French lina complex sana linataka utumbue macho haswaSasa french ndio draft hio nyingine haaitumiki hata vitani hapo UKRAINE.
HATA HIVYO NAWAPONGEZA KWA KUANDAA SHINDANO HILO.
MNAFELI LIVE COVERAGE HATA PICHA TU KUZIWEKA HUMU HAKUNA
Mwanza hawajui draft Mkuu. Hapo wa kulalamika ni TaboraBingwa wa draft Tanzania, mbona mikoa mingine haipo? Mfano Mwanza, Shinyanga, Tabora, Kigoma.
Shinyanga...?[emoji849]Bingwa wa draft Tanzania, mbona mikoa mingine haipo? Mfano Mwanza, Shinyanga, Tabora, Kigoma.
Kwa hiyo french sio draft !!??Hawana rekodi yoyote ya kidraft ,hao wengi wanacheza French
Sasa hilo ndio tunacheza sana Kanda ya ziwa .... Hayo madraft yenu mtu anapita nyuma yako kizembe SI tunakula kichwa ....inabidi uzame sana laboratory kupata majibu 🤣🤣🤣🤣 eti mtu anakatuza nyuma yako na huwezi mfanya kitu daah....French lina complex sana linataka utumbue macho haswa
mkorea mim tu huniwezi , kama unabisha sema tupige game 3 online nikutoe ngeu .Uyo bingwa akipatikana nitahitaji mpambano nae
Akitoa ata sare, nampa laki cash
naomba nikusaidie hapa , wanaposema washiriki watapitishwa na mikoa yao wana maana hii, mfano Iringa wachezaji wazuri wa draft tunawajua , sasa ni sisi wanairinga kuamua kupendekeza ni nani akatuwakilisha baada ya kujadiliana kwenye club zetu au kuamua kuandaa mashindano ambayo yatawakilisha wachezaji wotee wa mkoa afu mshindi atashinda ticket ya kwenda kutuwakilsha Dar es salaam katika mashindano ya kitaifa.Sasa mnasema washiriki watapitishwa na mikoa yao.,... Wakati we ndio unachagua mikoa.
Lindi, mtwara, znz, pwani, tanga, tabora....
Kuna mabingwa wa draft saana, nyinyi km wasimamiz ndio mlitakiwa kuratibu na sio kusubiria.
Km ndivyo msiite basi kuwa bingwa wa taifa, we unashndana na mtu toka Arusha unajiita bingwa, arusha sijui kilimanjaro na draft ni wap na wap.
Huu ujinga ndio unafany hii michezo ionekane ya kipumbavu
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna wachezaji wapo tanzania hiii hii wanakuruhusu utumie dalmax na bado wanakufunga yani hao watu ni zaidi ya software najua huaminiKuna game flani linaitwa 'Dalmax checkers' huwa nalifunga likiwa 100%difficulity
Nadhani kwa kiwango changu ninafaa kwenye hiyo michuano😆
Humjui Cisco, Ronaldo? Noel yupo group E , alikula goli 5 kwa siscoNadhani manhwerere ndio icon ya madraft hapa bongo
Sehemu yeyote ile ambapo watu wanacheza draft lazima wanajua jina la mangwerere.
Hao kima sisco, meno ya mamba, yassin ronaldo hawajulikani sana
Sema hapo kuna mwamba kutoka njombe anaitwa noeli sijamuona kwenye list
Anaitwa nan maana Arusha wataleta bingwa wao, na huwa wanaleta bingwa wao anakufa vzr TU,Nimefurahia hii. Ila kwa draft, hiyo zawadi ya mshindi wa kwanza ni ndogo sana, bora ingekuwa M5.
Kuna mwamba mmoja ''Msomali'' wa Arusha hapo hajawekwa. Huyo jamaa sijawahi kushuhudia akifungwa...kifupi hafungiki labda uambulie droo na uwe unajua sanaa.
Na haongei kabisa wakati wa kucheza na yupo faster ktk kucheza.
Shukran kaka umefafanunua vzr sananaomba nikusaidie hapa , wanaposema washiriki watapitishwa na mikoa yao wana maana hii, mfano Iringa wachezaji wazuri wa draft tunawajua , sasa ni sisi wanairinga kuamua kupendekeza ni nani akatuwakilisha baada ya kujadiliana kwenye club zetu au kuamua kuandaa mashindano ambayo yatawakilisha wachezaji wotee wa mkoa afu mshindi atashinda ticket ya kwenda kutuwakilsha Dar es salaam katika mashindano ya kitaifa.
Baadhi ya mikoa kutokuwepo kabisaa , hii inatokana na mikoa hiyo kutokuwa na clubs za mchezo wa draft na kupelekea ugumu fulani katika kuwasiliana na wahusika wa mkoa usika lkn pia baadhi ya mikoa kutokuwa na upenzi na huu mchezo au kutokucheza huu mchezo katika sheria pendekezwa hapo juu. Mwisho ni baadhi ya mikoa (katika historia ) kutoa wachezaji wenye uwezo mdogo mnoo .
Unajua huu mchezo haupo kama wengi wajuavyo . Hawa wenzetu wa dar wametuzidi pakubwa mno ktk huu mchezo, kuna kigezo hapo cha omary john 14 hivi hapo umekielewa hicho kigezo ?
- ngoja nikufahamishe ni hivi, wachezaji wengi wanajiona au wanaitwa mabingwa kwasababu ana namna fulani ya kucheza huu mchezo , lkn katika omary john kila mcheza anatakiwa aanze kete zote 7 za vyumba vya mwanzo yaani anatakiwa aanze
Pasati , nugza , meja , kavimba, taa ya treni , mabano na tege . sasa wachezaji wengi wa mikoani utakuta anajua meja lakini mabano hajua au tege hajui , sasa mikoa iliyotajwa kidogo wanaufahamu juu ya hiyo sheria ya omary- john
Kwanin wanaiita omary- john ni kama njia ya kuwaanzi wachezaji wa wili omary na john ambao walipenda kucheza katika utaratibu huo wa kuanza kete zote za mwanzo na kuzipa majina niliyotaja hapo juu.
- Katika mchezo unaoitwa tege . Kuna sheria imesema watacheza tege 4. kwanini wamesema tege na siyo meja , nugza au pasati ?
ni hivi tege ni mchezo unaotaka mchezaji aanze kete ambayo wachezaji wengi wanaamini ni kete dhaifu kama utaanza na kupelekea ufungwe kirahisi na mpinzani wako. Sasa kwasababu wengi wanajua hii itapelekea sare ziwe nyingi na kupelekea mashindano yawe marefu , hivyo kwa kupendekeza wacheze tege basi tunaweza kuokoa muda kwa kuepusha sare zisiwe nyingi.
Dalmax Kuna watu wanalipa sare 1 na hakipati TZ hii , watu Kama kina Noel, Sisco, au Mkulima hivi Hawa ukitumia dalmax si wanakuua game zoteMkuu kuna wachezaji wapo tanzania hiii hii wanakuruhusu utumie dalmax na bado wanakufunga yani hao watu ni zaidi ya software najua huamini