Pre GE2025 Mashekhe wafanya ibada na kuomba majini yasaidie Rais Samia kushinda kwenye uchaguzi ujao

Pre GE2025 Mashekhe wafanya ibada na kuomba majini yasaidie Rais Samia kushinda kwenye uchaguzi ujao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yule Mzee Hamid Jongo ni msomi mzuri tu ila njaa ndizo zinamfanya awe chawa wa mufti na chawa wa kila anayeweza kumpatia hela ya kwenda bucha.!.
Ni mzee anayependa kulakula sana ndiyo maana mwezi wa Ramadhani iliyopita akiwa anasomesha msikitini alitoa maoni ya kumkosoa Proffessor Janabi akidai kwamba maelekezo anayoyatoa ya watu kupunguza kula vyakula vyenye wanga watu watakimbiwa na wake zao kwa kushindwa kuwahudimia kitandani.!

KIELIMU Nimewahi kumsikia Mzee huyu ambaye ni imamu wa msikiti wa Manyema DSM alieleza historia yake ya kusoma kuwa amasoma chuo kikuu cha kiislamu cha Madina nchini Saudi Arabia.
Madina Islamic University.
Mwaka wake wa kuhitimu taasisi ya mufti wa zamani wa zamani wa Saudi Arabia marehemu sheikh Abdul Aziz bi Abdillaah bin Baaz رحمة الله تعالى عليه
ilikuwa inatoa ajira kwa wahitimu wa mataifa mbalimbali kutumikia dini ya kiislamu katika nchi zao na kupata mshahara Moja kwa moja toka ofisi ya Mufti wa Saudi Arabia.
Kwa bahati mbaya sheikh Jongo alifika ofisi ya Mufti amechekewa na mtu wa mwisho kuajiriwa ni yule aliyekuwa mbele ya sheikh Jongo kwenye foleni ya kutafuta ajira na siku hiyo ilikuwa siku ya mwisho wa zoezi la utoaji wa ajira kwa wahitimu wa kigeni hivyo Sheikh Jongo akarudi bila ajira na ndiyo maana kaamua kuwa mtu wa kujipendekeza kwa mufti wa BAKWATA ( Mimi binafsi huwa sipendi kumuita mufti wa TZ au sheikh mkuu wa TZ bali nasema ni sheikh mkuu wa BAKWATA )ili aweze kupata hela ya mboga.
Hali ya Mzee huyu kusoma kisha kuficha elimu yake haishangazi kwasababu moja ya watu waliopata bahati ya kusoma chuo alichosoma Sheikh Jongo Madina Islamic University ni mtu mmoja maarufu sana bongo movie Mzee Ahmed Olotu au maarufu Mzee Chilo.
Duh 🙄 !
Watu wengine hawajui kuwa tunakula ili tuishi, hatuishi ili tule 😁🤣🤣
Kumbe mzee anajitoa ufahamu ili tu atimize matamanio yake !
Hatari sana !
Maneno aliyoyatamka hayawezi kutamkwa na mtu aliyeisoma dini akaielewa !
 
Swali lako ni muhimu sana, japo likikosa JAWABU sahihi washirikina watapata kichochoro Cha kuhalalisha ushirikina wao.
Ni kweli Allaah ametumrisha kila tunaposwali tuseme
katika Aya ya 5 ya suuratul faatiha:
{ إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ }
"Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada."

