Masheikh wa uamsho ukweli ukoje?

Masheikh wa uamsho ukweli ukoje?

Kwanza kabisa hawa Masheikh wakati wanakamatwa Marais walikuwa ni Kikwete Muislam na Dkt. Shein muislam. Sasa hadi leo Marais ni Samia muislam na Dkt Hussein Mwinyi Muislam.

Lakini kila siku tunasikia hawa Masheikh 'wanaonewa' Kwa kukaa rumande miaka mingi bila kesi yao kupelekwa mahakamani.

Kuna mtu mwenye 'ukweli halisi' Atusaidie? Nini hasa kinaendelea?
Hawa jamaa inaonekana walifanya kosa ambalo sisi wananchi hatujui. Maana kelele zoote za kuwaachia hamna anayezisikia
 
Mpango nae ni muislam JPM nae alikua muislam
 
Ipo hv mkuu, uzuri nilikuwepo unguja kipindi sakasaka hili linatokea, masheikh wa miadhara (uhamsho) wao walikuwa na ajenda yao kubwa ya kuamsha wazanzibar waliolala juu ya swala zima la nchi yao, wao kipindi wapo walikua wanawakumbusha wazanzibar kuwa si ccm wala chadema wala cuf itakayowakomboa kutoka kwenye maisha ya dhiki bali ni kufata mwenendo wa quraan na sunna za mtume.

Hawa masheikh hawakuvutiwa na cuf wala chadema wao walikuwa na sera yao kuwa demokrasia ni ukafiri ndio maana kila walipokuta bendera ya cuf au ccm wao walikua wakizishusha na kupandisha zao ambazo zina rangi nyeupe tupu na maandishi meupe kati yaliyosomeka kwa kiarabu hakuna mola anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na muhammad ni mjumbe wa mwenyezi mungu, wao wao walikuwa wanaamini kuwa kwa umoja wao basi walikua na uwezo wa kuiforce serikali ya ccm kutoka madarakani na wao kuchukua mamlaka kamili, nakumbuka wakati huo mambo mengi yalijitokeza wanawake waliovaaa nusu uchi walipigwa fimbo sn mitaani na vijana wafuasi wa uhamsho, walipinga sn siasa ndani ya zanzibar maana wao hawakuwa na chama, wakawa wanadamana kudai mamlaka kamili ndiipo serikali iliposhtuka na kuona hawa watu wakiachiwa mambo yataharibika Muda si mrefu ndio ikabidi wakamatwe.

Na ndio wakati huo huo viongozi baadhi wa makundi ya kijihad waliwakebehi uhamsho kwa style yao ya kutaka utawala utolewe na kuuita style za kizamni bimana kwenye uislam hakuna maandamano , hvy walitakiwa washike silaha na kuutoa udhalimu. Note sina uhakika sn inavyosemekana kukamaktwa kwa wale watu agizo lilitoka marekani na kusema hao watu ni htr sn hvy wakamatwe kwa makosa ya ugaidi wapo wanaodai kuna viongozi wa uhamsho walifanya training kandahar, na wakati huo raia wa kigeni huko zenji kipindi cha uhamsho walikutwa na madhira mengi sn like kumwagiwa tindi kali na kufanyiwa vitendo visivyofaa. hayo ndio yaliyowasibu uhamsho hadi leo America wanatazama kwa jicho la mwewe if watatoka au laa kesi ngumu.

View attachment 1750626View attachment 1750627
Hatari faya kama dhamira yao ilikuwa hivyo....Kama kuna ushahidi wapelekwe mahakamani na wapewe hukumu kwa mujibu wa sheria.
 
Tatizo ushahidi wa moja kwa moja wa kupatikana na ugaidi amna, Tatizo kubwa ni vile hali ilipofikia wakati ule, kuanza kushusha bendera za vyama na kupandisha bendera zao, walikuwa wakikuta watu maskani wanapiga bakora (maskani ni kama vijiwe vya matawi ya vyama like cuf or ccm) serikali ilioona vile ikabidi sasa wachukue hatua.

Basi walifika pabaya walikuwa wanahatarisha uchumi wa nchi.
 
bila ya shaka alikuwa anafahamu mpango mzima wa kukamatwa kisirisiri hao watuhumiwa na baadae kupelekwa bara, hata pale wataalamu wa sheria walipotoa mawazo yao juu ya makosa ya kushitakiwa bara hao watuhumiwa yeye kama mtendaji mkuu wa serikali hakuonekana kuchukua hatua yeyote

You see, ishu ya Masheikh wa uamsho ni political
Huyo mzee amethibitisha hapo!
 
