Mashine ya Rostam inafanyaje kazi na imethibitishwa vipi?

Mashine ya Rostam inafanyaje kazi na imethibitishwa vipi?

It shouldn't be used for senior level leaders.
 
Kizazi cha kuhoji,safi sana.ila sidhani kama tutapata majibu.mwenye kuijua ID ya ummy amtag ajekujibu.
 
Kabla hazijaingia kwetu zipo mamlaka kama TBS na TFDA bila shaka wameshazipitia na kuzithibitisha ndio maana unaziona mtaani.. Taasisi zetu zinachapa kazi usiku na mchana kuhakikisha usalama wetu, tuko salama..
 
Rostam anajiandaa kupiga tukio ambalo wote mtakaa chini akishirikiana na Makonda
 
Kabla hazijaingia kwetu zipo mamlaka kama TBS na TFDA bila shaka wameshazipitia na kuzithibitisha ndio maana unaziona mtaani.. Taasisi zetu zinachapa kazi usiku na mchana kuhakikisha usalama wetu, tuko salama..
Inasemekena zimetengenezwa na SIDO.
 
Kwenye dharura kama hizi ni sawasawa na mfa maji. Unajaribu kila kitu. Hata kwenye tiba sasa wanajaribu kila kitu - kuanzia dawa ambazo hazijathibitishwa mpaka procedures mpya ambazo hakuna ajuaye kama zinafanya kazi ama la. Na wakati mwingine inakuwa ni ishu ya kisaikolojia zaidi. Hata kama unajua kabisa kuwa kitu hakisaidii kutatua tatizo lakini kama kinaweza kuwaondolea hofu watu basi unakitumia huku ukitafuta njia zingine zilizo bora. Ndicho kinachoendelea kwa sasa duniani. Mambo yakitulia ndiyo tutajua zipi zilikuwa mbivu na zipi zilikuwa mbichi....
 
Nimeona mara kadhaa ndani ya wiki hii aliyekuwa Mbunge wa Igunga na Mfanyabiashara Maarufu Rostam Aziz akitoa kile kinachoitwa mashine za kunyunyizia dawa zenye kuua virusi. Mashine hizi ni "full body spray" kwamba mtu anaingia mashine zinatoa kitu kama manyunyu au mvuke ambao unadawa zenye kunyunyiza na kwamba dawa hiyo inadaiwa "kuua" virusi vya corona. Maswali:

1. Mashine hiyo imetengenezwa wapi na kwa lengo gani kabla ya ujio wa corona?
2. Je, ni dawa gani inatumika kunyunyizia watu kiasi kwamba wanajiexpose pumzi na ngozi zao kwa dawa hizo?
3. Je, dawa hizo zina vitu gani vyenye uwezo wa kuua corona kwa manyunyu lakini zisiwe na madhara kwa tu kupumulia au kuingia kupitia ngozi?
4. Kutokana na swali la 4; je inawezekana dawa hizi hazina vitu vyovyote vikali (active ingredients) ambazo zinaweza kusababisha kansa (carcinogens)? Visije kuua virusi vya corona lakini vikawa na madhara kwenye chembe za ngozi!
5. Dawa au mashine yoyote ya kufanya tiba inatakiwa ipitiwe utafiti wa kisayansi kuona uwezo wake kufanya unachofanya (efficacy) na kwa usalama (safety). Je, mashine hizi zimefanyiwa utafiti wapi na wa namna gani kuonesha kuwa zinafanya kile inachodaiwa kufanya?
6. Na kutokana na hilo la 5 je mtu akishapita kwenye hii mashine anakuwa amejikinga kwa muda gani? Ni kuwa virusi haviwezi kumgusa (vikimgusa vinakufa kama nzi kwenye moto). Je akibadilisha nguo bado ana "kinga" hiyo?
7. Wizara ya Afya inatakiwa kujibu maswali haya na watu wa TFDA pia.

Haya ni baadhi ya maswali tu. NI wazi kuwa Rostam anataka kutoa msaada na hili ni jambo zuri kweli kweli lakini bila kujibu au kutoa maelezo ya kujibu maswali haya (na labda mengine) ni vizuri watu waangalie na kufikiria mara mbili kabla ya kupita kwenye mashine hizi wakiamini kuwa wameua virusi vya corona na hivyo wako "clear".

Ninachojua ni kuwa mashine za namna hii zimekuwa zikitumika kuspray kwenye maeneo kama aiport, migodi n.k kwa ajili ya decontaminate watu. Na zipo za aina nyingi lakini linapokuja suala la corona ni kwa kiasi gani ziko effective ndio hasa swali langu.

Nje ya hapo, kama majibu ya maswali haya yote yanakubalika kiakili na yana msingi wa kisayansi RA anastahili pongezi za dhati na badala kumsubiria yeye tu serikali iwezeke kwenye kupata vifaa vingi zaidi.

MMM

NB: Mashine hii isije kuwa kama kikombe cha fulani.
Uzuri na furaha yangu ni kwamba Wabunge wengi ni Wa CCM na ndio wengi wazee. Hilo tu
 
Wajinga ndio waliwao
Huu ni ujnga wa ccm na utawala uliopo
Rostam has got nothing to kupoteza kama WaTz mtakufa kama nzi
The guy is cooking something
Alirudi kwao Iran kilichomrudisha Tz ni nini?
ccm ni ile ile Jana leo na milele
Mlimpongeza sana jiwe hana jipya alilolifanya zaidi ya kupitia nyayo za waliomtangulia
It's same old same old
** Wizara husika au hata WHO wanapashwa wadhibiti upumbavu huu
 
Unafikiri wabunge, mawaziri, na timu mbalimbali zilizopo pale bungeni wamepokea pasipo kujiuliza ivo viswali ambavyo ata mwanao ukimletea pipi utakumbana na maswali kibao.
 
Nimeona sido wametengeneza the same! Ila za huyu jamaa sijui zimetoka wapi? Tatizo sijawahi Kumuamini. He is too smart with evil motives behind his doings.
 
Nakumbuka kuna kauli ilitamka Serikali hii haitegemei Fedha za misaada toka kwa matajiri sasa hii imekaaje tena?
 
Alafu hili swala linafikirisha, mbona hatujaona machine kama hii kwa nchi zingine au wenzangu mmeona wapi zinatumika kipindi hiki cha corona?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mashine zipo kwa ajili ya decontamination; miye tatizo langu kubwa ni kutumika kwake dhidi ya corona. Maana virusi vya corona vimekuja na mbwembwe zake... maana hizi mashine zingekuwa zinapunguza sana vifo au kukinga watu nchi kama US, UK, na zile nyingine za daraja la kwanza zingejaza hizi mashine kile mtaa...
 
Nimeona mtu kama Ndugai ndani anafanyiwa demo; ila viongozi wetu ni vichwa maji sana. Hapo karibu na mama wesimama hawajavaa Barakoa
 
Rostam anastahili pongezi kwa ushirikiano anaotoa kwenye kukabiliana na hili janga haya mengine ni mengineyo tu.
 
Back
Top Bottom