gallow bird
JF-Expert Member
- Aug 10, 2024
- 14,889
- 18,593
Atakua kayumba, sababu Quran imekataza kujifunza uchawi, haiwezi kataza kitu ambacho hakipoAmesema kabisa haamini uchawi, yeye anachukulia uchawi ni imani hewa tu ila kwenye imani za uchawi watu humshirikisha Mungu ndio maana kautaja uchawi kwenye mada yake ila yeye haamini kuwepo kwa uchawi.
Kwahiyo tiba ya uchawi ni ipi? Maana kama uchawi upo basi pia ipo tiba ya kuondoa madhara yenye kusababishwa na uchawi.
Mfano kusababisha maradhi ya stroke, kumfanya mwanamke ashindwe kupata mimba au mwanamke mwenye mimba asijifungue yani anapitiliza yale makadilio ya muda wa kuzaa na hili limetokea hapa napoishi mpaka huyo mdada alipoelekezwa dawa.Hebu tupe mfano wa hayo magonjwa pia ungejibu na hiyo hoja hapo juu nipate kuunganisha na hii
Kwahiyo tiba ya madhara yenye kusababishwa na uchawi ni ipi?Atakua kayumba, sababu Quran imekataza kujifunza uchawi, haiwezi kataza kitu ambacho hakipo
Ukiwa msafi,huzini,hunywi pombe,swala zote,uchawi haukupatiKwahiyo tiba ya madhara yenye kusababishwa na uchawi ni ipi?
Tatizo lako hata huo uchawi haujui ni nini na kuagua ni nini, ndio maana umeshikilia kutaja waganga tu et unataka uone mganga anayetumia biblia.ushahidi sio hizo picha na story za kusadikika ni field ya waganga wakiagua kwa kutumia biblia.
sio swala la kuamini ni swala la kujua,nawewe unatakiwa ujue kuanzia leo,mganga anayetumia bible anakuona wewe kiazi.
hakuna hiyo kitu.
Usifananishe novena na uchawi wa kiislam ndugu,sio haki.
Huo uganga unaozungumzia ni upi yani unatumia njia zipi kutibu ambazo si uchawi wala shirki?Ukiwa msafi,huzini,hunywi pombe,swala zote,uchawi haukupati
Nilikua hivyo mwanzoni mwa 2000,swala za usiku,wachawi wakawa wananiuliza 'ustadh huwa unafanyajefanyaje..' hiyo ni dom na dar niliulizwa,na Quran ndivyo isemavyo,ukianza tu kuchanganya mambo wachawi watakutia mpaka vidole
Ila kuna uchawi na uganga,ni vitu viwili tofauti, tumia uganga kuondoa uchawi
Stoke, mwanamke kukosa mimba au kushindwa kujifungua inatibika kitabibu hata hospital matibabu yapo zaidi ya hapo ni kumrejea Muumba na kudumisha ibada kama zilivyoelekezwa ili kama kweli sababu ni hao majini waasi wa Mwenyezi Mungu wakutokeMfano kusababisha maradhi ya stroke, kumfanya mwanamke ashindwe kupata mimba au mwanamke mwenye mimba asijifungue yani anapitiliza yale makadilio ya muda wa kuzaa na hili limetokea hapa napoishi mpaka huyo mdada alipoelekezwa dawa.
Hoja gani ya juu?
“Na tafuteni msaada kwa subira na Sala. Na hakika jambo hili ni zito isipokuwa kwa wanyenyekevu.”
Kitendo cha kutumia uganga kuondoa uchawi hiyo shirki yaani umejiingiza katika shirki kwa sababu uchawi kama uchawi ni shirki na hauwezi kumpata isipokuwa mshirikinatumia uganga kuondoa uchawi
“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa, na husamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi amezua dhambi kubwa.”
