Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mashekhe waliokutana chini ya Shekhe Mkuu Mufti Abbakari, kwenye msikiti wa kwa Mtoro, jijini Dar es Salaam wamefanya ibada maalum ya kumwombea Rais Samia ashinde kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Shekhe mkuu akiwa kwenye ibada hiyo ameagiza kuwa mashekhe wa mikoa yote, wilaya hadi kwenye kata, wafanye ibada ya kumwombea Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.
Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.
SWALI:
Tukiyaamini maneno ya mashekhe hawa, ina maana uchaguzi wa safari hii utakuwa ni ushindani kati ya wanadamu na majini? Kama majini yakishinda, huyu Rais atakuwa wa wanadamu wa Tanzania au atakuwa Rais wa majini?
Wananchi wanapomchagua kiongozi wao, matarajio yao ni kuwa huyo wanayemchagua atawaongoza katika jitihada zao za kuyafikia maendeleo, sasa kama majini yatamchagua mgombea kuwa Rais, hayo majini yanatarajia kunufaika vipi na huyo yaliyempigania?
Wataalam wa majini tunaomba litoleeni ufafanuzi hili la mashekhe kuomba majini yamsaidie Rais Samia, inamaanisha nini katika tafsiri pana?