Mashindano ya Draft - Ronaldo Awa Bingwa Kwa Kumfunga Issa Mamba

Mashindano ya Draft - Ronaldo Awa Bingwa Kwa Kumfunga Issa Mamba

Vipi Noel alikuwepo? Au Amani Siri maarufu kama Mchunguzi, Bad Face je.
Mangwelele vp anacheza au anaangalia maana jamaa anajua bao hadi kashauriwa na dokta asicheze draft.
noel yupo njombe
 
Vipi Noel alikuwepo? Au Amani Siri maarufu kama Mchunguzi, Bad Face je.
Mangwelele vp anacheza au anaangalia maana jamaa anajua bao hadi kashauriwa na dokta asicheze draft.

Mangwelele hachezi kabisa.

Noel hakuwepo, sina uhakika na Amani Siri, ila top 4 hakuwepo.

Imepangwa ligi ya watu 4 itakayofanyika Dodoma kumthibitisha bingwa (Ronaldo).

Itakuwa na Noel, Ronaldo, Simba wa Dodoma mtu wa nne sijampata vizuri.
 
Jana nilipata bahati ya kushuhudia Nusu Fainali pamoja na Fainali ya mashindano ya Draft yaliyofanyika Kinondoni - Manyanya.

Washiriki walikuwa 32, na walioingia nusu ilikuwa:

Ronaldo vs Jamaa mmoja sikulipata jina lake (nadhani ni Salehe au Sahia), Ronaldo alishinda 3 - 1.

Issa Mamba vs Dogo Yassin, Issa Mamba alishinda 3 bila.

Fainali Ronaldo aka Christian Bela akimshinda Issa (Meno ya Mamba) goli 3 kwa 1.

Wao wanasema ilikuwa ni warm up wakisubiria ligi ambayo mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 1.

Kwa mara ya kwanza niliweza kuwaona mabingwa ambao nimekuwa nikiwasikia kwenye vijiwe tofauti tofauti vya madraft.

Baadhi yao ni Mangwelele, Nduli, Dogo Sisqo, Dogo Yassin, Bedui (kawa chapombe siku hizi), Chaula, Ronaldo na Issa Mamba.

Nilifurahi sana kumwona Mangwelele aisee.
Hongera, mi sijawahi kumuona hata mmoja, ila nasikia ronaldo hatari sana
 
Akajinoe upya, draft mchezo mzuri sana, akina mangurere inabidi wafungue centres za kuendeleza hii michezo.
Mangwelele amebaki kwenye kitengo cha utafiti wa mabao magumu na kufundisha mbinu kwa vijana.

Kijana wake Issa aka Meno Ya Mamba anajitahidi naye, ndiye aliingia Fainali dhidi ya Ronaldo.
 
Akajinoe upya, draft mchezo mzuri sana, akina mangurere inabidi wafungue centres za kuendeleza hii michezo.

Issa yuko njema sana, magoli yote matatu aliyofungwa ilikuwa ni makosa madogo sana.

Ambapo kuna moja ilikuwa iwe sare, na lingine ilikuwa Ronaldo ndo afungwe.
 
nitawaibukiwa siku nikipata nafasi, japo wazee wa dar nawaheshimu mwaka 2017 niliburuzwa sana pale mapipa.

Hao jamaa hizo ndo shughuli zao, watu wanakesha hapo kwenye madanali.

Wako vizuri aisee, mimi nafurahia sana kuangalia jamaa wanavyocheza, ila hata kuambulia kitu hakuna, maana kumbukumbu sina kabisa.
 
Hao jamaa hizo ndo shughuli zao, watu wanakesha hapo kwenye madanali.

Wako vizuri aisee, mimi nafurahia sana kuangalia jamaa wanavyocheza, ila hata kuambulia kitu hakuna, maana kumbukumbu sina kabisa.
Umenikumbusha kitambo sana...

Halafu huu mchezo sijui upo vp, at least kwa upande wangu!!!

Enzi hizo ilikuwa nikicheza na watu wengine, ilikuwa wafanye kazi hasa... in short, mara nyingi kama sio zote nilikuwa najihakikishia ubingwa!!!

Kinyume chake, kulikuwa na Side Boy (RIP) na West... hawa walikuwa washikaji zangu wakubwa, tangu tukiwa vijana wadogo hadi kesho!!

Hawa wadudu, wote wawili, walikuwa wananisumbua sana...

Ingawaje kwa wengine walikuwa wanapigwa, nikikutana nao lazima wanitoe nishai, ama droo za kumwaga!!

Sijui walikuwa wananipatia wapi hawa, sema dah, games zetu zilikuwa zinavuta watu hasa!!
 
Back
Top Bottom