Mashushushu wa Fidel Castro walikuwa na hisia ya sita(Sixth Sense)

Joined
Sep 28, 2014
Posts
78
Reaction score
113
Mashushushu hawa ndio wenye mafanikio makubwa kuliko wote Duniani.

Njama 638 za mauaji aliyoepuka Fidel Castro.(Chini ya mashushushu wenye ustadi wa hali ya juu sana(skillful)

Njama ya kutumia sigara kumuua Fidel Castro ambayo ilitibuka inajulikana sana, lakini njama nyengine 637 dhidi ya maisha yake ni zipi?

Shirika la kijasusi nchini Marekani CIA na watu waliotoroka Cuba wakati wa uongozi wa Castro walitumia nusu ya karne moja kufanya njama za kumuua kiongozi ambaye taifa lake lina athari kubwa kwa Marekani, kulingana na balozi wa Marekani nchini Cuba Wayne Smith.

Wakati mmoja kiongozi huyo wa Cuba alinukuliwa akisema, iwapo kuepuka majaribio ya mauaji kungekuwa miongoni mwa michezo ya Olimpiki ningejishindia medali ya dhahabu.

Hatahivyo baadhi ya njama hizo hazikutekelezwa ,kulingana na aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Fidel Castro, Fabian Escalante.

Stakhabadhi zilizofichuliwa wakati wa utawala wa Bill Clinton zilionyesha kuwa CIA wakati mmoja walianza kuwafanyia utafiti konokono wa eneo la Carebean.

Njama, ilikuwa kutafuta konokono mmoja ambaye angemvutia Castro anayependa sana kuogelea na kumjaza vilipuzi ndani yake kabla ya kumlipua Castro atakapomshika

Mpango mwengine ulikuwa ule wa kutengeza boya la kuogelea ambalo huvaliwa kama shati na ambalo lingetiwa ugonjwa mbaya wa ngozi ili kumuathiri kiongozi huyo.

Mipango yote hiyo ilitupiliwa mbali.

Ajenti huyo alisikitika na akataka mpango mwengine ambao sio rahisi kuugundua,ripoti hiyo ilisema. Mpenzi wa zamani wa Castro, Marita Lorenz alipewa dawa za sumu kumwekea katika kinywaji chake.

Alipewa dawa zenye sumu ili kuweka katika kinywaji cha Castro.Lakini Castro aligundua jaribio hilo na anadaiwa kumpatia bunduki yake badala yake atumie kumuua.

''Huwezi kuniua. Hakuna anayeweza kuniua,"Bbi Lorenzo alisema Bw Castro alimwambia, alipokuwa anahojiwa na gazeti la New York daily.

Castro alidaiwa kutabasamu na kuendelea kuvuta sigara yake.''Nilijihisi nimetolewa pumzi kwa sababu alikuwa na uhakika juu yangu.Alinikumbatia na tukafanya mapenzi''.

Jaribio jingine lililokuwa maarufu dhidi ya maisha ya Castro ni lile la 2000, wakati ambapo mpango uliwekwa kuweka vilipuzi vingi katika jukwaa ambalo alitarajiwa kuhutubia nchini Panama.

Mpango huo ulitibuliwa na vikosi vya usalama vya Castro.

Watu wanne ikiwemo mtoto mmoja wa Cuba pamoja na ajenti wa CIA kwa jina Luis Posada walifungwa lakini baadaye wakaachiliwa.

Pia kulikuwa na mipango ya kumfanya Castro ambaye pia anajulikana '' The Beared'' aonekana kama chombo cha kukejeliwa badala ya kumuua.

Mpango mmoja ulikuwa kumwagia viatu vyake chumvi ya thallium wakati wa ziara yake ya ughaibuni kwa lengo kwamba anaposhika ndevu zake zingeweza kukatika.

Lakini mpango huo ulitibuliwa baada ya Castro kuahirisha ziara hiyo.Castro alichukua tahadhari ya hali ya juu ili kuwakwepa watu waliopanga mauaji yake.

Mwaka 1979 alipokuwa akielekea mjini New York ili kuhutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa hakuweza kuwazuia wanahabari waliomuuliza iwapo alikuwa amevaa fulana ya ndani ambayo ina kinga dhidi ya risasi, alivua shati lake na kuwaonyesha kifua chake.
''Nimevaa fulana ya kawaida'',alisema.

