Masheikh 6, leo ijumaa terehe 1/12/2023, wameshinda kesi lakini wamechukuliwa tena na vyombo vya dola

Masheikh 6, leo ijumaa terehe 1/12/2023, wameshinda kesi lakini wamechukuliwa tena na vyombo vya dola

Hawa mashehe wanavyolindwa wakiwa wanaletwa hapo mahakamani unaweza sema ni alqaida
ivi ulikuwepo na wewe pale central leo jioni...yani nikadhani kuna uvamizi umejitokeza...ilikuwa kama muvi ya Rambo aisee kumbe ni hawa masheikh ndio walikuwa wanatolewa ili warudishe gerezani....

jamani ivi ni kweli ni magaidi😭😭😭

kwa kile nilichokiona leo haki vile niliogopa sana...​
 
Uislamu na ugaidi wapi na wapi! Usome Uislamu acha uvivu

Umeshaambiwa wameshinda kesi👇
Hata hivyo katika hali ya kushangaza baada ya Mahakama Kuu kuwaona hawana hatia wamechukuliwa na vyombo vya Usalama na kuondoka nao.
ilikuwa kama muvi za rambo nilikuwepo leo mjini mida ya saa 10 hivi kuelekea saa 11 jioni makomandoo tuseme wa magereza walijitawanya huku na huko kuizingira gari yao ya kubebea wafungwa.

hiyo hali ilinitisha sana kwakweli haswa ukizingatia walikuwa wamefunga ile barabara inayoingia central pale...na mimi na kipikipiki changu nilikuwa nataka nikatize pale😭😭😭

muda huu kupitia hii post ndio napata picha ya kilichokuwa kinajiri pale...​
 
ivi ulikuwepo na wewe pale central leo jioni...yani nikadhani kuna uvamizi umejitokeza...ilikuwa kama muvi ya Rambo aisee kumbe ni hawa masheikh ndio walikuwa wanatolewa ili warudishe gerezani....

jamani ivi ni kweli ni magaidi😭😭😭

kwa kile nilichokiona leo haki vile niliogopa sana...​
Unadhani ni Cinema mkuu?
Sina uhakika wala Ushahidi, binafsi Siwezi kuwahukumu wala kuwatetea.
Kama wana haki wataipata, kama ni magaidi kweli cha moto wakipate.
 
Tangu 2014 mpaka Leo?. Shida serikali inakomoa. Kwanini kesi isisikilizwe mapema?. Watu wake ndani miaka tisa utawahukumu miaka mingapi
 
Naiona Gaza inakaribia.
Mfano
Ukitaka kuwashinda kikundi cha kigaidi cha kiislamu cha Boko Haram pale Nigeria na kuwaondoa wote.

Kamata viongozi wakubwa na wadogo wa kiislamu pale Nigeria weka jela. Kwenye mabaraza yao yote kamata weka ndani hautasikia tena kuwepo kwa kundi lolote la kigaidi la kiislamu.
Hawa jamaa unatakiwa u-deal nao kama wanayofanya Israel kwa Hamas
 
Hawa mashehe wanavyolindwa wakiwa wanaletwa hapo mahakamani unaweza sema ni alqaida
Ukiona hivyo jua ni watu hatari sana kwa usalama wa nchi hii.
Kinacho nipendezesha ni kuwa walikamatwa kipindi cha utawala wa ndg yao ktkt Imani.
Na sasa hizi blah blah zinafanyika kipindi cha utawala wa ndg yao ktk imani.
 
Mfano
Ukitaka kuwashinda kikundi cha kigaidi cha kiislamu cha Boko Haram pale Nigeria na kuwaondoa wote.

Kamata viongozi wakubwa na wadogo wa kiislamu pale Nigeria weka jela. Kwenye mabaraza yao yote kamata weka ndani hautasikia tena kuwepo kwa kundi lolote la kigaidi la kiislamu.
Hawa jamaa unatakiwa u-deal nao kama wanayofanya Israel kwa Hamas
Wacha wee mfuasi wa Bwajima nawaonea huruma jirani zako waislam kwa chuki hii..mrudishe Magufuli au msimike Kabudi ili aje kuwatesa waisla tena furaha yako irudi.
 
Wacha wee mfuasi wa Bwajima nawaonea huruma jirani zako waislam kwa chuki hii..mrudishe Magufuli au msimike Kabudi ili aje kuwatesa waisla tena furaha yako irudi.
Magufuli aliwatesaje?
 
Mpaka washikiliwe na vyombo vya usalama ina maana ni watu hatari sana, waendelee kushikiliwa mpaka nguvu za ugaidi wao ziishe
 
Pole yao sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Wadau hamjamboni nyote?

Kutoka Ukurasa wa Sheikh Ibrahim Ghulaam

Shura ya Maimamu Tanzania imetoa taarifa ya maamuzi ya kesi iliokuwa ikiwakabili Masheikh sita katika Mahakama kuu ya Tanzania

Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa leo Ijumaa na Kaimu Amir wa Shura ya Maimamu Sheikh Imamu Shaaban Ibrahim 0656654546 taarifa imesema, Masheikh hao ni sehemu ya mamia ya Waislamu walio kamatwa na kushikilia takribani mika 10 iliyopita na kufunguliwa mashtaka mbalimbali ya ugaidi.

Masheikh hawa sita baada ya kukaa gerezani kwa zaidi ya miaka 9, leo wameshinda kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaa.

Masheikh walio shinda kesi hio hao ni:

1. Fundi Khamisi Kamaka.
2. Issa Mussa Mustafa.
3. Eliasa Kalinda Kazana.
4. Athumani Khamisi Abeid.
5. Juma Rajab Mbonde. Na-
6. Issa Abdullah Kokoko.

Wamekua gerezani toka 2014.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza baada ya Mahakama Kuu kuwaona hawana hatia, vyombo vya Usalama viliwashikilia tena na kuondoka nao.

Shura ya Maimamu Tanzania inaendelea kufuatilia kushikiliwa tena Masheikh hao na itatoa taafa baada ya kazi hiyo, imemalizia taarifa hio ya Imamu Shaaban Kaimu Amiri wa Shura ya Maimamu Tanzania
 
Huku majizi yanayotajwa katika ripoti za CAG kila mwaka, yakilindwa na serikali hiyo hiyo inayoweka watu ndani kwa miaka 9 na kushindwa kuthibitisha tuhuma zinazowakabili.

Mimi ni Mkristo, lakini siwezi fumbia macho huu uonevu kwassbabu kesho inaweza kuwa zamu yangu kama sio ya wachungaji ama maadkofu, ingawa hizi dini siku hizi nazo zimekuwa ni miyeyusho na hutumika kama vitega uchumi vya viongozi wa kidini .
 
Back
Top Bottom