Lakini ni Allaah huyohuyo aliyesema katika Aya ya 2 ya suuratul maaidah:
وَتَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡإِثۡمِ" وَٱلۡعُدۡوَٰنِۚ
" Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui."
Aya 2 hizi hazipungani na maelezo yake kama walivyoeleza wanachuoni ni kama ifuatavyo;.
1️⃣ Kumuomba msaada binadamu mwenzio anayeendelea kuishi ( sio mfu, maiti, marehemu )
katika jambo ambalo lipo katika uwezo wake wa kibinaadamu kama kukusaidia au kukukopesha pesa, kukubebea mzigo, kupeleka ujumbe fulani kwa binadamu wengine, kukutibu ugonjwa ulionao kama anayo elimu ya matibabu ( sio kuonyesha! Daktari anatibu, Allaah anaponyesha akitaka ) kusaidiana huku ni HALALI na ndio kusudio la Aya ya pili katika suuratul Maaidah.
2️⃣. Kumuomba msaada binadamu mwenzio ambayo yapo nje ya uwezo wa kibinadamu kama kuleta mvua, kuotesha mimea, kuponyesha maradhi ( sio kutibu!, daktari anatibu , Allaah anaponyesha akitaka )
kufufua wafu na mengineyo yaliyopo nje ya uwezo wa binadamu katika hali ya kawaida kusaidiana huku ni HARAMU.
3️⃣. KUWAOMBA MSAADA WATU WALIOKUFA HATA KAMA NI MITUME NA MANABII NI HARAMU.Wale waislamu wanaodai kufanya kisomo cha Albadiri kisomo hicho ni haramu kwa sababu huwa wanawaomba wafuasi wa Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم waliopigana vita pamoja na mtume katika eneo maalumu linaloitwa Badru.
Kwahiyo ukisikia kisomo cha Albadiri ni KUWAOMBA MASHUJAA WA VITA VYA BADRU. HARAMU.

4️⃣. Kuwaomba viumbe wasioonekana kwa macho ya kawaida kama malaika , majini na mashetani ( majini waovu ) pia ni HARAMU.
Kwahiyo ni haramu kuomba msaada kwa majini hata jambo jema?
 
Najaribu ku imagine this way; muumini mmoja wa Kikristo asimame kanisani halafu asifie uchawi na kumuombea kiongozi yeyote wa Kikristo kwamba mashetani yamlinde, narudia hayo maneno ayatamkie kanisani, waumini wasikie, wapita njia wasikie na ma askofu wa hilo kanisa pamoja na wachungaji wapo humo, najaribu tu ku imagine what will happen. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Ukristo na uislamu wallah
Wengine hufanya mizaha mahali hapastahili kufanya mzaha !
Hatari sana !
 
inawezekana hadi sasa tunaongozwa na majini ndio maana maisha ni magumu sana mtaani, Ni wapumbavu wale wote wanaoomba wajini yawasaidie ktk mambo yao..tutayakemea kwa Jina la Yesu yafe kabisa....apigiwe kura mwanaume na ashinde...atoke upande wowote wa chama cha siasa...biashara ya majini piga chini
 
Hiyo ndo laana yenu kamwe haitowaacha mmeweza kwa manabii mtashndwa vipi kwa binadamu?
Juzi tuu hapa Papa Francis kaleta uzushi na kiroja cha ajabu eti kaongea na mungu awabariki LGBT...bado mtasema na mnaamini lkn hamchoki kutafuta uzushi juu ya uislamu mara ugaidi mara majini alimradi litakokupendeza...
Hebu weka link tumsikie tujiaminishe.
 
Kwhy hiyo clip yametajwa majini?au Samia ndo Rais wa kwnz kuombewa na viongozi wa dini?...uzushi ndo laana mliyopewa wagalatia...kwani uzushi wa Papa Francis awabariki LGBT hukuhusikia?...kwmb aliongea na mungu?
Majini yametajwa, haujaisikiliza?
 