Miongo kadhaa awali mwaka 1975, tume ya bunge la seneti nchini Marekani ilifichua maelezo ya njama nane dhidi ya maisha ya Castro kwa kutumia vifaa ambavyo tume hiyo inasema ''vinachosha akili''.

Njama moja iliopangwa na ambayo karibu ifaulu mara mbili ilikuwa ile ya kutuma dawa za sumu Cuba na kuwapeleka watu kumuua kiongozi huyo.

Ndevu za Fidel Castro pia zililengwa katika njama hizo za mauaji.

Ulikuwa wakati kama huo ambapo rais Kennedy, ambaye aliruhusu uvamizi wa kumuondoa madarakani rais Castro mwaka 1961 aliuawa, ambapo ajenti wa CIA alikuwa anatoa kalamu yenye sumu ilio na sindano kwa ajenti mmoja wa Cuba ili kumuua kiongozi huyo.

NYONGEZA 1


NYONGEZA 2




NYONGEZA 3







DOCUMENTARY: 638 Ways To Kill Castro

 
Na hatimaye amekufa kwa amri ya Mungu.
Wakati wa utoto tulisikia simulizi nyingi sana kumuhusu Castro,ikiwa ni pamoja na kusema huyu jamaa alikuwa akivaa shati lenye vifungo ambavyo akiviunganisha vinatengeneza bastora.

Marafiki zake kama Huggo Chavez,Che Guavara na kina Samora Machel waliuwawa na CIA.Chevez kafa "juzi" tu tukiwa wazee na familia...CIA walimpandikizia liugonjwa lililomuua,na mwaka mmoja kabla ya kifo chake wakampa taarifa kuwa washammaliza,ndio maana siku za mwisho za maisha yake,Chavez alikuwa anawatukana sana Wamarekani na hasa akipata nafasi ya kuhutubia UN..

Marekani sio mtu mzuri hata kidogo,juzi nikaona wale ambao wengi ni mashoga waliokimbilia MIAMI wakishangilia kifo,wakati wale wa CUBA wa kweli wakilia kwa uchungu.
 
Nitaanzia mbali kidogo..

Baada ya fidel kutwaa madaraka kwa kumpindua Batista ndani ya siku 100 za mwanzo alifanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaa baadhi ya mashamba ya miwa, kusogeza huduma za jamii karibu, kupiga marufuku ubaguzi wa rangi nk..

Nchi ya Cuba ilikuwa na idadi kikubwa ya watu ambao hawajasoma zaidi ya asilimia 60 ya watu wale walikuwa hawajui kusoma na kuandika, chini ya Castro akaanzisha utaratibu wa wale wachache wanaojua kusoma na kuandika wawafundishe wale wasiojua, wakasambaa kote nchini chini ya msemo maarufu wa 'kama hujui jifunze ujue na kama unajua fundisha'.

Kupitia mpango huo watu wengi wa Cuba wengi walijua kusoma na kuandika na elimu ilitolewa bure.

Pia nchi hiyo wakati wa Fidel anaingia madarakani ilkuwa na jumla ya madaktari 6000 tu na wengi walikuwa hapoHavana, kule vijijini huduma zilikuwa hakuna na watoto wengi walikufa kwa kukosa huduma. Castro akawaambia madaktari wale waliorundikana mjini wasambae mpaka vijijini wakatoe huduma. Wengi waligoma na kukimbia nchi, ndio chanzo cha wengi kwenda miami na pia watu wengi waliokuwa na uchumi mzuri ambao mali zao zilitaifishwa walimchukia Fidel na kuikimbia nchi, ndio hao walokuwa wakishangilia juzi.

Ili kuleta huduma za afya karibu Fidel alianzisha vyuo vitatu maalum kwa ajili ya kupambana na uhaba wa madaktari na alifanikiwa sana, vifo hasa vya watoto vilipungua sana kuliko baadhi ya miji huko USA wakati huo.

Maadui wa Castro waliongezeka toka nje na ndani ya nchi, CIA walitumia mbinu chafu za kumuondoa Fidel duniani na mipango mingi iliwahusisha wacuba wengi waliokimbia nchi hasa waliokuwa wakiishi Miami.

