DOKEZO Mashirika na Taasisi jengeni Shule za Sekondari za kutwa. Kutakuwa na uhitaji mkubwa Dodoma

DOKEZO Mashirika na Taasisi jengeni Shule za Sekondari za kutwa. Kutakuwa na uhitaji mkubwa Dodoma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mashirika hasa ya dini kama KKKT na RC pamoja na wawekezaji binafsi watusikie Wazazi wa Dodoma.

Dodoma kuna uhitaji mkubwa sana wa Shule bora za Sekondari za kutwa, kwa sababu Mwakani 2027 Watoto watamaliza shule ya msingi wakiwa wadogo wengi katika wastani wa miaka 10 mpaka 11.

Hivyo, wazazi wengi kutokana na changamoto za kimaadili na usalama wa Watoto wanachagua zaidi kupeleka mtoto shule ya kutwa kuliko ya bweni.

Sasa changamoto iliyopo Dodoma, kuna shule nyingii za msingi tena zenye viwango bora vya huduma ila Sekondari za kutwa hamna.

Hebu mtusaidie kupaza sauti labda mashirika na wawekezaji watasikia. Wawekeze Dodoma Soko la shule za sekondari za kutwa zenye huduma bora na usalama wa Watoto.
 
Back
Top Bottom