Kwahiyo ni haramu kuomba msaada kwa majini hata jambo jema?
Sio majini tu hata malaika haturuhusiwi kuwaomba kwasababu kiwataka msaada ni kuwatoa kwenye majukumu yao waliyopangiwa ambayo ni kumtii Allaah yale anayowaamrisha na sio kusikiliza maombi ya wanaadamu.
Upande wa malaika wote ni wema.
Hakuna malaika muovu hata mmoja ila ndio kama nilivyosema kwamba kujibu maombi ya wanaadamu sio sehemu ya majukumu yao ila pale Allaah anapowaamrisha kumnusuru au kumpa nguvu mwanadamu basi hufanya hivyo kwa kumtii Mola wao.
Ama kuhusu MAJINI WAMEGAWANYIKA WEMA NA WAOVU!
Na unapomuomba msaada huna elimu ya kukujulisha kuwa jini unayemuomba msaada ni mwema au ni muovu, ana uwezo wa kufanya hicho unachomuomba au hana uwezo?!
Hawa viumbe wamepewa uwezo wa kutuona ila sisi hatuwaoni!
Mimi ni mwalimu wa madrasa na kiarabu ninakijua kiasi chake!.
HIVYO VITABU WANAVYOTUMIA AKINA DR SULE KIVUTA MAJINI NIMEWAHI KUVITIPIA JICHO KIDOGO!
Ili kimvuta jini aweze kukufanyia mambo unayoyataka kuna proces ndefu ya kupitia mambo mengi ya ukafiri na madhambi.
Kwa mfano jini ili kumuita aweze kufuata maelekezo yako unaweza kuambiwa ukadumbukize msahafu chooni, uandike Aya kadhaa za Quran kwa kutumia damu ya hedhi , ukae siku 40 bila kuoga wala kutawadha na mambo mengine ya madhambi kabla hujafika hapo kwenye kuchinja mnyama mwenye sifa na rangi maalumu ili kumpa jini sadaka ya damu.
Kumtumia jini lazima uingie katika ukafiri kwakuwa ni maelewano na mikataba na makubaliano maalumu, nifanyie hiki nikufanyie kile hakuna jini anayetoka msaada kwa binadamu bila masharti ya kumkufuru Mungu, labda binadamu huyo awe Nabii na mtume kama ilivyokuwa kwa Nabii Suleymani.
 
Mashekhe waliokutana chini ya Shekhe Mkuu Mufti Abbakari, kwenye msikiti wa kwa Mtoro, jijini Dar es Salaam wamefanya ibada maalum ya kumwombea Rais Samia ashinde kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Shekhe mkuu akiwa kwenye ibada hiyo ameagiza kuwa mashekhe wa mikoa yote, wilaya hadi kwenye kata, wafanye ibada ya kumwombea Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.

Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.

SWALI:
Tukiyaamini maneno ya mashekhe hawa, ina maana uchaguzi wa safari hii utakuwa ni ushindani kati ya wanadamu na majini? Kama majini yakishinda, huyu Rais atakuwa wa wanadamu wa Tanzania au atakuwa Rais wa majini?

Wananchi wanapomchagua kiongozi wao, matarajio yao ni kuwa huyo wanayemchagua atawaongoza katika jitihada zao za kuyafikia maendeleo, sasa kama majini yatamchagua mgombea kuwa Rais, hayo majini yanatarajia kunufaika vipi na huyo yaliyempigania?

Wataalam wa majini tunaomba litoleeni ufafanuzi hili la mashekhe kuomba majini yamsaidie Rais Samia, inamaanisha nini katika tafsiri pana?
View attachment 3222655
View attachment 3222658
Inafikirisha sana
 
Aliyeongea maneno yenye Ushirikina ndani yake sio Shehe bali ni mzee muumini tu wa kawaida ambaye kwa yale matamshi yake anajidhihirisha kuwa hana Elimu yeyote ya Dini zaidi ya kwenda kusali tu msikitini !

Shehe na mwanazuoni ni yule Mufti aliyeongea mwanzoni na ndio maana huwezi kumsikia akisema Eti majini yamuombee mtu fulani !
Wasingempa platform, amewadhalilisha hao wengine inaonekana lao ni moja. Yuko high table na anaongea maneno yanayodhalilisha dini yake kusema ataomba majini yamsaidie rais. Watu distinguished wanapokaa huwa kuna utaratibu maalum wa kuongea, haiwezekani kila mtu asimame na kuongea anavyojisokia.
 
