Sasa mnasema washiriki watapitishwa na mikoa yao.,... Wakati we ndio unachagua mikoa.
Lindi, mtwara, znz, pwani, tanga, tabora....
Kuna mabingwa wa draft saana, nyinyi km wasimamiz ndio mlitakiwa kuratibu na sio kusubiria.
Km ndivyo msiite basi kuwa bingwa wa taifa, we unashndana na mtu toka Arusha unajiita bingwa, arusha sijui kilimanjaro na draft ni wap na wap.
Huu ujinga ndio unafany hii michezo ionekane ya kipumbavu
Sent using
Jamii Forums mobile app
naomba nikusaidie hapa , wanaposema washiriki watapitishwa na mikoa yao wana maana hii, mfano Iringa wachezaji wazuri wa draft tunawajua , sasa ni sisi wanairinga kuamua kupendekeza ni nani akatuwakilisha baada ya kujadiliana kwenye club zetu au kuamua kuandaa mashindano ambayo yatawakilisha wachezaji wotee wa mkoa afu mshindi atashinda ticket ya kwenda kutuwakilsha Dar es salaam katika mashindano ya kitaifa.
Baadhi ya mikoa kutokuwepo kabisaa , hii inatokana na mikoa hiyo kutokuwa na clubs za mchezo wa draft na kupelekea ugumu fulani katika kuwasiliana na wahusika wa mkoa usika lkn pia baadhi ya mikoa kutokuwa na upenzi na huu mchezo au kutokucheza huu mchezo katika sheria pendekezwa hapo juu. Mwisho ni baadhi ya mikoa (katika historia ) kutoa wachezaji wenye uwezo mdogo mnoo .
Unajua huu mchezo haupo kama wengi wajuavyo . Hawa wenzetu wa dar wametuzidi pakubwa mno ktk huu mchezo, kuna kigezo hapo cha omary john 14 hivi hapo umekielewa hicho kigezo ?
- ngoja nikufahamishe ni hivi, wachezaji wengi wanajiona au wanaitwa mabingwa kwasababu ana namna fulani ya kucheza huu mchezo , lkn katika omary john kila mcheza anatakiwa aanze kete zote 7 za vyumba vya mwanzo yaani anatakiwa aanze
Pasati , nugza , meja , kavimba, taa ya treni , mabano na tege . sasa wachezaji wengi wa mikoani utakuta anajua meja lakini mabano hajua au tege hajui , sasa mikoa iliyotajwa kidogo wanaufahamu juu ya hiyo sheria ya omary- john
Kwanin wanaiita omary- john ni kama njia ya kuwaanzi wachezaji wa wili omary na john ambao walipenda kucheza katika utaratibu huo wa kuanza kete zote za mwanzo na kuzipa majina niliyotaja hapo juu.
- Katika mchezo unaoitwa tege . Kuna sheria imesema watacheza tege 4. kwanini wamesema tege na siyo meja , nugza au pasati ?
ni hivi tege ni mchezo unaotaka mchezaji aanze kete ambayo wachezaji wengi wanaamini ni kete dhaifu kama utaanza na kupelekea ufungwe kirahisi na mpinzani wako. Sasa kwasababu wengi wanajua hii itapelekea sare ziwe nyingi na kupelekea mashindano yawe marefu , hivyo kwa kupendekeza wacheze tege basi tunaweza kuokoa muda kwa kuepusha sare zisiwe nyingi.