Kisomo vya Ruqya wewe unachukuliaje katika tiba maana hutumika katika matatizo ya uchawi na majini?Stoke, mwanamke kukosa mimba au kushindwa kujifungua inatibika kitabibu hata hospital matibabu yapo tofauti na hapo ni kumrejea Muumba na kudumisha ibada kama zilivyoelekezwa ili kama kweli sababu ni hao majini waasi wa Mwenyezi Mungu wakutoke
Allah anasema
Surat Al-Baqarah (2:45)
Kwahiyo katika matatizo yote ya dunia suluhisho ni kumuomba Mwenyezi Mungu pekeake ukiliomba hilo jini umepotoka na huo ndio ushirikina wenyewe
Hivi matatizo yanayosababishwa na majini waasi wa Mwenyezi Mungu ndio uchawi?Kisomo vya Ruqya wewe unachukuliaje katika tiba maana hutumika katika matatizo ya uchawi na majini?
Tz mbongo hapa hukunipa Aya naomba unipe tafadhaliLete andiko, mimi lakwangu hili hapa
Allah anasema(Suratul-taghaabun)
64:11 - Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Kwahiyo misiba na matatizo mengine yote hayampati mja isipokuwa kwa idhini yake Mwenyezi Mungu na suluhisho la hayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu lete lakwako
Umeanza kuongea kimakundi,mleta mada kaongelea wasomi wa dini ya kiislamu,hajataja madhehebu,jikite katika mada tafadhali,tunachelewa saana waislamu kwa kuendekeza umadhehebu,why!!???Mahizbi na masufi ndio mishe zao hizo makhurafi
Mkuu wewe unadai uchawi hakuna lakini nilikuuliza inawezekana mtu akafanya uchawi pasina kumshirikisha Mungu? Hukujibu unasema tujadili tu shirki tuache kujadili uchawi ila hapo unaeleza uchawi kiujumla ni kuwa shirki.Kitendo cha kutumia uganga kuondoa uchawi hiyo shirki yaani umejiingiza katika shirki kwa sababu uchawi kama uchawi ni shirki na hauwezi kumpata isipokuwa mshirikina
Surat An-Nisa (4:48)
Mimi nawewe tumekubaliana uchawi ni miongoni mwa shirki kwahiyo hapa tunajadili shirki hatuujadili uchawi kama uchawi jibu maswali niliokuuliza tuendeleeMkuu wewe unadai uchawi hakuna lakini nilikuuliza inawezekana mtu akafanya uchawi pasina kumshirikisha Mungu? Hukujibu unasema tujadili tu shirki tuache kujadili uchawi ila hapo unaeleza uchawi kiujumla ni kuwa shirki.
Hebu jibu mkuu inawezekana mtu akafanya anachoamini ni uchawi ila pasipo kutumia maneno wala kitendo cha kumshirikisha Mungu?
Ni mambo yenye kuhusiana kwa ukaribu sana, kwa mfano inawezekana ukatumika uchawi kumtupia mtu jini limsumbue mtu au kumtia maradhi. Majini hutumika sehemu kubwa kwenye uchawi.Hivi matatizo yanayosababishwa na majini waasi wa Mwenyezi Mungu ndio uchawi?
Maana hapo nimekujibu hoja ya majini na Aya nikakupa naona umeambatanisha na uchawi
Nikupe andiko lipi tena wakati mie nataka kusikia kutoka kwako unazungumziaje kuhusu kisomo cha Ruqya kama nayo ni shirki au sio shirki maana hicho kisomo waislamu hutumia kitiba na ndio hutambulika ndio tiba kisharia, kwahiyo kama sio sahihi nijibu sio sahihi kufanya hicho kisomo.Nipe andiko kuthibitisha hoja yako ili niweze kukupa mtazamo wa dini katika hilo kwa ufahamu wangu
Mimi najua majini waasi humuingia binadamu kwa sababu ya upungufu wa ibada zake, Allah anasemainawezekana ukatumika uchawi kumtupia mtu jini
“Na anayegeuka na kujiepusha na kumkumbuka Mwingi wa Rehema, tunamwekea shetani, naye ndiye anakuwa mwandamizi wake.”