Masheikh wa Uamsho wafutiwa kesi, warejea uraiani
LEO TUKO FURAHANI KWA KUACHIWA MASHEIKH WETU

Iko kasda huwa tunaimba katika kusheherekea kuzaliwa kwa Mtume SAW...

Kasda hii maarufu tumekuwa tukiosoma toka tuko wadogo hado leo tunakaribia mwisho wa maisha yetu.

Kasda hii ni maarufu sana kiasi kila isomwapo hadhira yote itaingia kuiimba kwani hakuna asiyeijua.

Lakini kasda hii maarufu hutufurahisha sisi wazee kwa kuwa wanaotuongoza siku zote na miaka yote huwa watoto wadogo wa madrasa wa kike na kiume.

Kasda hii tamu inaanza na maneno haya, ''Leo tuko furahani kwa kuzaliwa Nabiyya...''

Sisi leo tuko furahani kwa masheikh wetu kutolewa gerezani baada ya takriban miaka tisa.

Binafsi taarifa hii nimeanza kuisikia toka jana usiku lakini sikuzingatia kwani ni habari ambazo tunazo wakati wote na muda wote na kwa miaka yote tisa.

Leo asubuhi na mapema ndiyo habari zikapata yakini.

Leo baada ya Sala ya Dhuhr Imam wetu hapa Masjid Nur, Magomeni Mapipa, Sheikh Amir bin Hangali Bombo baada ya sala akatuomba tusome ''Alamnashrah'' na ''Ayatu Kursiyu'' (Moyo wa Qur'an) tumshukuru Allah kwa hisani hii kubwa aliyotufanyia.

Hakika baada ya dhiki huja faraja, baada ya dhiki huja faraja.

Napenda nishereheshe maneno yaliyomo katika Ayatu Kursiyu lakini naogopa.

Huo si uwanja wangu.
Unahitaji ilm.

Naam Masjid Nur ilizizima kwa kisomo hiki na kwa shukurani kwa Allah na mwitikio wa dua aliyosoma Imam wetu Sheikh Amir.

Na kwa hakika waumini wote walionekana na sura zilizochangamka.

Leo tuko furahani.

Sheikh Ponda amefika Zanzibar leo asubuhi kuwapokea masheikh kama picha inavyoonyesha.

Screenshot_20210616-150801_Facebook.jpg
 
wameachiwa kwa sababubya kila mwenye nia njema alipiga kelele juu ya uonevu ikiwemo pamoja na Vyama hasa Chadema. We ni mjinga unapinga jitihada za wazi zilifanywa na CHADEMA na Tundu Lissu wakati aa kampeni
Ukimfahamisha mjinga sometimes unapoteza tu nguvu na muda wako.

Wajinga wapelekwe kijingajinga hivyohivyo.

CDM ilipaza sauti sana sana sana juu ya suala hili.
 
Hiyo sio agenda yao. Kama unataka wewe pia unaweza ukaanza kuifundisha jamii juu ya kuacha zinaa, kutunza family na kuacha dawa za kulevya.

Wao agenda yao ni kuukataa Muungano huu wa Ukandamizaji na uonevu kwa Wazanzibari wenzao.

Na kazi hiyo ITAENDELEA kwa kauli mbiu ya KAZI IENDELEE

Wao ni masheikh au mwanaharakati au wapigania uhuru?
 
Kwa hivyo wanzazibari hawana haki ya kudai mamlaka kamili? Kwa hili nakupa jibu la Prophet Bob marley:
Every man has the right to decide his own destiny and in this judgement there is no partiality.
Uamsho hawajatendewa haki.
Simple and clear
 
Je ukiambiwa uthibitishe utakuwa tayari?

Tumuogope Mwenyezi Mungu...
Na ndio sababu hiyo hiyo inayomfanya rais ahakikishe ndani ya uongozi wake haki inatendwa.

Kwa mujibu wa uislam, uongozi ni dhamana kubwa sana tena sana. Mtu mmoja tu kati ya unaowaongoza akidhulumiwa basi wewe kiongozi unakuwa liable.

Muacheni Mama afanye kazi. Hawa watu wameshikiliwa miaka tisa na hao waliotangulia JK na JPM japo waliapa kwa vitabu vya dini zao lakini hawakujali haki za hawa watu.
 
Naulizia hivi;

Je huko gerezani hakuna wengine ambao wamekaa zaidi ya muda huo?...
Hapa nakubaliana na hoja yako.

Kwa kweli kama kuna mtu amekaa huko gerezani muda mrefu na kesi yake inapigwa danadana tupazeni sauti haki zao zipatikane as well.

Na ndio maana tunasisitiza kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
 
huku hayawahusu wao na ccm chungu kimoja
Mkuu wapo CCM wengi tu ambao tunawajua/tunajijua kwamba walikuwa wakikataa uonevu huu. Baadhi walizisaidia hata familia za Masheikh juu ya mambo mbali mbali
 
Maskini machozi ya yule padre aliyemwagiwa tindikali, yule shehe mwenye asili ya tanga aliyemwagiwa tindikali, yule polisi aliyechinjwa hapo mwanakwwrekwe, wataliinwaliokuwa wanamwagiwa tindikali, makanisa yaliyokuwa yanachomwa , bar, pamoja na mabucha ya kitimoto🙆‍♂️🙆‍♂️
Mkuu, huoni kama ilitakiwa kama walifanya hayo kesi yao isikilizwe na iishe badala ya kuwekwa kizuizini miaka nenda rudi?!?
 
sasa watatokea chagadomo na kumbebesha lawama mwendazake utadhani yeye ndo aliwafungia ndani...ifikie sehemu usalama wa nchi uwe zaidi ya dini,kabila wala jinsia..big up kikwete..big up magufuri..hope mama samia kuwatoa hawa ndugu zake amewaonya waende wakatulie na kulea watoto wao..hii nchi ni zaidi ya mtu mmoja mmoja
Hao uliowapa big up wote hawastahili.

Katika tawala zao waliona hawa watu wanaonewa lakini wakaamua kuunyamazia kimya uonevu huo.

Mama tutamkumbuka kwa uongozi wake milele na milele
 
Back
Top Bottom