Mashindano ya Drafti kitaifa

Darius RR

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2019
Posts
385
Reaction score
793
Mashindano makubwa ya Draft Tanzania yanatarajiwa kufanyika Tar 7 July, 2021

Mshindi wa kwanza anatarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi 700,000/-.

Yamepangwa kufanyikia Kinondoni Manyanya.

Mafundi wote unaowajua wanatarajiwa kuwepo.

Baadhi ya mafundi wanaotarajiwa kuwepo ni:

Ronaldo (Field Marshall), Noel, Issa (Meno ya Mamba), Nduli, Dogo Sisqo, Dogo Yassin, Simba Dodoma, Shabani Katoto, Hemedi Gaidi na wengine wengi.

Mtaalamu Mkuu wa Madraft Mr Mangwelele atakuwa mmoja wa waratibu.

Tutaendelea kupeana updates za nini kitakachojiri na kama kuna mabadiliko yoyote.

Update: Mashindano yameahirishwa mpaka Tar 8 August.
 
Ungeeni na milard ayo tukio liwe live youtube tatizo mnapofeli ni sehemu moja tu huwa hatuoni hata video clips za fainali ilikuwaje mnaishia kutuletea taarifa ya kuwa kutakuwa na mashindano tu

Wazo zuri sana hili.

Changamoto ni gharama, maana Fainali au Game za mitoano zinakuwa ni games 24, sasa imagine game 24 zitatumia muda gani?
 
Wazo zuri sana hili.

Changamoto ni gharama, maana Fainali au Game za mitoano zinakuwa ni games 24, sasa imagine game 24 zitatumia muda gani?
Hapo kweli kuna ugumu ila mkiongea nao wao kama watangazaji wanaweza kujua cha kufanya hata kutengeneza documentary na mjumuiko wa video clips ukawekwa mtandaoni na tukauona baada ya mashindano
 
Hapo kweli kuna ugumu ila mkiongea nao wao kama watangazaji wanaweza kujua cha kufanya hata kutengeneza documentary na mjumuiko wa video clips ukawekwa mtandaoni na tukauona baada ya mashindano

Nitajaribu kuongea na Millard, anaweza kushauri nini cha kufanya.

Faida moja ya kupata coverage kwa Millard inaweza kuongeza au kupata wadau wanaoweza kushauri nini cha kuongeza kwenye mashindano.
 
Kamati ya ufundi iko chini ya Mshana Jr
 
Nitajaribu kuongea na Millard, anaweza kushauri nini cha kufanya.

Faida moja ya kupata coverage kwa Millard inaweza kuongeza au kupata wadau wanaoweza kushauri nini cha kuongeza kwenye mashindano.
Ntafurahi nikisikia mmefanya hivyo. Wao wanajua ni kazi yao wanaweza kushauri na kupromot zaidi shindano hilo na hata kulifanya lisikike nchi nzima na kusababisha hata wadhamini kujitokeza zaidi kwa mashindano yajayo who knows? Leo laki saba kesho mnajikuta washiriki wanagombania milioni tano!!!
 
Nitaongea na jamaa nione anashauri nini, nitaleta mrejesho.

Jumatatu nitapata muda wa kuongea naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…