Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
LEO TUKO FURAHANI KWA KUACHIWA MASHEIKH WETU
Iko kasda huwa tunaimba katika kusheherekea kuzaliwa kwa Mtume SAW...
Kasda hii maarufu tumekuwa tukiosoma toka tuko wadogo hado leo tunakaribia mwisho wa maisha yetu.
Kasda hii ni maarufu sana kiasi kila isomwapo hadhira yote itaingia kuiimba kwani hakuna asiyeijua.
Lakini kasda hii maarufu hutufurahisha sisi wazee kwa kuwa wanaotuongoza siku zote na miaka yote huwa watoto wadogo wa madrasa wa kike na kiume.
Kasda hii tamu inaanza na maneno haya, ''Leo tuko furahani kwa kuzaliwa Nabiyya...''
Sisi leo tuko furahani kwa masheikh wetu kutolewa gerezani baada ya takriban miaka tisa.
Binafsi taarifa hii nimeanza kuisikia toka jana usiku lakini sikuzingatia kwani ni habari ambazo tunazo wakati wote na muda wote na kwa miaka yote tisa.
Leo asubuhi na mapema ndiyo habari zikapata yakini.
Leo baada ya Sala ya Dhuhr Imam wetu hapa Masjid Nur, Magomeni Mapipa, Sheikh Amir bin Hangali Bombo baada ya sala akatuomba tusome ''Alamnashrah'' na ''Ayatu Kursiyu'' (Moyo wa Qur'an) tumshukuru Allah kwa hisani hii kubwa aliyotufanyia.
Hakika baada ya dhiki huja faraja, baada ya dhiki huja faraja.
Napenda nishereheshe maneno yaliyomo katika Ayatu Kursiyu lakini naogopa.
Huo si uwanja wangu.
Unahitaji ilm.
Naam Masjid Nur ilizizima kwa kisomo hiki na kwa shukurani kwa Allah na mwitikio wa dua aliyosoma Imam wetu Sheikh Amir.
Na kwa hakika waumini wote walionekana na sura zilizochangamka.
Leo tuko furahani.
Sheikh Ponda amefika Zanzibar leo asubuhi kuwapokea masheikh kama picha inavyoonyesha.