Masheikh wa uamsho ukweli ukoje?

Hawa jamaa inaonekana walifanya kosa ambalo sisi wananchi hatujui. Maana kelele zoote za kuwaachia hamna anayezisikia
 
Mpango nae ni muislam JPM nae alikua muislam
 
Hatari faya kama dhamira yao ilikuwa hivyo....Kama kuna ushahidi wapelekwe mahakamani na wapewe hukumu kwa mujibu wa sheria.
 
Tatizo ushahidi wa moja kwa moja wa kupatikana na ugaidi amna, Tatizo kubwa ni vile hali ilipofikia wakati ule, kuanza kushusha bendera za vyama na kupandisha bendera zao, walikuwa wakikuta watu maskani wanapiga bakora (maskani ni kama vijiwe vya matawi ya vyama like cuf or ccm) serikali ilioona vile ikabidi sasa wachukue hatua.
Hatari faya kama dhamira yao ilikuwa hivyo....Kama kuna ushahidi wapelekwe mahakamani na wapewe hukumu kwa mujibu wa sheria.
 

Basi walifika pabaya walikuwa wanahatarisha uchumi wa nchi.
 
You see, ishu ya Masheikh wa uamsho ni political
Huyo mzee amethibitisha hapo!
 
Waacheni wamuabudu Hugo wanayemuamini atawatetea tu hata kama no miaka mia. Kwa upande mwingine walihatarisha saana kwa kiwamwagia tindikali mapadre. Vatican inawamulika wakiwa hukohuko mahabusu. Maana na mapadre wanamuomba Mungu wao hao watu wasitoke hata Kama no miaka 100. Mid ndo nasemaga dini ya hivi hapana kuiharibu ili wewe utawale kwa mabavu
 
Wewe sema umeandika ulichotaka kuona. Wangewezaje kuiangusha hio Serikali ya CCM ikiwa wao sio Chama cha Siasa na kwa sheria za Uchaguzi za Tanzania kwa jumla kuingingia kwenye Uchaguzi wowote? Nilijua tu utazungumzia suala la Islamic state, nilijua utazungumzia suala la kutiwa Tindikali kwa Padri.

Suala kujiuliza ni hili Baada ya kutiwa Tindikali sio mbio mbio mulileta wataalamu wa FBI kutoka Marekani? Mbona walirejeshwa kimya kimya na ripoti ya nini kilitokea haikutolewa mpaka leo? Sio wewe unaijua sababu ya wao kutiwa ndani? Mbona miaka saba imepita na Upande wa Serikali wameshinda kuwakilisha ushahidi?

Sasa nikueleze ukweli na utabaki kubakia ukweli mpaka dunia itamalizika, Uamsho wametiwa ndani kwa sababu kama walivyo Wazanzibari walio wengi wanapinga na wataendelea kupiga dhulma inayoitwa Muungano. Na kuwatia ndani Uamsho hakuwazuii wazanzibari kudai khaki yao ya msingi, kama unaelewa hivi sasa kuna kesi UN ya wazanzibari kuhusu Muungano.

Kama mnakataa kuurekebisha Muungano kwa maelewano, utavunjika kisheria ni wakati tu ndio utakaosema. Kuna Theory moja ya Physics inasema Water is incompressible maana yake nguvu ile ile unayotumia kuyakandamiza ndio nguvu hio hiyo inayotumia kutaka kutoka
 
Wapi nimezungumzia Islamic state!!nimeandika kutokana na nilichokiona au kujua kutokana na hali ilivyokuwa kule visiwani sipo hapa kutetea uhalali wa muungano au kutetea masala ya siasa, mtoa mada alitaka kujua baadhi ya vitu nami nikajaribu kueleza hali ilivyokuwa kule.pia nikueleze kuiangisha serikali sio lazima uwe au muwe watu wa serikali, kwani yanayoendelea msumbiji sasa hv wale ni watu ambao wapo serikalini au wanavyama vya siasa !!!masheikh wao walitaka mamlaka kamili na kuwaunganisha wazanzibar pasi na kuwa na mfumo wa vyama na walianza kufanikiwa kwenye hilo.
 
Mimi ni Mtanganyika, nina marafiki wengi tu wenyeji wa Zanzibar,
Ishu ya Uamsho siyo kusimika Islamic state, walikuwa wanawaamsha Wazanzibar kuhusu muungano.
Nakubaliana na wewe kabisa, ishu siyo ugaidi, unajua serikali ya CCM imeminya elimu ya utambuzi, hivyo baada ya kuona Uamsho wanatoa elimu ya utambuzi kwa raia, kwa uoga wa serikali wakabambika ugaidi.
Kama ishu ni ugaidi mbona hawapelekwi mahakamani kushitakiwa?
 
Angalu ww umeenda sawa na kama comments yangu umeisoma vzr nilisema hawa jamaa walipewa kesi ya ugaidi ambayo ushahidi wa moja kwa moja hamna, ila beyond ya hii kesi ni kuwa jamaa walikuwa wanaamsha wazanzibar dhidi ya nchi yao na kukataa kutumika kisisasa wakidai kuwa wanasiasa wanamslai yao, sasa ilipofikia hatua ya kuanza kushisha bendera za vyama na kuweka bendera zao juu serikali ilingilia kati
 

Kwamba Tanzania Visiwani (aka Zanzibar) ni kama maji?? Hayatafuti njia ila yanafuata njia?

If only we all knew our wealth.......!!!
 
Guys ukiwa na kaharufu ka ugaid ..kabisa kabisa na kwa dhati ya maslahi ya mama Tanzania ..si tu kwamba hutaishi hapa..bali utakamatwa na kuswekwa jela..Ili iwe funzo kwa wengine...

Kama walikuwa wanahubiri kuwaamsha wa znz..why waifanye kwa fujo... Na kujaribu kuharibu Mali za watu!? Hao wazee sio wa kuwacha wakiwa hai..hata kidogo..ni kuwapeleka kwa mola wao tu..

Na kamtu kanakuja hapa kanatetea malengo yao kwamba sijui nini na nini..shenzi kabisa...kheri tuish masikini kwa amani kuliko kuishi maisha wanayoyataka wao huku ukiwa na bastola kiunoni...

Watanzania washakombolewa toka mwaka 1961 ..now hatutaki ukombozi mwingine..mtu akitaka kujikomboa na ajikomboe mwenyewe kwa kuhama nchi..

I wish I could be president hao watu wangetaja.majina yote matano ya Mzee karume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…