Msiione haki kwa upande mmoja tu kutaka nyie mpewe zaidi ya wengine, huo ni ubinafsi, aina ya mahubiri mliyotoa yalihamasisha chuki zilizowaumiza wengine ambao nao wana haki zao, baada yenu kuwekwa ndani hali ikatulia.
Mkajifunze kuheshimu haki za wengine kama nyie mnavyotaka haki zenu ziheshimiwe, msijione bora zaidi ya wengine mpaka kuwasababishia maumivu ya aina yoyote.
Mmefurahi kutoka jela ila mjue sasa mna jukumu la kulinda raia wengine wasio wa imani kama yenu, muache mihemko, fanyeni yenu muwaache wengine wafanye yao kwa uhuru wao, hii Tanzania ni yetu sote, hakuna alie juu ya mwingine wala hatakuwepo.