Mashushushu wa Fidel Castro walikuwa na hisia ya sita(Sixth Sense)

Mashushushu wa Fidel Castro walikuwa na hisia ya sita(Sixth Sense)

N


Ni kweli mkuu, Mimi mwanangu wakiume nimemuita Sankara.

Nimempa jina hilo kwasababu nilivutiwa Sana na harakati za aliyewahi kua Rais wa Burkina Faso hayati Thomas Sankara.

Yupo rafiki yangu mmoja ambaye amewaita watoto wake wawili majina ya Che Guevara na Ho Chi Minh. Wote ni wa kiume.
 
Yupo rafiki yangu mmoja ambaye amewaita watoto wake wawili majina ya Che Guevara na Ho Chi Minh. Wote ni wa kiume.

Ho Chi Minh alikuwa ni mmoja wa majasusi wa kutisha wakati ule wa harakati za ukombozi khasa kwa watu wa Vietnam.

Minh alipofikisha umri wa miaka 10 baba yake ambae alikuwa mwalimu alimpa jina la Nguyen Tat Thanh, Nguyen likimaanisha accomplished yaani mtu aliekamilika kwasababu kabla ya kuanza shule rasmi, tayari alikuwa anafahamu kusoma na kuandika.

Minh wakati wa harakati zake aliweza kusafiri kati ya miji ya Brooklyn nchini Marekani, Paris, London na Moscow akitumia majina ya bandia kama Van Ba, Chen Vang, Luy Thuy na hilo la Nguyen.

Mji mkuu wa Vietnam unaitwa Ho Chi Minh City baada ya kubadilishwa kutoka jina la Saigon mwaka 1976.
 

Baada Kennedy kuingia madarakani CIA walimwambia ni lazima Fidel aondolewe madarakani hii ni baada ya Fidel kutaifisha mali nyingi zilizokuwa zikimiliwa na Wamarekani na pia alianza kuagiza bidhaa toka Soviet.

Baada ya pressure kubwa toka kwa CIA, Rais kenedy akaidhinisha kuondolewa madarakani kwa Fidel Castro na katika mpango huo Kennedy alisema hataki ijulikane kuwa Marekani ndio imehusika na mpango huo kwa hiyo akawataka CIA wahakikishe wanakamilisha mpango huo bila kuacha alama ya mhusika mkuu.

CIA wakaanza mpango huo kwa kuwahusisha wacuba waliokimbia nchi hasa wale waliokuwa Miami, jumla yao ilikuwa 1400 na kikosi cha watu hao kikapewa jina la kikosi 2506, wakapelekwa eneo maalumu na kuanza kupewa mafunzo ya kwenda kumwondoa madarakani El commandante Fidel Castro.

Mazoezi ya anga, majini na ardhini yalifanyika katika kundi hilo la wakimbizi waliokuwa wakipewa mafunzo walikuwepo maagent wa Fidel waliokuwa wakipenyeza taarifa zao havana.

Mazoezi yalipokamilika zilipangwa hatua tatu za mashambulizi ambazo Rais Kennedy alizipitisha, njia ya kwanza ilikuwa ni kutumia ndege za kivita kuzipiga air base zote za Jeshi la Anga la Fidel, walitaka kushambulia na kuzimaliza ndege zote.

Njia ya pili ilikuwa ni kwenda kumalizia mabaki yoyote ya ndege ambayo haikulipuka kwenye mpango wa kwanza na njia ya tatu ilikuwa ni kuingia kwa hao wakimbizi wa Cuba waliopewa mafunzo kwenda kushambulia na kumwondoa Fidel madarakani.

Njia ya kwanza ikaanza kutumika, marubani wavamizi walipewa ndege, ndege zile za kivita zilibadilishwa rangi na kufanana sana na zile za Jeshi la Cuba na pia zilipakwa matope ili zikiwa angani zionekane ni chakavu, jamaa wakaenda wakashambulia kambi ya anga ya Fidel na waliangamiza asilimia 80 ya ndege za Castro, Jeshi la Anga la Castro lilibakiwa na ndege sita tu na marubani saba, ilikuwa big loss kwa comrade.

