yapo hadi majini ya kwenye kikwapa 😂😂😅
Kulingana na imani ya kiislamu iliyofundishwa na mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم
A. Binadamu tumeumbwa kutokana na udongo.
B. Malaika wameumbwa kutokana na nuru ( mwanga ) na
C. Majini wameumbwa kutokana na moto.
D. Malaika na majini Allaah amewapa uwezo wa kujigeuza maumbo mbalimbali kama vile kujivika sura ya kibinadamu nk.
E. Malaika wanapojivika sura ya kibinadamu hujivika sura ya mwanadamu mwanaume mwenye sura, umbo , mavazi na mwonekano mzuri.
F. Majini ndio hujigeuza katika maumbo mbalimbali mazuri kwa mabaya kama wanyama, wadudu , ndege nk, kulingana na mahitaji pia kulingana na aina ya jini,dini yake, dhehebu lake nk kwa kuwa kulingana na mafundisho ya Quran majini pia wapo katika dini, madhehebu na makundi tafauti.
Yapo majini waislamu, hao waislamu kama ilivyokuwa kwetu sisi waislamu wa kibinadamu waislamu wakijini pia wapo katika madhehebu na makundi mbalimbali.
Pia yapo majini ya kikristo , kiyahudi, kibudha nk na hayo pia yapo pia katika madhehebu na makundi mbalimbali kama majini ya kikatoliki, kianglikana, kipentekoste, kiorthodox, kilutheri nk.
G. Katika hadithi ya mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم
iliyopokelewa na Imamu Albukhary kutoka kwa swahaba Alliy bin Alhusain kasema mtume :
"إِنَّ الشَّيْطَانَ يَجْرِي مِنَ الْإِنْسَانِ مَجْرَى الدَّمِ"
( Hakika shetani anatembea ndani ya mwanadamu kupitia njia ( mishipa ) ya damu".
Hadithi hii sahihi inathibitisha kuwa shetani anao uwezo wa kujigeuza kiumbe mdogo sana sawa na kirusi au bakteria na kuingia katika mwili wa mwanadamu kupitia mishipa ya damu akaenda hadi kwenye ubongo au kwenye moyo wake akamtia maradhi au kumshawishi kutenda matendo mabaya yenye kumchukiza Allaah , bali hata kuwachukiza binadamu wengine kwa kumfanya mwanadamu huyu kwa nguvu ya shetani aliyemwingia afanye matendo yenye kumchonganisha na jamii iliyomzunguka.