Pre GE2025 Mashekhe wafanya ibada na kuomba majini yasaidie Rais Samia kushinda kwenye uchaguzi ujao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Duh 🙄 !
Watu wengine hawajui kuwa tunakula ili tuishi, hatuishi ili tule 😁🤣🤣
Kumbe mzee anajitoa ufahamu ili tu atimize matamanio yake !
Hatari sana !
Maneno aliyoyatamka hayawezi kutamkwa na mtu aliyeisoma dini akaielewa !
 
Kwahiyo ni haramu kuomba msaada kwa majini hata jambo jema?
 
Wengine hufanya mizaha mahali hapastahili kufanya mzaha !
Hatari sana !
 
inawezekana hadi sasa tunaongozwa na majini ndio maana maisha ni magumu sana mtaani, Ni wapumbavu wale wote wanaoomba wajini yawasaidie ktk mambo yao..tutayakemea kwa Jina la Yesu yafe kabisa....apigiwe kura mwanaume na ashinde...atoke upande wowote wa chama cha siasa...biashara ya majini piga chini
 
Hebu weka link tumsikie tujiaminishe.
 
Kwhy hiyo clip yametajwa majini?au Samia ndo Rais wa kwnz kuombewa na viongozi wa dini?...uzushi ndo laana mliyopewa wagalatia...kwani uzushi wa Papa Francis awabariki LGBT hukuhusikia?...kwmb aliongea na mungu?
Majini yametajwa, haujaisikiliza?
 
Kwahiyo ni haramu kuomba msaada kwa majini hata jambo jema?
Sio majini tu hata malaika haturuhusiwi kuwaomba kwasababu kiwataka msaada ni kuwatoa kwenye majukumu yao waliyopangiwa ambayo ni kumtii Allaah yale anayowaamrisha na sio kusikiliza maombi ya wanaadamu.
Upande wa malaika wote ni wema.
Hakuna malaika muovu hata mmoja ila ndio kama nilivyosema kwamba kujibu maombi ya wanaadamu sio sehemu ya majukumu yao ila pale Allaah anapowaamrisha kumnusuru au kumpa nguvu mwanadamu basi hufanya hivyo kwa kumtii Mola wao.
Ama kuhusu MAJINI WAMEGAWANYIKA WEMA NA WAOVU!
Na unapomuomba msaada huna elimu ya kukujulisha kuwa jini unayemuomba msaada ni mwema au ni muovu, ana uwezo wa kufanya hicho unachomuomba au hana uwezo?!
Hawa viumbe wamepewa uwezo wa kutuona ila sisi hatuwaoni!
Mimi ni mwalimu wa madrasa na kiarabu ninakijua kiasi chake!.
HIVYO VITABU WANAVYOTUMIA AKINA DR SULE KIVUTA MAJINI NIMEWAHI KUVITIPIA JICHO KIDOGO!
Ili kimvuta jini aweze kukufanyia mambo unayoyataka kuna proces ndefu ya kupitia mambo mengi ya ukafiri na madhambi.
Kwa mfano jini ili kumuita aweze kufuata maelekezo yako unaweza kuambiwa ukadumbukize msahafu chooni, uandike Aya kadhaa za Quran kwa kutumia damu ya hedhi , ukae siku 40 bila kuoga wala kutawadha na mambo mengine ya madhambi kabla hujafika hapo kwenye kuchinja mnyama mwenye sifa na rangi maalumu ili kumpa jini sadaka ya damu.
Kumtumia jini lazima uingie katika ukafiri kwakuwa ni maelewano na mikataba na makubaliano maalumu, nifanyie hiki nikufanyie kile hakuna jini anayetoka msaada kwa binadamu bila masharti ya kumkufuru Mungu, labda binadamu huyo awe Nabii na mtume kama ilivyokuwa kwa Nabii Suleymani.
 