Baada ya njia ya kwanza kuleta matokea chanya kwa Wamarekani, huko New York kiongozi wa Cuba Umoja wa Mataifa akaitisha kikao, akaituhumu Marekani, Marekan ikakataa katakata kuhusika, wakadai ndege zilizoshambulia ni za Wacuba wenyewe walioasi Jeshi.

Balozi wa Cuba akasema ndege za Jeshi la Cuba sio zilizoshambulia, ndege zilizoshambulia zina mngurumo tofauti na ndege za Cuba, ndege zilizoshbulia ni za Marekani ila mmezibadilisha rangi zifanane na za Cuba ila mmeshindwa kubadili muungurumo.

Hapo rais Kennedy akaingiwa na ubaridi na akasitisha njia ya pili iliyokuwa imepangwa, Maafisa wa CIA walichukia sana kuona rais amekataa njia ya pili kutumika.

CIA wakaenda njia ya tatu ya kuwa deploy wale 1400 ili wavamie Cuba, kule Cuba Fidel mwenyewe aliingia front na kusema hii ni kazi ya Marekani na Cuba will respond in kind.

Baada ya kauli hiyo Fidel alizihamisha zile ndege sita zilizosalia na pia akaandaa mpango mkakati wa kujibu.

Wale wavamizi 1400 wa mara ya kwanza ilikuwa imepangwa waingie Cuba kupitia Trinidad lakini baada ya Kennedy kuigomea njia ya pili, Maafisa wa CIA nao wakabadili njia ya kuingia Cuba kwa hawa wavamizi, wakaelekezwa waingie cuba kupitia hapo the bay of pigs. Mahali hapo Fidel alipafahamu sana sana, lakini katika kujiandaa na adui mwonekano wa pwani ile ilibadilishwa kwa kiasi kikubwa, kiasi kwamba maadui walipokuwa wakija walishindwa kuona vizuri hasa ni wapi Majeshi ya Cuba yamejificha.

Meli zikiwa zimewabeba wavamizi zikafika Pwani ila Jeshi la Cuba likawa na taarifa. El Commandante Fidel akiwa mstari wa mbele kuendesha mapambano, wale wavamizi walishambuliwa sana na meli moja iliyobeba vifaa maalumu ilizamishwa na nyingine iliyowabeba hao wavamizi.

Walipigwa sana, zile ndege sita zilizosalia zikawa zinazunguka anga ya Cuba hasa hapo bay of pigs, wengi wa wavamizi waliuawa na wengine kuchukuliwa mateka. Taarifa zikafika Marekani juu ya hasara kubwa na kushindwa kwa zoezi hilo.

Rais Kennedy akatoa ndege sita za kijeshi kwenda kusaidia, hazikufua dafu kwani ndege nne zilidunguliwa na Jeshi la Cuba, ilikuwa loss kubwa kwa Marekani.

Mpango wa kumtoa madarakan Fidel ukafeli vibaya sana, hivyo ndivyo ilivyokuwa juu ya bay of pigs.
 
Asante De Levis. Tunahitaji wadau walete humu pia simulizi ya "The Cuban Missile Crisis 1962"
 
Ho Chi Minh alikuwa ni mmoja wa majasusi wa kutisha wakati ule wa harakati za ukombozi khasa kwa watu wa Vietnam.

Minh alipofikisha umri wa miaka 10 baba yake ambae alikuwa mwalimu alimpa jina la Nguyen Tat Thanh, Nguyen likimaanisha accomplished yaani mtu aliekamilika kwasababu kabla ya kuanza shule rasmi, tayari alikuwa anafahamu kusoma na kuandika.

