Mashindano ya Draft - Ronaldo Awa Bingwa Kwa Kumfunga Issa Mamba

Vipi Noel alikuwepo? Au Amani Siri maarufu kama Mchunguzi, Bad Face je.
Mangwelele vp anacheza au anaangalia maana jamaa anajua bao hadi kashauriwa na dokta asicheze draft.
noel yupo njombe
 
Vipi Noel alikuwepo? Au Amani Siri maarufu kama Mchunguzi, Bad Face je.
Mangwelele vp anacheza au anaangalia maana jamaa anajua bao hadi kashauriwa na dokta asicheze draft.

Mangwelele hachezi kabisa.

Noel hakuwepo, sina uhakika na Amani Siri, ila top 4 hakuwepo.

Imepangwa ligi ya watu 4 itakayofanyika Dodoma kumthibitisha bingwa (Ronaldo).

Itakuwa na Noel, Ronaldo, Simba wa Dodoma mtu wa nne sijampata vizuri.
 
Hongera, mi sijawahi kumuona hata mmoja, ila nasikia ronaldo hatari sana
 
Akajinoe upya, draft mchezo mzuri sana, akina mangurere inabidi wafungue centres za kuendeleza hii michezo.
Mangwelele amebaki kwenye kitengo cha utafiti wa mabao magumu na kufundisha mbinu kwa vijana.

Kijana wake Issa aka Meno Ya Mamba anajitahidi naye, ndiye aliingia Fainali dhidi ya Ronaldo.
 
Akajinoe upya, draft mchezo mzuri sana, akina mangurere inabidi wafungue centres za kuendeleza hii michezo.

Issa yuko njema sana, magoli yote matatu aliyofungwa ilikuwa ni makosa madogo sana.

Ambapo kuna moja ilikuwa iwe sare, na lingine ilikuwa Ronaldo ndo afungwe.
 
nitawaibukiwa siku nikipata nafasi, japo wazee wa dar nawaheshimu mwaka 2017 niliburuzwa sana pale mapipa.

Hao jamaa hizo ndo shughuli zao, watu wanakesha hapo kwenye madanali.

Wako vizuri aisee, mimi nafurahia sana kuangalia jamaa wanavyocheza, ila hata kuambulia kitu hakuna, maana kumbukumbu sina kabisa.
 
Hao jamaa hizo ndo shughuli zao, watu wanakesha hapo kwenye madanali.

Wako vizuri aisee, mimi nafurahia sana kuangalia jamaa wanavyocheza, ila hata kuambulia kitu hakuna, maana kumbukumbu sina kabisa.
Umenikumbusha kitambo sana...

Halafu huu mchezo sijui upo vp, at least kwa upande wangu!!!

Enzi hizo ilikuwa nikicheza na watu wengine, ilikuwa wafanye kazi hasa... in short, mara nyingi kama sio zote nilikuwa najihakikishia ubingwa!!!

Kinyume chake, kulikuwa na Side Boy (RIP) na West... hawa walikuwa washikaji zangu wakubwa, tangu tukiwa vijana wadogo hadi kesho!!

Hawa wadudu, wote wawili, walikuwa wananisumbua sana...

Ingawaje kwa wengine walikuwa wanapigwa, nikikutana nao lazima wanitoe nishai, ama droo za kumwaga!!

Sijui walikuwa wananipatia wapi hawa, sema dah, games zetu zilikuwa zinavuta watu hasa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…