Waacheni wamuabudu Hugo wanayemuamini atawatetea tu hata kama no miaka mia. Kwa upande mwingine walihatarisha saana kwa kiwamwagia tindikali mapadre. Vatican inawamulika wakiwa hukohuko mahabusu. Maana na mapadre wanamuomba Mungu wao hao watu wasitoke hata Kama no miaka 100. Mid ndo nasemaga dini ya hivi hapana kuiharibu ili wewe utawale kwa mabavu
 
Nilikuwa kule mkuu so nimeandika nilichokiona na kukijua na hizo ndio bendera zao na hiyo ni picha walikuwa wakiandamana mjini kutaka mamlaka kamili zanzibar na kudai tanganyika inaikalia kimabavu zanzibar, serikali ilipoona kuundi linazidi kupata nguvu siku baada ya siku ndio ikabidi wakamatwe.
Wewe sema umeandika ulichotaka kuona. Wangewezaje kuiangusha hio Serikali ya CCM ikiwa wao sio Chama cha Siasa na kwa sheria za Uchaguzi za Tanzania kwa jumla kuingingia kwenye Uchaguzi wowote? Nilijua tu utazungumzia suala la Islamic state, nilijua utazungumzia suala la kutiwa Tindikali kwa Padri.

Suala kujiuliza ni hili Baada ya kutiwa Tindikali sio mbio mbio mulileta wataalamu wa FBI kutoka Marekani? Mbona walirejeshwa kimya kimya na ripoti ya nini kilitokea haikutolewa mpaka leo? Sio wewe unaijua sababu ya wao kutiwa ndani? Mbona miaka saba imepita na Upande wa Serikali wameshinda kuwakilisha ushahidi?

Sasa nikueleze ukweli na utabaki kubakia ukweli mpaka dunia itamalizika, Uamsho wametiwa ndani kwa sababu kama walivyo Wazanzibari walio wengi wanapinga na wataendelea kupiga dhulma inayoitwa Muungano. Na kuwatia ndani Uamsho hakuwazuii wazanzibari kudai khaki yao ya msingi, kama unaelewa hivi sasa kuna kesi UN ya wazanzibari kuhusu Muungano.

Kama mnakataa kuurekebisha Muungano kwa maelewano, utavunjika kisheria ni wakati tu ndio utakaosema. Kuna Theory moja ya Physics inasema Water is incompressible maana yake nguvu ile ile unayotumia kuyakandamiza ndio nguvu hio hiyo inayotumia kutaka kutoka
 
Wapi nimezungumzia Islamic state!!nimeandika kutokana na nilichokiona au kujua kutokana na hali ilivyokuwa kule visiwani sipo hapa kutetea uhalali wa muungano au kutetea masala ya siasa, mtoa mada alitaka kujua baadhi ya vitu nami nikajaribu kueleza hali ilivyokuwa kule.pia nikueleze kuiangisha serikali sio lazima uwe au muwe watu wa serikali, kwani yanayoendelea msumbiji sasa hv wale ni watu ambao wapo serikalini au wanavyama vya siasa !!!masheikh wao walitaka mamlaka kamili na kuwaunganisha wazanzibar pasi na kuwa na mfumo wa vyama na walianza kufanikiwa kwenye hilo.
Wewe sema umeandika ulichotaka kuona. Wangewezaje kuiangusha hio Serikali ya CCM ikiwa wao sio Chama cha Siasa na kwa sheria za Uchaguzi za Tanzania kwa jumla kuingingia kwenye Uchaguzi wowote? Nilijua tu utazungumzia suala la Islamic state, nilijua utazungumzia suala la kutiwa Tindikali kwa Padri. Suala kujiuliza ni hili Baada ya kutiwa Tindikali sio mbio mbio mulileta wataalamu wa FBI kutoka marekani? Mbona walirejeshwa kimya kimya na ripoti ya nini kilitokea haikutolewa mpaka leo? Sio wewe unaijua sababu ya wao kutiwa ndani? Mbona miaka saba imepita na Upande wa Serikali wameshinda kuwakilisha ushahidi?.
Sasa nikueleze ukweli na utabaki kubakia ukweli mpaka dunia itamalizika, Uamsho wametiwa nddani kwa sababu kama walivyo Wazanzibari walio wengi wanapinga na wataendelea kupiga dhulma inayoitwa Muungano. Na kuwatia ndani Uamsho hakuwazuii wazanzibari kudai khaki yao ya msingi, kama unaelewa hivi sasa kuna kesi UN ya wazanzibari kuhusu Mungano. Kama munakataa kuurekebisha Muungano kwa maelewano, utavunjika kisheria ni wakati tu ndio utakaosema. Kuna Theory moja ya Physics inasema Water is incompressible maana yake nguvu ile ile unayotumia kuyakandamiza ndio nguvu hio hiyo inayotumia kutaka kutoka
 
Mimi ni Mtanganyika, nina marafiki wengi tu wenyeji wa Zanzibar,
Ishu ya Uamsho siyo kusimika Islamic state, walikuwa wanawaamsha Wazanzibar kuhusu muungano.
Nakubaliana na wewe kabisa, ishu siyo ugaidi, unajua serikali ya CCM imeminya elimu ya utambuzi, hivyo baada ya kuona Uamsho wanatoa elimu ya utambuzi kwa raia, kwa uoga wa serikali wakabambika ugaidi.
Kama ishu ni ugaidi mbona hawapelekwi mahakamani kushitakiwa?
 
