Mashirika na Taasisi za Umma zinazostahili kufutwa na zile zinazostahili kuunganishwa

Mashirika na Taasisi za Umma zinazostahili kufutwa na zile zinazostahili kuunganishwa

Kipindi inaitwa TFDA nafikiri ndo ilikuwa inaendana sana na TBS.

Nimeonelea hii TMDA na NIMRI ziwekwe pamoja maana zote zinabase kwenye madawa.
Siyo kweli. Mmoja ni mzalishaji na mtafiti huku mwingine ni mamlaka ya usimamizi
 
NIMR imejikita kwenye tafiti za magonjwa ya binadamu.

TMDA imejikita kwenye udhibiti wa madawa ya binadamu na mifugo.

Ebu fikiria tena namna ya kuziunganisha
TMDA labda ikaunganishwe na TPRI (sijui siku hizi inaitwaje?)
 
Mkuu kwa haraka haraka nimegundua unafaidika na moja ya Taasisi kati ya TARURA au TANROADS kwahyo ukiona wazo kama hilo la kuziunganisha unaona kama ugali unaingia mchanga...

Mkuu ni kawaida kuogopa mabadiliko ila lazma tufanye mabadiliko kwa ustawi wa maisha ya baadae
TARURA ni ya kufuta kabisa. Haina inachofanya maana barabara za mitaani zipo TAMISEMI yani haitakiwi hata kupewa bajeti maana ni ufisadi mtupu
 
Chadema na CCM ziunganishwe, hii itapunguza makelele yasiyo na msingi, nchi inahitaji maendeleo
 
Latra na Sumatra kwann wameachwa
SUMATRA iligawanywa na kuwa LATRA na nyingine ile ya usafiri wa majini (sikumbuki jina). Mimi ninaona imependeza ikiwa hivyo.

Ila TANESCO ilitakiwa igawanywe ziwe tatu: kazalisha umeme, ugavi wa umeme na kukusanya madeni na malipo ingependeza sana kuliko sasa ambapo TANESCO ni kama imezidiwa
 
Mnyumbuliko WA mashirika unatokana hasa na dira na dhima zao katika nchi na katika kuleta mgawanyo WA majukumu ie specialization. Hii unasaidia nchi kufocus kwenye maeneo inayotaka kwa kuhakikisha rasilimali zinafika huko.

Kuunganisha taasisi kuzimgatie ;
1.ikiwa kweli taasis zinaovelap kwa kiwango kubwa yaan dhima zao zinafanana
2.mahitaji ya nyakati ikiwa shirika halihitajiki tena.ie mission fullfilled.
3.Ikiwa shirika halina tija kabisa
 
TMDA labda ikaunganishwe na TPRI (sijui siku hizi inaitwaje?)
Hapana mkuu Mi naona NIMR ndo ingeunganishwa na TPRI siku hizi Imeunganishwa na Maswala ya kilimo Inaitwa TPHPA..
Ila combination ya NIMR na TPRI ingekuwa moto sana
 
Kwenye Sekta Ya Ujenzi:
* AQRB: Architects And Quantity
Surveyors Registration Board.
  • ERB: Engineers Registration Board.
  • CRB: Contractors Registration Board.
Hii tungeziacha ziwe Moja kwa sababu..
Kila mmoja anashughulikia Taaluma yake binafsi ni kama afya tu kama MCT,TNMC,MLC na zingine kibao zote zinashughulikia watu wao
 
Siyo kweli, mwanzoni ilikuwa TMDA wanaingilia kazi za TBS ndo maana ikatolewa kutoka TFDA kuwa TMDA kwa sasa wapo sahihi
Mkuu uko sahihi kabisa..

Waliitoa Kutoka TFDA (Tanzania Food And Drugs Authority) kwenda TMDA (Tanzania Medica and Medical devices Authority)

Moja ya sababu ikiwa ni hiyo kuingiliana kimajukumu kwa sababu walikuwa wakifanya ukaguzi na kutoa Licence kwa products zote related to food, drugs, cosmetics and medical services.

Na TBS ikawa inakosa kazi za kufanya kwa sababu hata maji ni Food, kitu chochote kinachoingizwa Mdomoni kiliitwa food na kitu chchote kinachopakwa kiliitwa cosmetics Na ukakuzi wa chemical Zote zitumikazo kutengenezea chakula na Mafuta na lotion..

TBS wakaona ohoo tutakosa kazi kipengele kilichoondolewa ni kimoja tu Ni Food..

Ila sasa Ninaona bado Changamoto Ipo kwanini wasiunganishe Nguvu tupate kitu kimoja maana bado naona mbeleni kutatokea mgongano tu wa kimaslahi kitakuja chakula chenye Dawa ndani TMDA watataka wakikague Na TBS watataka pia kwa sababu ni chakula na TMDA watasema kwa sababu ni dawa..

So ili kuondoa hivi ni bora ziungwe
 
Back
Top Bottom