia, kupanga matumizi, kusimamia ratiba za usafi, kushauri mume na kumliwaza, kubeba ujauzito na kulea mtoto au watoto, kushiriki shughuli za koo na familia.

Nadhani kuna elimu inahitajika hapa ili hili swala lisipotoshwe. Waarabu wanalifanya ila ni familia zenye uwezo ndizo zinakuja na matokeo mazuri ila za kimasikini ndipo shida huanza.

Zee la miaka 50 kumvulia binti wa miaka 14 nguo haijakaa sawa. Kwanza haitamuacha huyu binti salama kiakili.
 
Hii ilianza pale duniani ilipotaka mwanamke apewe nafasi ya kusoma kwanza, lakini huo SIO MPANGO WA MUNGU, tena huwezi kuwa na hoja kupinga
Ila mkuu dini yenu huwa mahubiri hayaishi bila kuzungumzia, Ngono, fuatilia mahubiri ya Shehe Kioozeo, na mashehe wengine Yaani tendo mnalipa uzito mkubwa mno. hadi leo hamuelezi kuwa Mwanamke atapewa nini huko peponi. Maana nyie mnajinasibu na mabikira 72. clips za mashehe mitandaoni ni kuhusu ngono tu
 
Mimi sio Muislamu ndugu yangu.
 
Ukijenga hoja kwa Biblia hata utumwa unaruhusiwa.

Wewe unakubali utumwa?
Ni kweli kabisa - hata Korani inakubali utumwa. Kwa hiyo turejeshe utumwa? Na kukatwa mkono je? Upuuzi mtupu!
Mbona mkiwa huko Ulaya hamleti hoja zenu za kidini? Mwislamu gani anaoa wake wawili au watatu huko Marekani na Canada? Thubutu
 
Wewe ndio jieleze vizuri, usiseme tu Biblia inaruhusu utumwa, toa na vifungu.
Ahaa, ulikuwa hujajieleza vizuri kwamba nijieleze kuhusu nini.

In Paul's letters to the Ephesians, Paul motivates early Christian slaves to remain loyal and obedient to their masters like they are to Christ. Ephesians 6:5-8 Paul states, “Slaves, be obedient to your human masters with fear and trembling, in sincerity of heart, as to Christ” which is Paul instructing slaves to obey their master.
 
Ni kweli kabisa - hata Korani inakubali utumwa. Kwa hiyo turejeshe utumwa? Na kukatwa mkono je? Upuuzi mtupu!
Mbona mkiwa huko Ulaya hamleti hoja zenu za kidini? Mwislamu gani anaoa wake wawili au watatu huko Marekani na Canada? Thubutu
Masheikh kibao wapo wameoa wake wanne tena wazungu walioslimu

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna ambae anasemakuolewa kwa mtoto alie vunja ungo kama ni dhambi kiimani... Ila tunazungumzia utu kwanza...

Huyo mtoto ni mdogo anahitaji elimu kwanza na kukomaa
 
Naomba uwe unaandika mtazamo wako mwenyewe sio copy and paste. Haya, nitakujibu muda kidogo, ngoja nitulie kwanza.
 
Hakuna ambae anasemakuolewa kwa mtoto alie vunja ungo kama ni dhambi kiimani... Ila tunazungumzia utu kwanza...

Huyo mtoto ni mdogo anahitaji elimu kwanza na kukomaa
Hapo ninekuele6vema mkuu, ndipo hasa hoja yangu ilipo. Hoja ni kwamba tunafuata huu utaratibu MPYA sio kwa sababu ya umri bali kutimiza matakwa ya kidunia, ELIMU KWA MTOTO WA KIKE. Halafu kwa kiasi kikubwa wakishenda huko wanakuwa hawafai tena kwa maisha ya ndoa. Hili ni ukweli uliokataliwa na kizazi kipya. Mojawapo ya sababu KUU za ndoa nyingi kuvunjika hivi sasa ni wanawake kujiingiza mwenye elimu ambayo haikukusudiwa kwa ajili yao tangu mwanzo. Kwa sasa kuongea hivi utaonekana ounguani, ni sawa na mtu atakayejaribu kuupinga ushoga miaka 20 baadaye.
 
Naomba uwe unaandika mtazamo wako mwenyewe sio copy and paste. Haya, nitakujibu muda kidogo, ngoja nitulie kwanza.
Nikiipinga Biblia kwa maneno yangu, unaniambia niweke vifungu vya Biblia, maana yake nisitumie maneno yangu tu.

Nikiweka vifungu vya Biblia, unaniambia niweke maneno yangu mwenyewe.

Hivi, hata wewe mwenyewe unajua unataka nini?
 
SITAKI COPY AND PASTE. Ikiwa hivyo hata mimi nitakujibu kwa mwendo huo. Weka kifungu ambacho ufafanuzi kwa namna ulivyoelwwa. Google kila mtu anaweza kuitumia, lakini ukipata hoja ielezee kwa jinsi ulivyoielewa WEWE.
 
Kwanza kabisa, kwa nini hutaki copy and paste?

Hoja ni hoja tu, pinga hoja, usipinge kitu kwa sababu ni copy and paste.

Hata hiyo Biblia unayoiamini hujaiandika wewe.

Sasa na mimi nikitumia mfumo wako wa "sitaki copy and paste" na kusema kifungu chochote cha Biblia utakachoniletea ni batili, kwa sababu kimsingi ni "copy and paste", nataka unipe hoja wewe mwenyewe, utasemaje?

Huoni kwamba ukikataa copy and paste umeikataa Biblia hapo?

Huoni kwamba hoja hii inatuambia tukatae vitabu, tulete hoja za kutoka vichwani mwetu tu?
 
Basi wewe hauko kujifunza, siwezi kujadili na mtu adiyeshughulisha ubongo wake. Nenda google utapata majibu yote
 
Basi wewe hauko kujifunza, siwezi kujadili na mtu adiyeshughulisha ubongo wake. Nenda google utapata majibu yote
Wapi sijashughulisha ubongo wangu?

Wewe unaji contradict. Hutaki copy and paste, halafu unataka kutumia maandiko ya vitabu kwa copy and paste.

Hujui hata unataka nini.

Nimekwambia Biblia ina makosa, kwa sababu ina support utumwa. Hayo maneno yangu, si copy and paste.

Ukataka nikupe vifungu vya Biblia, ambavyo siwezi kuandika vyangu, inanibidi ni copy and paste kama vilivyo katika Biblia.

Kisha unanilaumu kuwa na copy and paste.

Nikiandika maneno yangu hutaki, unataka nilete vifungu vya Biblia.

Nikileta vifungu vya Biblia hutaki, unasema nina copy and paste.

Hujui hata unataka nini zaidi ya ubishi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…