Angalu ww umeenda sawa na kama comments yangu umeisoma vzr nilisema hawa jamaa walipewa kesi ya ugaidi ambayo ushahidi wa moja kwa moja hamna, ila beyond ya hii kesi ni kuwa jamaa walikuwa wanaamsha wazanzibar dhidi ya nchi yao na kukataa kutumika kisisasa wakidai kuwa wanasiasa wanamslai yao, sasa ilipofikia hatua ya kuanza kushisha bendera za vyama na kuweka bendera zao juu serikali ilingilia kati
Mimi ni Mtanganyika, nina marafiki wengi tu wenyeji wa Zanzibar,
Ishu ya Uamsho siyo kusimika Islamic state, walikuwa wanawaamsha Wazanzibar kuhusu muungano.
Nakubaliana na wewe kabisa, ishu siyo ugaidi, unajua serikali ya CCM imeminya elimu ya utambuzi, hivyo baada ya kuona Uamsho wanatoa elimu ya utambuzi kwa raia, kwa uoga wa serikali wakabambika ugaidi.
Kama ishu ni ugaidi mbona hawapelekwi mahakamani kushitakiwa?
 
Wewe sema umeandika ulichotaka kuona. Wangewezaje kuiangusha hio Serikali ya CCM ikiwa wao sio Chama cha Siasa na kwa sheria za Uchaguzi za Tanzania kwa jumla kuingingia kwenye Uchaguzi wowote? Nilijua tu utazungumzia suala la Islamic state, nilijua utazungumzia suala la kutiwa Tindikali kwa Padri. Suala kujiuliza ni hili Baada ya kutiwa Tindikali sio mbio mbio mulileta wataalamu wa FBI kutoka marekani? Mbona walirejeshwa kimya kimya na ripoti ya nini kilitokea haikutolewa mpaka leo? Sio wewe unaijua sababu ya wao kutiwa ndani? Mbona miaka saba imepita na Upande wa Serikali wameshinda kuwakilisha ushahidi?.
Sasa nikueleze ukweli na utabaki kubakia ukweli mpaka dunia itamalizika, Uamsho wametiwa nddani kwa sababu kama walivyo Wazanzibari walio wengi wanapinga na wataendelea kupiga dhulma inayoitwa Muungano. Na kuwatia ndani Uamsho hakuwazuii wazanzibari kudai khaki yao ya msingi, kama unaelewa hivi sasa kuna kesi UN ya wazanzibari kuhusu Mungano. Kama munakataa kuurekebisha Muungano kwa maelewano, utavunjika kisheria ni wakati tu ndio utakaosema. Kuna Theory moja ya Physics inasema Water is incompressible maana yake nguvu ile ile unayotumia kuyakandamiza ndio nguvu hio hiyo inayotumia kutaka kutoka

Kwamba Tanzania Visiwani (aka Zanzibar) ni kama maji?? Hayatafuti njia ila yanafuata njia?

If only we all knew our wealth.......!!!
 
Guys ukiwa na kaharufu ka ugaid ..kabisa kabisa na kwa dhati ya maslahi ya mama Tanzania ..si tu kwamba hutaishi hapa..bali utakamatwa na kuswekwa jela..Ili iwe funzo kwa wengine...

Kama walikuwa wanahubiri kuwaamsha wa znz..why waifanye kwa fujo... Na kujaribu kuharibu Mali za watu!? Hao wazee sio wa kuwacha wakiwa hai..hata kidogo..ni kuwapeleka kwa mola wao tu..

Na kamtu kanakuja hapa kanatetea malengo yao kwamba sijui nini na nini..shenzi kabisa...kheri tuish masikini kwa amani kuliko kuishi maisha wanayoyataka wao huku ukiwa na bastola kiunoni...

Watanzania washakombolewa toka mwaka 1961 ..now hatutaki ukombozi mwingine..mtu akitaka kujikomboa na ajikomboe mwenyewe kwa kuhama nchi..

I wish I could be president hao watu wangetaja.majina yote matano ya Mzee karume.
 
Back
Top Bottom