Minh wakati wa harakati zake aliweza kusafiri kati ya miji ya Brooklyn nchini Marekani, Paris, London na Moscow akitumia majina ya bandia kama Van Ba, Chen Vang, Luy Thuy na hilo la Nguyen.

Mji mkuu wa Vietnam unaitwa Ho Chi Minh City baada ya kubadilishwa kutoka jina la Saigon mwaka 1976.
Daah kweli upo vizuri. Leta mavitu mkuu mengine.
 
Asante De Levis. Tunahitaji wadau walete humu pia simulizi ya "The Cuban Missile Crisis 1962"
Baadaya vita ya bay of pigs kuisha na ushindi ukawa wa el comandante fidel castro,marwkan hakuwa tena mshirika wa cuba bali adui nambari one...fidel alifanya mawasiliano ya siri ni waziri mkuu wa akati huo huko ussr aliyeitwa nikita krushchev..nawasliano yao yalikuwa juu ya sovieti kuweka vituo vya silaha nchini cuba ili kuilinda cuba dhidi ya uvamizi wowotte toka marekan....kumbuka wakati huo marekan na sovieti zilikuwa katika vita baridi...
Makubaliano yakafikiwa na kwa siri sana sovieti ikaanza kujenga vituo hivyo nxhini cuba...mmerakan hakujua nini kinaendelea mpaka mmoja wa magent wa cuba akiwa bar alimwambia mwenzake aliyekuwa jasusi la CIA kuwa kwa sasa cuba tuna nyuklia...agent akarudisha taarifa washington..
CIA wakatuma ndege yao moja iliyokwwbda cuba na ikapiga picha za size ya kati na kubwa na kuainisha maeneo inakojwngwa mitambo hiyo..ndege ikarudi marekan ba taarifa ya picha na ruban wake..asubuhi siku iliyofuata repot ikafika mezan kwa kennedy..kenedy akaitika kikao pamoja na washauri wake..wakatarhimini hali ilivyo..ndani ya kikao kile mabishano yakaibuka ..wengine wakitaka cuba ishambuliwe kijeshi na wengine wakitaka ipeww onyo kali..
Mabishano talw yakamfanya rais kenedy kumwambia nikita wa soviet kwa barua kuwa asitishe mpango wa kujenga vinu na vituo vya kijeshi nchini cuba vinginenevyo nguvu itatumika...mabadilishano ya barua na majibizano yalichukua silu 13 kati ya hawa wawili..
Taarifa nyingine ikatua washington kuwa vituo vingi vimekamilika na karibu vitaanza kazi..kenedy akamuonya tena nikita wa soviet..nikita akamjibu kenedy hivi..mipango ya sovieti nchin cuba itaendelea kama ilivyipangwa...dunia nzima ilijua sasa vita ya nyuklia inakuja...baadae nikita akatuma barua nyingine ikisema soviet ikisitisha mpango wake nchini cuba basi marekan iape kuwa haitaivamia kijeshi cuba lakini iondoe kituo chake cha kijeshi huko turkey kilichoitwa jupiter....kenedy akajibu kwa kusema nitakubaliana na pendekezo la kwanza na si la pili..
Baada ya jibu hilo nikita akatuma ujumbe wake kwenda marekan alimtuma jasu mmoja na jasusi yule alienda kituo cha abc news na kuongea na mmoja wa watangazaji akamwambia marekan ikubali mpango wa kuondoa kituo chake uturuki na sovieti itasitisja mpango wake cuba..
Siku hiyo hiyo ndege ya kipelelezi ya marekani ijulikano kama U-2 ilidunguliwa na jshi la cuba..kenedy akachukia sana akaanda vikosi vyake kuicamia cuba..gafla ujumbe mwingine ukaja toka klemlin ukisema sovieti imekubali kusitisha mpango wake nchini cuba..wakaharibu mitambo yao na vituo vyao...na marekan ikaondoa kituo chake nchini turkey.....ukawa mwisho wa crisis ile vita baridi ikaendelea
 
Asante De Levis. Tunahitaji wadau walete humu pia simulizi ya "The Cuban Missile Crisis 1962"

Cuban Missile Crisis ilikuwa ni pamoja na mgogoro ambao Fidel Castrol aliuanzisha baada ya Marekani kukataa kununua sukari ilozalishwa Cuba.

