Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Kwahiyo ukimuabudu Mungu hiyo ndio tiba?
Ndio, ukiona jini lililoasi limekuingia jiangalie ibada zako zitakuwa haziposawa kwahiyo kuondoa hiyo shida rudi kwa Mola wako na ufanye ibada kwa usahihi
 
bible haijaelekeza kusali novena,bible imeelekeza kusali na kumwachia Mungu kama hakimu wa haki,zoezi hilo la kumshitakia Mungu ndio huitwa novena,ila kuagua hakuna tafsiri hiyo kwa maelezo ndani ya bible.


hakuna majibu wanapata,Mungu hajibu mambo ya kichawi.

maandiko ya bible hayatumiki kuagua,wachana na hizo article za wafakamia mihogo.

hapa sio swala la wewe kunibembeleza nikubali,ni swala la facts kwamba hakuna waaguzi wanatumia bible,neema hizo zinapatikana kwenye quran pekee.
Mimi nimeweka ushahidi siongei maneno matupu kama wewe, nimekuwekea ushahidi wa jinsi biblia inavyotumika kwenye ushirikina sasa mimi sipo hapa kukushawishi wala kukulazimisha kukubali hilo halinihusu wewe amini utakavyo ni uhuru wako.

Kama unaona biblia haiwezi kutumika kwenye kuagua sawa ila inatumika kwenye ushirikina na ushahidi nimeweka.

Maombi ya novena hayapo kwenye biblia ni utaratibu tu ambao watu wameuunda wa maombi hakuna tofauti na albadri.
 
Kuna hii tabia ambayo imeshakuwa mazoea kwa wengi wa masheikh wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kuchanganya dini na uganga au uchawi.

Utakuta mtu kasoma dini vizuri na ana elimu kubwa lakini badala ya kuitumia elimu hiyo katika kufanya mema na kuitafuta pepo ya Allah (S. W) huitumia kama kigezo cha kuaminika katika masuala ya kiuganga na kichawi jambo ambalo haliruhusiwi katika dini na ni shirki

Katika Surat mubayyina, Allah anasema baada ya Bismillah Arahman rahiim

98:1 - Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,

98:2 - Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika,

98:3 - Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka

98:5 - Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.

Katika aya hizo M/Mungu anasema waumini wote na masheikh hatujaamrishwa ila tuwe wema, tutoe zaka na kusali hayo ya uganga na ushirikina mmeyatoa wapi nyie masheikh nawauliza?

Mmeiharibu dini kiasi kuwa uislamu unaonekana ni dini ya wachawi na mila zingine potofu mlizokuwa nazo kabla hata hamkuujua huo uislamu wala elimu ya dini.

Kupitia andiko hili kama wewe ni Sheikh na una tabia hiyo iache mara moja na tubia kwa Mwenyezi Mungu haraka kabla kifo hakija kufika itakuwa ni khasara kwako siku ya kiyama

NB, tujadili kistaarabu
Uislamu na uganga/uchawi ni kama shingo na kichwa.
 
Ndio, ukiona jini lililoasi limekuingia jiangalie ibada zako zitakuwa haziposawa kwahiyo kuondoa hiyo shida rudi kwa Mola wako na ufanye ibada kwa usahihi
Hicho unachoeleza kipo kimaandiko au ni mtazamo binafsi?
 
Ushirikina ni kushirikisha Mungu na viumbe vingine katika uungu wake,mfano kuomba mizimu,mtu,kuabudu miti,ng'ombe etc
Japo imezoeleka uchawi kuitwa ushirikina lakini uchawi kwa misingi ya Quran si ushirikina bali ni dhambi inayojitegemea na Quran haikukataza tu kuutenda bali hata kujifunza
Sasa mbona mleta mada anasema hakuna uchawi na anakataa hadi matumizi ya kutumia Qur'an kama tiba?
 
Sasa mbona mleta mada anasema hakuna uchawi na anakataa hadi matumizi ya kutumia Qur'an kama tiba?
Sijaona sehemu kakataa uchawi, Quran siyo tiba ya busha wala uchawi, Quran ni muongozo wa namna Gani binadam wahusiane wao kwa wao na wao na mungu
 
Wewe una andiko linaloonesha tofauti na nilichokisema? Hebu nifunze kwalo nipate ufahamu
Mimi najua tiba sahihi ya kisheria kwenye uislamu ni Ruqya kwa matatizo kama hayo ya majini, ila wewe unasema tiba ni kuswali tu.
 