Nakuunga mkono.
Waliokuwa kwenye kile kikao lao Moja! Na hayo ni machache waliyoyaropoka kama bahati mbaya lakini huko sirini hutenda na kusema mabaya kushinda hayo ambayo hawako tayari kuyaweka hadharani isipokuwa kwa watu maalumu ambao huwafuata kuomba kutatuliwa shida zao ikiwa pamoja na WANASIASA ambao huwafuata katika vipindi kama hivi vya kuelekea kwenye uchaguzi kuwaomba wawafanyie makafara waweze kushinda ubunge na udiwani.
Hiki ni kipindi cha makuhani kula vizuri na kunenepa kutokana na hela za WANASIASA wanazomwaga ili wafanyiwe utaalamu uchaguzi uwaendee vizuri.
 
Usidanganye watu kuwa eti nchi za kiislam ni tajiri, ni uwongo mkubwa.

Soma hapo chini, labda utaijiwa na akili:

Is Yemen a rich or poor country?

Despite possessing significant oil and gas resources and a considerable amount of agriculturally productive land, Yemen remains one of the poorest of the world's low-income countries. In 2018, more than 80 percent (2018) of the population lived in poverty.

Does Lebanon have a good economy?

Lebanon's economic and financial crisis ranks among the worst economic crises globally since the mid-nineteenth century

Malaika hawashikamani na majini. Kiimani, hata ukimwomba Mungu, halafu ukamwunganisha katika maombi na shetani, atakuacha na shetani wako. Ni sawa utangaze kuomba msaada kutoka kwa majambazi na watu wema, watu wema watakuacha na majambazi yako.

Malaika hawasaidiani na mashetani katika utendaji wao.
Hajatajwa shetani wametajwa majini, suala la majini kuwa ni malaika(waliyoasi) ni mtazamo wa wakristo ila waislamu kwao majini ni viumbe ambao si malaika wala si binaadamu. Sijawahi kuelewa kwanini hao malaika waliyoasi waitwe majini.
 
Sio majini tu hata malaika haturuhusiwi kuwaomba kwasababu kiwataka msaada ni kuwatoa kwenye majukumu yao waliyopangiwa ambayo ni kumtii Allaah yale anayowaamrisha na sio kusikiliza maombi ya wanaadamu.
Upande wa malaika wote ni wema.
Hakuna malaika muovu hata mmoja ila ndio kama nilivyosema kwamba kujibu maombi ya wanaadamu sio sehemu ya majukumu yao ila pale Allaah anapowaamrisha kumnusuru au kumpa nguvu mwanadamu basi hufanya hivyo kwa kumtii Mola wao.
Ama kuhusu MAJINI WAMEGAWANYIKA WEMA NA WAOVU!
Na unapomuomba msaada huna elimu ya kukujulisha kuwa jini unayemuomba msaada ni mwema au ni muovu, ana uwezo wa kufanya hicho unachomuomba au hana uwezo?!
Hawa viumbe wamepewa uwezo wa kutuona ila sisi hatuwaoni!
Mimi ni mwalimu wa madrasa na kiarabu ninakijua kiasi chake!.
HIVYO VITABU WANAVYOTUMIA AKINA DR SULE KIVUTA MAJINI NIMEWAHI KUVITIPIA JICHO KIDOGO!
Ili kimvuta jini aweze kukufanyia mambo unayoyataka kuna proces ndefu ya kupitia mambo mengi ya ukafiri na madhambi.
Kwa mfano jini ili kumuita aweze kufuata maelekezo yako unaweza kuambiwa ukadumbukize msahafu chooni, uandike Aya kadhaa za Quran kwa kutumia damu ya hedhi , ukae siku 40 bila kuoga wala kutawadha na mambo mengine ya madhambi kabla hujafika hapo kwenye kuchinja mnyama mwenye sifa na rangi maalumu ili kumpa jini sadaka ya damu.
Kumtumia jini lazima uingie katika ukafiri kwakuwa ni maelewano na mikataba na makubaliano maalumu, nifanyie hiki nikufanyie kile hakuna jini anayetoka msaada kwa binadamu bila masharti ya kumkufuru Mungu, labda binadamu huyo awe Nabii na mtume kama ilivyokuwa kwa Nabii Suleymani.
SI kwamba hapo umeelezea aina ya majini ambao ni waovu tu(mashetani)?
 
