- Thread starter
- #41
Umenikumbusha kitambo sana...
Halafu huu mchezo sijui upo vp, at least kwa upande wangu!!!
Enzi hizo ilikuwa nikicheza na watu wengine, ilikuwa wafanye kazi hasa... in short, mara nyingi kama sio zote nilikuwa najihakikishia ubingwa!!!
Kinyume chake, kulikuwa na Side Boy (RIP) na West... hawa walikuwa washikaji zangu wakubwa, tangu tukiwa vijana wadogo hadi kesho!!
Hawa wadudu, wote wawili, walikuwa wananisumbua sana...
Ingawaje kwa wengine walikuwa wanapigwa, nikikutana nao lazima wanitoe nishai, ama droo za kumwaga!!
Sijui walikuwa wananipatia wapi hawa, sema dah, games zetu zilikuwa zinavuta watu hasa!!
Hapo kwa hao jamaa zako ni kwamba miguu yako yote wanaijua, na wanakuwa wanaweza ku-predict move zako kwa sababu ya kucheza muda mrefu na wewe.
Hata hawa mabingwa huwa wakikutana wa kambi moja utaona sare zinakuwa nyingi sana kwa sababu copy zao zote wanazo (wanajuana).
Na Bingwa akifungwa mchezo fulani atatafuta mtu wa kumwelekeza jinsi ya kutoa sare au kushinda hiyo game, na unakuta anaanza kutafuta either kutoka kwenye kambi yako au anaenda moja kwa moja kwa mtaalamu Mangwez.