Mashindano ya kumtafuta bingwa wa draft Tanzania 2022

Mashindano ya kumtafuta bingwa wa draft Tanzania 2022

Daah
naomba nikusaidie hapa , wanaposema washiriki watapitishwa na mikoa yao wana maana hii, mfano Iringa wachezaji wazuri wa draft tunawajua , sasa ni sisi wanairinga kuamua kupendekeza ni nani akatuwakilisha baada ya kujadiliana kwenye club zetu au kuamua kuandaa mashindano ambayo yatawakilisha wachezaji wotee wa mkoa afu mshindi atashinda ticket ya kwenda kutuwakilsha Dar es salaam katika mashindano ya kitaifa.

Baadhi ya mikoa kutokuwepo kabisaa , hii inatokana na mikoa hiyo kutokuwa na clubs za mchezo wa draft na kupelekea ugumu fulani katika kuwasiliana na wahusika wa mkoa usika lkn pia baadhi ya mikoa kutokuwa na upenzi na huu mchezo au kutokucheza huu mchezo katika sheria pendekezwa hapo juu. Mwisho ni baadhi ya mikoa (katika historia ) kutoa wachezaji wenye uwezo mdogo mnoo .

Unajua huu mchezo haupo kama wengi wajuavyo . Hawa wenzetu wa dar wametuzidi pakubwa mno ktk huu mchezo, kuna kigezo hapo cha omary john 14 hivi hapo umekielewa hicho kigezo ?
- ngoja nikufahamishe ni hivi, wachezaji wengi wanajiona au wanaitwa mabingwa kwasababu ana namna fulani ya kucheza huu mchezo , lkn katika omary john kila mcheza anatakiwa aanze kete zote 7 za vyumba vya mwanzo yaani anatakiwa aanze

Pasati , nugza , meja , kavimba, taa ya treni , mabano na tege . sasa wachezaji wengi wa mikoani utakuta anajua meja lakini mabano hajua au tege hajui , sasa mikoa iliyotajwa kidogo wanaufahamu juu ya hiyo sheria ya omary- john
Kwanin wanaiita omary- john ni kama njia ya kuwaanzi wachezaji wa wili omary na john ambao walipenda kucheza katika utaratibu huo wa kuanza kete zote za mwanzo na kuzipa majina niliyotaja hapo juu.

- Katika mchezo unaoitwa tege . Kuna sheria imesema watacheza tege 4. kwanini wamesema tege na siyo meja , nugza au pasati ?
ni hivi tege ni mchezo unaotaka mchezaji aanze kete ambayo wachezaji wengi wanaamini ni kete dhaifu kama utaanza na kupelekea ufungwe kirahisi na mpinzani wako. Sasa kwasababu wengi wanajua hii itapelekea sare ziwe nyingi na kupelekea mashindano yawe marefu , hivyo kwa kupendekeza wacheze tege basi tunaweza kuokoa muda kwa kuepusha sare zisiwe nyingi.
kumbe huu mchezo una sheria nyingi ambazo ni ngeni masikioni mwa wengi tulio mikoani
 
Nadhani manhwerere ndio icon ya madraft hapa bongo

Sehemu yeyote ile ambapo watu wanacheza draft lazima wanajua jina la mangwerere.

Hao kima sisco, meno ya mamba, yassin ronaldo hawajulikani sana

Sema hapo kuna mwamba kutoka njombe anaitwa noeli sijamuona kwenye list
Mangwerere na kasikio
 
Ungeandika bingwa wa mashindano ya draft ( british). Hata mwanza kuna wachezaji husafiri hadi Nairobi kucheza draft, sema vimwanaume vya dar kazi kujisifia tu eti vinajua draft wakati binti anakupita nyuma hata humtazami makalio 😁😁
Hahaaha nao wadau wa british nao wanapiga vijembe draft la french wanakuambia kucheza french ni kuzidi kupigia kampani ushoga

Kwanini ule mbele na nyuma?
 
Hivi unajua siku hizi yuko wapi? Kuna mwenzake nilisikia akili ziliruka jina silikumbuki vizuri wote walikuwa miamba wakikutana ni droo tupu zinashamiri

Anachezea kirumba,igoma na buhongwa ila Mara nyingi huwa anakuwa kirumba.ila mwezi ujao tutakuwa naye kwenye mabula cup.
 
Nadhani manhwerere ndio icon ya madraft hapa bongo

Sehemu yeyote ile ambapo watu wanacheza draft lazima wanajua jina la mangwerere.

Hao kima sisco, meno ya mamba, yassin ronaldo hawajulikani sana

Sema hapo kuna mwamba kutoka njombe anaitwa noeli sijamuona kwenye list
Hakuna kilinge kikubwa kisichowafahamu hao wanyama uliowataja
 
Back
Top Bottom