Kwanini muumini wa kikristo amuombee kiongozi wa kikristo ?! Kwani muumini wa kikristo hawezi kumuombea kiongozi muislamu ?! Na je muumini muislamu hawezi kumuombea kiongozi mktisto ?!
Je mnadhani huyu mufti na chawa wake wamemuombea mama Samia kwakuwa tu ni muislamu ?
Kama mnaamini hivyo mnakosea sana!
Bakwata ni watu wa kujipendekeza kwa kila mtawala ambaye yuko madarakani bila kujali ni muumini wa dini gani!
Hivi miaka minne tu mmeishasahau nmna mufti alivyokuwa karibu sana na Magufuli ?!
Ukaribu wa BAKWATA na Magufuli ilikaribia watu kuamini kwamba Magufuli asingekufa mapema labda alikuwa na mpango wankusilimu!.
Hata hivyo kama angesilimu angeangukia katika huu uislamu wa bakwata wa kuomba majini na hapo angekuwa karuka mavi na kukanyaga mkono!.
BAKWATA ni moja ya jumuia za CCM kama ilivyo UVCCM.
 
SI kwamba hapo umeelezea aina ya majini ambao ni waovu tu(mashetani)?
Wewe uwezo wa kutofautisha jini mwema na jini muovu (shetani ) unautoa wapi bila kuingia katika vitabu vya elimu za uchawi ambavyo ndivyo vinaelekeza namna ya kuanzisha mawasiliano na urafiki na majini?!
Elewa kwamba majini ni jamii ya viumbe tofauti na sisi wanaadamu na wamepewa uwezo wa kutuona sisi ila sisi hatuwaoni, na hao majini wema. Allaah hajawapa mamlaka ya kutatua shida za wanaadamu bali yatakiwa wanaadamu wasaidiane wenyewe kwa wenyewe katika mambo mema, na majini nao wasaidiane wenyewe kwa wenyewe katika mambo mema.
Elimu yoyote inayoelezea namna ya kuanzisha mawasiliano na mahusiano na majini ni katika elimu za uchawi ambazo ni haramu kujifundisha elimu hizo.
 
Kwahiyo ni haramu kuomba msaada kwa majini hata jambo jema?
Wewe unaombaje msaada kwa kiumbe ambaye humuoni? ! Wajuaje kama muda huo anakusikia?! Wajuaje kama muda huo amelala au Yuko mbali sana na wewe ?! Hakuna namna ya kuhakikisha kuwa unachokiomba kwa majini kinapatikana bila kujifunza elimu ya uchawi tuliyoletewa huku Afrika na baadhi ya waarabu waliojivika sura na matendo ya kiislamu wakatuchanganyia haki na batili na sisi kutokana na ujinga tukashindwa kutofautisha karama na uchawi!
Allaah peke yake ndiye twatakiwa kumuomba hali ya kuwa hatumuoni.
Mwingine yeyote utakayemuomba hali ya kuwa haumuoni utakakuwa umemfananisha na Allaah na huo ndio ushirikina.
 
Shekhe mkuu akiwa kwenye ibada hiyo ameagiza kuwa mashekhe wa mikoa yote, wilaya hadi kwenye kata, wafanye ibada ya kumwombea Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.
Huu ndio wakati wa kujua CCM inamiliki misikiti mingapi nchini...

Bila kuyasahau makanisa yanayomilikiwa na c CCM
 
Back
Top Bottom