Hapo kabla Marekani ilikuwa ni mteja mkubwa wa sukari ya Cuba na walipoweka vikwazo vya kiuchumi ikiwemo kutonunua sukari, Fidel Castrol akaamua kuzungumza na Russia (zamani USSR) na wakaingia mkataba wa kununuliana na kuuziana bidhaa hiyo adimu.

Lakini sababu kubwa ya msingi kabisa ya mgogoro huu ni USSR kuamua kuweka mitambo ya nyuklia nchini Cuba baada ya Marekani kuweka mitambo hiyo kwenye pwani za Uturuki na Italia.

Mkutano wa siri kati ya kiongozi wa USSR Nikita Khrushchev na Fidel Castrol ulifanywa na makubaliano yalifikiwa kati ya USSR na Cuba ambapo kiongozi wa USSR Khrushchev akamuomba Fidel Castrol aweke mitambo ya Nyuklia nchini Cuba ili kuweka uwiano wa nguvu kati ya USSR na Marekani, ulikuwa ni mpango wa siri mno.

Lakini pia Fidel Castrol alikuwa kwa muda mrefu akiiomba USSR kuweka mitambo hiyo nchi kwake ili kujilinda na uvamizi wa Marekani ambao Castrol aliwaona ni maadui wake.

Na hii ilichangiwa sana na kushindwa kwa jaribio la waasi wa Cuba wakisaidiwa na CIA waliposhambulia pwani ya nguruwe au "Bay of Pigs" mwezi April mwaka 1961 na kushindwa jaribio hilo. Kuna jaribio lingine liloitwa Cuban Project Operation Mongoose lilofanywa mwezi Novemba mwaka huohuo ambalo kama jaribio la "Bay of Pigs" liliidhinishwa na raisi JF Kennedy.

Walofahamu mpango huo ni watu wa karibu kabisa na Castrol kama mdogo wake Raul, Ernesto Guevara, Dorticos na mkuu wa usalama bwana Ramoro Valdes.

Lakini Marekani kwa kutumia mitambo yake ya angani na wakagundua msafara wa meli za kivita za USSR zikielekea Cuba, na wakawa wameghadhibika na kitendo hicho Castrol akawaambia wamarkani kwamba mitambo hiyo na silaha za nyuklia zilikuwa ni kwa ajili ya kujihami tu.

Fidel Castrol akamsihi Khrushchev kwamba atumie silaha za nyuklia endapo Marekani wangeishambulia Cuba na Khrushchev hakutaka kufanya jambo hilo.

Khrushchev akiwa hataki vita na Marekani akakubaliana na Marekani kwamba angeondoa silaha na meli za kivita ambazo tayari zilikuwa katika pwani ya Cuba lakini kwa masharti kwamba Marekani iondoe meli zake za kivita katika pwani za Uturuki na Italia na pia itoe uhakika wa kutoishambulia Cuba.

Castrol akiwa amekasirishwa sana na kitendo cha Khrushchev akaweka mpango wa miaka mitano ambao alitaka Marekani wakubaliane nao kwamba kwanza ni kuondoa meli ya kivita kwenye pwani ya Guantanamo, kuachana na kuwasaidia wananchi wa Cuba walokimbilia Miami, kuacha kuingia bila ruhusa katika anga la Cuba na eneo la bahari ya nchi hiyo na pia kuondoa vikwazo vya silaha kwa nchi hiyo.
 
Mkuu kwani Osama ni jina la kiislamu? usiogope kumwita osama aaisee ni jina liko neutral tu
 
Back
Top Bottom