Inafikirisha sana
 
Wasingempa platform, amewadhalilisha hao wengine inaonekana lao ni moja. Yuko high table na anaongea maneno yanayodhalilisha dini yake kusema ataomba majini yamsaidie rais. Watu distinguished wanapokaa huwa kuna utaratibu maalum wa kuongea, haiwezekani kila mtu asimame na kuongea anavyojisokia.
 
Nakuunga mkono.
Waliokuwa kwenye kile kikao lao Moja! Na hayo ni machache waliyoyaropoka kama bahati mbaya lakini huko sirini hutenda na kusema mabaya kushinda hayo ambayo hawako tayari kuyaweka hadharani isipokuwa kwa watu maalumu ambao huwafuata kuomba kutatuliwa shida zao ikiwa pamoja na WANASIASA ambao huwafuata katika vipindi kama hivi vya kuelekea kwenye uchaguzi kuwaomba wawafanyie makafara waweze kushinda ubunge na udiwani.
Hiki ni kipindi cha makuhani kula vizuri na kunenepa kutokana na hela za WANASIASA wanazomwaga ili wafanyiwe utaalamu uchaguzi uwaendee vizuri.
 
Hajatajwa shetani wametajwa majini, suala la majini kuwa ni malaika(waliyoasi) ni mtazamo wa wakristo ila waislamu kwao majini ni viumbe ambao si malaika wala si binaadamu. Sijawahi kuelewa kwanini hao malaika waliyoasi waitwe majini.
 
SI kwamba hapo umeelezea aina ya majini ambao ni waovu tu(mashetani)?
 
BAKWATA ni moja ya jumuia za CCM kama ilivyo UVCCM.
 
SI kwamba hapo umeelezea aina ya majini ambao ni waovu tu(mashetani)?
Wewe uwezo wa kutofautisha jini mwema na jini muovu (shetani ) unautoa wapi bila kuingia katika vitabu vya elimu za uchawi ambavyo ndivyo vinaelekeza namna ya kuanzisha mawasiliano na urafiki na majini?!
Elewa kwamba majini ni jamii ya viumbe tofauti na sisi wanaadamu na wamepewa uwezo wa kutuona sisi ila sisi hatuwaoni, na hao majini wema. Allaah hajawapa mamlaka ya kutatua shida za wanaadamu bali yatakiwa wanaadamu wasaidiane wenyewe kwa wenyewe katika mambo mema, na majini nao wasaidiane wenyewe kwa wenyewe katika mambo mema.
Elimu yoyote inayoelezea namna ya kuanzisha mawasiliano na mahusiano na majini ni katika elimu za uchawi ambazo ni haramu kujifundisha elimu hizo.
 
Kwahiyo ni haramu kuomba msaada kwa majini hata jambo jema?
Wewe unaombaje msaada kwa kiumbe ambaye humuoni? ! Wajuaje kama muda huo anakusikia?! Wajuaje kama muda huo amelala au Yuko mbali sana na wewe ?! Hakuna namna ya kuhakikisha kuwa unachokiomba kwa majini kinapatikana bila kujifunza elimu ya uchawi tuliyoletewa huku Afrika na baadhi ya waarabu waliojivika sura na matendo ya kiislamu wakatuchanganyia haki na batili na sisi kutokana na ujinga tukashindwa kutofautisha karama na uchawi!
Allaah peke yake ndiye twatakiwa kumuomba hali ya kuwa hatumuoni.
Mwingine yeyote utakayemuomba hali ya kuwa haumuoni utakakuwa umemfananisha na Allaah na huo ndio ushirikina.
 
Shekhe mkuu akiwa kwenye ibada hiyo ameagiza kuwa mashekhe wa mikoa yote, wilaya hadi kwenye kata, wafanye ibada ya kumwombea Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.
Huu ndio wakati wa kujua CCM inamiliki misikiti mingapi nchini...

Bila kuyasahau makanisa yanayomilikiwa na c CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…