Masheikh wa Uamsho wafutiwa kesi, warejea uraiani
Lipo jambo
Wakati mwingi sherehe hugeuka vilio
Ni swala la muda mtagundua jambo
Majuto atakuwa mjukuu
Mtashangazwa
Endeleeni kupiga makofi
uamsho kwanza
Wapinzani mtasubiri sana

Watakuelewa wachache
 
Naunga mkono hoja, jamii ina changamoto nyingi sana zinazohitaji mafundisho ili kuzitatua kuliko, kung'ang'ana kufundisha chuki dhidi ya wengine.

Kwa uchache tu, sasa wana kazi ya kuwafundisha vijana kuacha, zinaa, wanaume kuwa waaminifu kwa wake zao na kutunza familia, jamii iepuke wizi, rushwa, madawa ya kulevya, ulevi, mauaji, uchawi n.k.

Pia wakiwahamasisha wanajamii kupendana na kusameheana lea kweli Mwenyezi Mungu atawarehemu na kuwapa barka nyingi katika maisha haya na ahera.

Bismillahir Rahmaanir Rahiim
Hiyo sio agenda yao. Kama unataka wewe pia unaweza ukaanza kuifundisha jamii juu ya kuacha zinaa, kutunza family na kuacha dawa za kulevya.

Wao agenda yao ni kuukataa Muungano huu wa Ukandamizaji na uonevu kwa Wazanzibari wenzao.

Na kazi hiyo ITAENDELEA kwa kauli mbiu ya KAZI IENDELEE
 
Na tangu hawa watu wahifadhiwe, hali ilikuwa shwari.
Magaidi wa msumbiji viongozi wake wengine wanatoke a Tanzania.
Leo hii, yanatukuta tena Watanzania.
Mungu Irehemu nchi ya Tanzania, maana bila Rehema ya Mungu kinachofuata ni kilio na kusaga meno.
Ni kweli mkuu wataanza kutokea watu kama waliompiga risasi Tundu Lisu,waliompoteza Mawazo,Ben Sanane ,Azory Gwanda,Mawazo na wengne.Mungu huyu adhihaikiwi lakini huwezi ukafanya kinyago ni muuumba wako ukawa na akili ,over

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Utaratibu wa fidia ukiwepo tena kwa kuwakata mafao yao watumishi wote wanaoweka watu ndani kabla ya ushahidi kukamilika itasaidia kupunguza utitiri watu kukaa mahabusu na kuokoa kodi zetu.

Kwa sababu hakuna utaratibu huo easy tu mtu kukaa ndani hata miaka zaidi ya hio. Hao ni mashehe tu je kuna wangapi Wana miaka zaidi ya hio ndani?

Ulimwengu wa Sasa hivi ni ngumu Sana huwezi jificha popote pasipojulikana kama upo nje kwa Dhamana. Ipo haja kama ushahidi haujakamilika mtu asikamatwe kama walivyo wenzetu.
 
Hongera sana Shehe Ponda ni wewe pekee kati ya wachache tulikusikia ukipaza sauti kwa uwazi bila ya kutetereka tikea yule aliepelekewa akae nao hajaaiaga dunia. Bila ya kuwasahau mashehe wengine waliopo vizuizini kwenye mikoa mbalimbali na pale arusha ambapo uwazi wake upo kweupe kabisa.
DPP amewaahidi Masheikh wa UAMSHO kwamba hata wale wa Arusha na nchi nzima atashughulikia masuala yao na haki zitapatikana in shaa Allah.

Tunae rais ambae anastahili kuombewa na Watanzania wote maana neema tele zinakuja.
 
jiwe hatetewi usipoteze muda wako. Unafata maneno ya watu au unazingatia haki? halafu watu wakikushauri ndio utukane?
Nimtete marehemu? mtu aliyekufa anatetewa kwa jambo lipi? upo sawa lakini mkuu?

Halafu wewe unafikiri hao masheikh wametoka kwa sababu ya kuzingatiwa haki? hivi huko gerezani kulikuwa na hao masheikh tu ndio ambao waliwekwa huko gerezani muda mrefu isivyo haki?
 
Eee..!.Mungu Baba Mwenyezi twakuomba uliepushe taifa letu lisije tena likapata watawala dhalimu kama jiwe milele na milele sio leo,kesho na hata vizazi vyetu vijavyo.

Nafunga katika Jina la YESU jina kuu kuliko majina yote.Nikiomba na kuamini hakika hakuna kiongozi dhalimu tena ataketokea katika taifa hili katika Jina la YESU Kristo ulie hai.! Nateketeza kwa moto ulao !

roho zote chafu za viongozi kama Sabaya bashite zisiinuke tena katika taifa hili milele na milele.Tukiomba na kuamini.Na KILA mmoja na aseme.Amee...ni !
Hili ni jambo la faraja sana hasa ukichukulia hawa watu hawajahukumiwa kutokuwa na makosa bali kesi imefutwa. Kilio cha wengi kwa muda wote huu kilikuwa kwenye options 3, kwamba ushahidi uaptikane na wafungwe jela, kama ushahidi ulikuwa haupo basi wangepewa dhamana ili ukikamilika ndio waitwe Mahakamani au basi waachiwe huru kama ilivyotokea ....hii imesubiri miaka 9 (ajabu),
Huenda wapo wengine wengi kama hawa na wanapitia mateso haya haya.

Kuwekana sana, hili si tatizo la mwendazake maana naye aliwakuta ndani tayari na akawaacha. Sijui tunaweza kusema ni tatizo la ccm au vyovyote lakini lililo kubwa ni kupata aina ya KATIBA itakayotulazimisha kutendeana haki na hata tusipoitenda haki basi tuone haya.
Tujifunze sasa badala ya kutegemea huruma au 'ukatili' wa mtu binafsi eti sababu ya cheo chake basi tuitegemee Katiba walau kwa 60%
 
DPP amewaahidi Masheikh wa UAMSHO kwamba hata wale wa Arusha na nchi nzima atashughulikia masuala yao na haki zitapatikana in shaa Allah.

Tunae rais ambae anastahili kuombewa na Watanzania wote maana neema tele zinakuja.
Watolewe masheikh tu halafu unataka aombewe na watanzania wote?
 
Mbona hukupeleka ushahid Mahakamani kwa kipindi cha miaka Kumi NYINYI ni madhalimu washenzi but haki huchelewa lkn hupatikani

Munawazuia watu miaka Kumi kwa kesi za ujanja ujanja kisa chuki zenu dhidi ya ZANZIBAR kwa taarifa yako mateso haya mnayotufanyia ndio yanayotuleta pamoja zaid

Ushindi wa wazi wa Maalim Seif alioupata 2015 kisa ni hawa masheikh

WAKOLONI WEUSI TUACHENI TUPUMUWE
Hlf nyie mna fikra la kiarabu hilo eneo ni la tanganyika msituletee ufirauni wenu
 
Watolewe masheikh tu halafu unataka aombewe na watanzania wote?
Wewe Mrundi kama hutaki kumuombea Mheshimiwa Rais wacha.

Kwanza maombi yako hayana msaada wowote. Sisi Watanzania tutamuombea maana ndio nchi yetu itapata neema kwa kuwa na rais muadilifu asiependa wananchi wake waonewe.
 
Back
Top Bottom