Kwa nini unawafuatulia mashoga, kwa nini unawawaza? Je una interest nao, chanya au hasi, wamekudhuru kwa lipi, wamekuudhi kwa lipi?
Akitokea mtoto wako au ndugu yako akawa shoga utamuua ?
Wameleta madhara kiasi gani.
Je wamevunja haki zako ?
Je wapo wangapi? Kwa nini wameamua kuwa mashoga.
Je unaouthibitisho kama unaowaona ni mashoga au unasikia tu kama mimi huku njombe.
Kwa nini mimi naishi hata miaka 2 huo msamiati haupo kichwani mwangu, kwa nini wewe unakuzunguka kichwani mwako?
Is it a big issue in TZ.
Je una mamkaka na mwili wa mtu mwingine?
Binafsi naamini mtu mbaya ni yule anaedhilumu haki ya mwnine, kama mwizi,muuaji,mbakaji wa watoto, mdhulumati nk mtu wa hisia kwangu hana nafasi kwa sababu hajaingilia uhuru wangu. Iwapo atakuja kunilazimisha nimfanyie ushoga kwa nguvu, huyo anastahili adhabu kwa sababu kaingilia uhuru wangu vinginevyo aendelee na maisha yake.
Nimekuwa nikijiuliza swali hivi kwa nini binadamu mmoja ampangie binadamu mwenzie jinsi ya kuishi, kuamini na kuamua!
Maadili ya jamii ni uwongo mtupu, maadili yapo katika mtu mmoja mmoja, hivyo pigania maadili yako na familia yako vinginevyo utakosa raha bule kwa sababu ya watu wengine waliokengeuka dhidi ya jamii.