CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Hio ndogo ya mayai 150 inaweza patikana kwa bei gani????
Tehe tehe, mkuu ukitaka kufaidi tengeneza parents wako mwenyewe, ndo suluhisho pekee, kununua mayai kwa watu yataka moyo make unaweza nunua mayai ukaambiwa ni fertilized baada ya kuweka kwenye mashine unakuja kugundua sio, au yanaweza kuwa fertilized lakini yakawa yamepitiliza mudawake yaani yana zaidi ya siku 7, hivyo mayai ya kuyaamini ni yale unayo yatoa kwenye kuku wako, haya ya kununua ni 50%
Incubator zinategemeana bei kulingana na manufacture, Ila ushauri wangu na kwa wengine wote kuliko kuchukua incubator ya mayai 150-300 bora kuchukua incubator ya mayai 880 -1000 na zaidi. SABABU KUU NI KWAMBA Gharama za kutumika kutengeneza incubator ya mayai 150-300 ni sawa na gharama za kutengeneza incubator ya mayai 800 na kuendelea, kinacho zitofautisha ni ile body ambayo hata hivyo sio gharama sana vitu vingine vyote ni sawa.
Chukulia mfano wa Memory card, flash au external, utaona kwamba bei ya external ya GB 500 inatofautiana kidogo sana bei na external ya GB 1000
Kamanda i salute you..kila nikisoma post zako uwa ni pana sana na hazina longo longo..naomba nisaidie kitu kimoja,ninataka kuingiza incubator toka China,i have a friend there anaekaribia kumaliza masomo yake,so ameniambia naweza iweka hiyo machine kwenye container yake ikaja na vitu vyake,nakua na shaka juu ya ushuru wa hiyo kitu pale bandarini, hiyo incubator ni ya maya 524, pia sehemu ninayotaka kufanyia project yangu ni Morogoro wilaya ya Kilosa, tatizo hakuna umeme wa uhakika, je naweza nunua solar kwa kusukuma incubator hiyo?natanguliza shukrani zangu!
Unapo sema hakuna umeme wa uhakika sielewi kwa sababu Tanzania haijawahi kuwa na umeme wa uhakika, je umeme upo au haupo? Kama upo ni tofauti na kutokuwepi kabisa, kama umeme haupo kabisa unatakiwa kuwa na solar zenye nguvu kubwa zinazo fua umeme mwingi kuliko inayo tumia mashine hapo unaweza tumia solar 24 hours ingawa ni vizuri vile vile ukawa na genereta ndogo ili solar ikileta shida utumie genereta,mashine ya mayai 540 inahitaji genereta ndogo hizi zinasukuma bila shida, Ila kama umeme upo ila unakatika basi genereta ni nzuri kuliko solar, ila kama umeme hakuna kabisa tumia solar.
Ushuru bandalini upo, walicho ondoa ni import Duty ila VAT iko.pale pale na chaji zingine zipi kama gharama za meli sijui kupakua, kuhifadhi, TBS na kazalika,
Tehe tehe, mkuu ukitaka kufaidi tengeneza parents wako mwenyewe, ndo suluhisho pekee, kununua mayai kwa watu yataka moyo make unaweza nunua mayai ukaambiwa ni fertilized baada ya kuweka kwenye mashine unakuja kugundua sio, au yanaweza kuwa fertilized lakini yakawa yamepitiliza mudawake yaani yana zaidi ya siku 7, hivyo mayai ya kuyaamini ni yale unayo yatoa kwenye kuku wako, haya ya kununua ni 50%
Umenifurahisha ulipoweka fact kua nchi haijawahi kuwa na umeme wa uhakika!ni kweli kabisa mkuu!eneo ninalotaka kuanza hiyo project umeme haujafika kabisa!je ni solar ya ukubwa gani yaweza kuendesha hii incubator?ukubwa wa incubator ni watts 800 kwa volts 240,natanguliza shukrani zangu mkuu,na samahani kwa usumbufu!
naomba utaalamu wa kutengeneza kuku wazazi, na jinsi ya kuongeza tabia fulani kwa kupandisha baina ya kuku wenye tabia tofauti mfano kuongeza idadi ya mayai, kuongeza uwezo wa kukua kwa haraka, au rangi ya manyoya n.k.
Umenifurahisha ulipoweka fact kua nchi haijawahi kuwa na umeme wa uhakika!ni kweli kabisa mkuu!eneo ninalotaka kuanza hiyo project umeme haujafika kabisa!je ni solar ya ukubwa gani yaweza kuendesha hii incubator?ukubwa wa incubator ni watts 800 kwa volts 240,natanguliza shukrani zangu mkuu,na samahani kwa usumbufu!
Bei inategemea na idadi ya mayai, mimi niliagiza ambayo ni automatic inayogeuza upande wa mayai kila baada ya masaa mawili.
Niliyo nayo ni JN96 nilinunua 270,000 kabla ya usafiri na kodi,usafiri nilikuja nayo mwenyewe kutoka huko juu TRA pale airport walichuku35,000.
Ni nzuri kiasi yangu unaweka maji kila baada ya siku tatu ili humidity ndani ya incubator iwe btn 60-70.
Nimeshatotolesha mayai ila wajinga walinipa mayai mabovu nimebahatisha 25 tu.
Bei inategemea na idadi ya mayai, mimi niliagiza ambayo ni automatic inayogeuza upande wa mayai kila baada ya masaa mawili.
Niliyo nayo ni JN96 nilinunua 270,000 kabla ya usafiri na kodi,usafiri nilikuja nayo mwenyewe kutoka huko juu TRA pale airport walichukua 35,000.
Ni nzuri kiasi yangu unaweka maji kila baada ya siku tatu ili humidity ndani ya incubator iwe btn 60-70.
Nimeshatotolesha mayai ila wajinga walinipa mayai mabovu nimebahatisha 25 tu.