Mashushushu wa Fidel Castro walikuwa na hisia ya sita(Sixth Sense)

Mashushushu wa Fidel Castro walikuwa na hisia ya sita(Sixth Sense)

Na hatimaye amekufa kwa amri ya Mungu.
Wakati wa utoto tulisikia simulizi nyingi sana kumuhusu Castro,ikiwa ni pamoja na kusema huyu jamaa alikuwa akivaa shati lenye vifungo ambavyo akiviunganisha vinatengeneza bastora.

Marafiki zake kama Huggo Chavez,Che Guavara na kina Samora Machel waliuwawa na CIA.Chevez kafa "juzi" tu tukiwa wazee na familia...CIA walimpandikizia liugonjwa lililomuua,na mwaka mmoja kabla ya kifo chake wakampa taarifa kuwa washammaliza,ndio maana siku za mwisho za maisha yake,Chavez alikuwa anawatukana sana Wamarekani na hasa akipata nafasi ya kuhutubia UN..

Marekani sio mtu mzuri hata kidogo,juzi nikaona wale ambao wengi ni mashoga waliokimbilia MIAMI wakishangilia kifo,wakati wale wa CUBA wa kweli wakilia kwa uchungu.
Ha haaaaa umenikumbushambali sana
 
Dah! hii historia ni nzuri sana na sina budi kuongezea nyama.

Fidel Castrol alikuwa ni mwanachama wa kundi liloitwa The July 26 Movement ambalo lilikuwa likipanga kumuondoa jenerali Batista ambae akiwa kiongozi wa Cuba pia alikuwa akilindwa na Marekani.

Lakini Fidel Castro akiwa na mdogo wake Raul wakiwa nchini Mexico walikutana na maestro daktari, mwanafalsafa na mtaalam wa vita ya msituni Ernesto Che Guevara.

Harakati za kumuondoa Batista zilichukua miaka miwili huku Fidel Castrol na Guevara wakipanga mikakati porini na Che Guevara akapandishwa cheo na kuwa tayari alikuwa na uzefu wa harakati hizi za vita ya msituni katika nchi kama ya Guatemala.

Guevara alikuwa na sifa ya kutumia neno "che" akimaanisha sikiliza au "attention" ili kuwafanya wanaomsikiliza wawe makini.

Walipozungumza na Fidel Castrol, Guevara akamwambia kwamba suala la mapinduzi ya Cuba alikuwa na hamu nalo sana kushiriki na kutoa mchango wake kama mwanamapinduzi na siku hiyohiyo ya mkutano akasaini kujiunga na kundi la The July 26 Movement.

Ernesto che Guevara ndiye aliemsaidia Fidel Castrol kuwafunza vijana wake, khasa mbinu ya kushambulia na kukimbia au "hit and run tactic" mbinu maarufu katika vita vya msituni.

Hii ilikuwa baada ya mafunzo ya hali ya juu alopata kutoka kwa mkuu wa mafunzo wa kundi hili alijulikana kama jenerali Alberto Bayo.

Alisaidia kufundisha matembezi na mchakamchaka porini na kwenye milima, kushambulia na kukimbia bila kukamatwa.

Baada ya mapinduzi Fidel Castrol alimpa jukumu Guevara la kumsaidia kupanga mipango mbalimbali katika sekta za elimu, na khasa kujua kusoma na kuandika.
 
Nashukuru Mungu kuwa kupitia ' uzi ' huu naanza sasa kuwajua wana ' Eagle Wing House ' wa Tanzania kwani ni ukweli usiopingika kuwa kama huna ' experience ' ya ' kutukuka ' ya hiyo ' Fani ' kabisa huwezi kuyajua hayo mambo ya ' Kijasusi ' na ambayo ni ya ' Kitaalam ' kabisa na kuja ' kutiririka ' nayo humu. Akhsante mno muanzisha ' uzi ' umenisaidia sana katika ' utafiti ' wangu usio rasmi ninaoufanya sasa kupitia huu huu ' uzi ' wako.
 
Kipindi che guavara yupo Drc kongo castro alimuambia aende cuba haraka cia wanamsaka che hakwenda akaja kukaa dar akiwa anatumia jina tofauti ili kuficha identity mwisho wa siku akaenda bolivia kufanya mapinduzi ya kuiondoa serikali maskini ndo ukawa mwisho wake. R.I.P shujaa.

Duh...kumbe Marehemu Che Guavara alishakaa hadi Dar! Shikamoo Mkuu.
 
Kama Mungu anakujaalia Mtoto wa kiume, italeta raha kumuita majina kama Fidel au Castro. Sio Juma.
mtoto nae akili zake zinakuwa zakilevilevi tu,unaropoka tu tena wale walevi wa pombe zisozopita kwa mkemia
 
mwanangu wa kiume japo jina lake la ubatizo ni la kikristu,siku nikiwa nimefurahi napenda kumuita Osama aka geronimo.
nilimwita mwanangu tupac shakur kwa ukamilifu wake no addition ya jina langu lakini familia kama unavyojua nilipingwa sana nikaona isiwe tabu ntamuita kimoyomoyo tu hilo jina but lastly nikaona nimuite Ambwene means Ameniona
 
Back
Top Bottom