Sasa Fidel alipambana na mbinu hizo kwanza kitengo cha ujasusi kilikuwa chini yake, kiliitwa DGI(Director General of Intelligence) na kitengo hiki kilikuwa kama mali binafsi ya Fidel, wengi wa waliofundishwa walikuwa nI vijana wadogo hasa walioungana nae huko kwenye milima ya Ciera Maestra wakati wakipambana na Batista na vijana hawa walikusanywa na mama mmoja aliyekuwa karibu sana na Fidel, aliitwa Celia Sanches, huyu alikufa kwa Saratani mwaka 1980.

Vijana hawa asilimia 95 walifanya kazi ya kijasusi bure bila malipo na wakati mwingine walichukuliwa vijana wadogo sana na kupelekwa ""shambani""ambako walipewa elimu ya ujasusi wa hali ya juu sana, na pia walikuwa wazalendo sana kwa nchi yao na watiifu kwa Fidel.

Hakuna CIA officer aliyeingia Cuba bila kufahamika, mipango ya mauaji iliyopangwa na Fidel iligundulika haraka kwani Fidel alifanikiwa kupenyeza vijana wengi kwenda USA hasa Miami na Florida na huko waliishi wakifuatilia kila Wamarekani wanachokipanga juu ya Fidel na wengi wa vijana hawa bila CIA kufahamu kwamba ni majasusi waliwatrain tena ili kufanikisha mipango yao ya kumuua Fidel Castro, vijana hawa walibaki watiifu kwa Fidel na hivyo mipango yote waliyopanga ilimfikia el comandante Fidel Castro bila wasiwasi.

Baada ya John F. Kennedy kuwa Rais wa Marekani alimkabidhi ndugu yake aliyeitwa Robert Kennedy jukumu la kumuua Fidel Castro kwa kupitia Counter Intelligence na Double Agent.

Vijana wa Fidel waligundua njama hizo na zikafika mezani kwa el comandante Fidel Aljandro Castro luz.

Akihojiwa na mwandishi wa Reuters, Fidel alitahadharisha Marekani kwa kusema jaribio lolote la kumuua kiongozi wa Cuba litakuwa na madhara kwa Marekani na wasitishe mipango yao, Wamarekani walisikia lakini walikaidi na Robert Kennendy akaendelea na mipango ya kumuua Castro.

November 22 Lee Oswald alimpiga risasi Rais wa Marekani John F. Kennedy na baada ya saa moja ikatangazwa raisi ameuawa, inaaminika Castro alifahamu mipango hiyo japo alikanusha sana.

Nitarudi.
 
El Comandante de'levis tunakusubiri

Japo sijui ni kweli Fidel alikuwa na taarifa za mipango ya kumuua Kennedy ,kuna aide wake Fiorentino Aspillaga wanasema huyu alikuwa kwenye jumba fulani la mawasiliano na alipewa kazi maalumu ya kufuatilia mawasiliano ya CIA na ile siku ya mauaji basi Fiorentino akapewa order asiendelee kufuatilia hayo mawasiliano ..na badala yake akusanye taarifa zozote kutoka Texas kumbuka Kennedy alipigwa risasi Dallas

Ingawa wakati Fidel anapewa taarifa za kupigwa risasi Kenedy wakati akiwa kwenye beach house yake wakila chakula cha mchana alijua kwa vyovyote lazima atahusishwa na mauaji ya Kennedy hivyo hakuwa na uoga wowote kwa sababu siku zote za maisha yake alikuwa kwenye hatari pamoja na hayo alipata hofu kwamba kumuua raisi wa Marekani sio jambo dogo ,Marekani inagusa karibia dunia nzima hivyo kupotelewa kwa raisi sio tu kutaathiri Cuba bali dunia nzima

Ila pia wanahisi Castro alihusika kwa sababu huyu Oswald aliyempiga risasi Kennedy kuna wakati aliomba visa ya kwenda Cuba kwenye embassy yao iliyopo Mexico akanyimwa visa basi kwa hasira akaropoka atampiga Kennedy risasi ...na inaaminika ubalozi huo wa Mexico ulikuwa center ya ujasusi ya Cuba hivyo chochote kinachofanyika pale Castro lazima anajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…