Sijaona sehemu kakataa uchawi, Quran siyo tiba ya busha wala uchawi, Quran ni muongozo wa namna Gani binadam wahusiane wao kwa wao na wao na mungu
Amesema kabisa haamini uchawi, yeye anachukulia uchawi ni imani hewa tu ila kwenye imani za uchawi watu humshirikisha Mungu ndio maana kautaja uchawi kwenye mada yake ila yeye haamini kuwepo kwa uchawi.

Kwahiyo tiba ya uchawi ni ipi? Maana kama uchawi upo basi pia ipo tiba ya kuondoa madhara yenye kusababishwa na uchawi.
 
Mimi najua tiba sahihi ya kisheria kwenye uislamu ni Ruqya kwa matatizo kama hayo ya majini, ila wewe unasema tiba ni kuswali tu.
Lete andiko, mimi lakwangu hili hapa

Allah anasema(Suratul-taghaabun)
64:11 - Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Kwahiyo misiba na matatizo mengine yote hayampati mja isipokuwa kwa idhini yake Mwenyezi Mungu na suluhisho la hayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu lete lakwako
 
Amesema kabisa haamini uchawi, yeye anachukulia uchawi ni imani hewa tu ila kwenye imani za uchawi watu humshirikisha Mungu ndio maana kautaja uchawi kwenye mada yake ila yeye haamini kuwepo kwa uchawi.

Kwahiyo tiba ya uchawi ni ipi? Maana kama uchawi upo basi pia ipo tiba ya kuondoa madhara yenye kusababishwa na uchawi.
Hivi uchawi ni ugonjwa? Maana nijuavyo mimi imesuniwa kuwa Mwenyezi Mungu hakuleta ugonjwa isipokuwa na tiba yake

Sasa je uchawi ni ugonjwa? Au ni imani tu za kishirikina
 
Hivi uchawi ni ugonjwa? Maana nijuavyo mimi imesuniwa kuwa Mwenyezi Mungu hakuleta ugonjwa isipokuwa na tiba yake

Sasa je uchawi ni ugonjwa? Au ni imani tu
Uchawi unaweza kutumika kumsababisha mtu ugonjwa, hata uwepo wa majini ni imani mkuu ndio maana nilikwambia kuna waislamu wengine hawaamini uwepo wa majini kama ambavyo wewe hauamini uchawi.
 
Hii mada haikuhusu kaa pembeni hatupo hapa kukejeli tupo hapa kufundishana kwa tusiyoyajua wewe na kejeli zako anzisha uzi wako

After all wewe sio miongoni mwa masheikh niliyowazungumzia hapa
We maamuma,Nikikuambia kwamba msingi wa elimu ya usihiri upo kwenye juzuu moja wapo katika msururu wa juzuu zenu je utanibishia?,sidhqn kama kuna shehe anakosa kitabu kama Abu maashar al falak kabir na vinginevyo ambavyo ni vitabu vya usihiri,
 
Uchawi unaweza kutumika kumsababisha mtu ugonjwa, hata uwepo wa majini ni imani mkuu ndio maana nilikwambia kuna waislamu wengine hawaamini uwepo wa majini kama ambavyo wewe hauamini uchawi.
Hebu tupe mfano wa hayo magonjwa pia ungejibu na hiyo hoja hapo juu nipate kuunganisha na hii
 
Mimi nimeweka ushahidi siongei maneno matupu kama wewe,
ushahidi sio hizo picha na story za kusadikika ni field ya waganga wakiagua kwa kutumia biblia.
nimekuwekea ushahidi wa jinsi biblia inavyotumika kwenye ushirikina sasa mimi sipo hapa kukushawishi wala kukulazimisha kukubali hilo halinihusu wewe amini utakavyo ni uhuru wako.
sio swala la kuamini ni swala la kujua,nawewe unatakiwa ujue kuanzia leo,mganga anayetumia bible anakuona wewe kiazi.
Kama unaona biblia haiwezi kutumika kwenye kuagua sawa ila inatumika kwenye ushirikina na ushahidi nimeweka.
hakuna hiyo kitu.
Maombi ya novena hayapo kwenye biblia ni utaratibu tu ambao watu wameuunda wa maombi hakuna tofauti na albadri.
Usifananishe novena na uchawi wa kiislam ndugu,sio haki.
 
We maamuma,Nikikuambia kwamba msingi wa elimu ya usihiri upo kwenye juzuu moja wapo katika msururu wa juzuu zenu je utanibishia?,sidhqn kama kuna shehe anakosa kitabu kama Abu maashar al falak kabir na vinginevyo ambavyo ni vitabu vya usihiri,
Hizo zote ulizotaja ni shirki hivyo wanayofanya hayo wana ya kujibu mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya kiyama

Albadir ni shirki

Falaki ni ushirikina
 
Back
Top Bottom