Mashushushu wa Fidel Castro walikuwa na hisia ya sita(Sixth Sense)

Mashushushu wa Fidel Castro walikuwa na hisia ya sita(Sixth Sense)

Ni kweli Castro alikuwa anatembea na mwanamke mpya kila siku na harudii tena! Yasemekana alitimiza takribani wanawake elfu 30.

Anayejua atujuze juu ya hili.
 
Mmmh kwa kweli ni ushujaa ulioje!! RIP Fidel Castro.[emoji16][emoji23]
 
Umetupa habari nyeti ambayo hatukuijua ,huyu Fidel alikuwa jasusi la kimataifa hizi njama za kumuuwa zilifanywa kwa ustadi mkubwa lakini watu wake walimsaidia yeye kuwa salama.
 
Simulizi nyingine ambaye msiache kuileta humu ni ile ya ushindi mkubwa ambao Castro aliupata dhidi ya wavamizi Katika Pwani ya Nguruwe ama Bay of the Pigs mwaka 1961.
 
Well said, ila kama nakumbuka vizuri Robert Kennedy alikuwa Attorney General chini ya kaka yake, akuwahi kuwa Mkurugenzi mkuu wa CIA au Waziri wa Ulinzi - sasa Kaka yake alimpa jukumu ya kumumaliza Castro akiwa chini ya kitengo/mwamvuli hupi au alitaka ku hire a private snipper!!

Actually imekuja kudhilika juzi juzi hapa kwamba muuaji hakuwa Oswald, Oswald aliwekwa kama chambo tu kupoteza lengo, muuaji alisi alikuwa ni former Marine ambaye alikuwa ni namba one katika jeshi la Merikani katika masula ya kulenga shabaha, alifanyiwa mpango wa kujificha nyuma ya shrubs za Glass Knoll mjino Dallas Texas ukiwa chini ya uangalizi wa FBI, alifyatua risasi aina ya dum dum ikafumua kichwa cha Kennedy baada ya kutekeleza mauuji akafungia silaha yake kwenye mkoba wake na kuondoka nayo kwenda Hotelini - makachero wa FBI na Polisi wakimwangalia tu bila ya kumchukulia hatua yoyote! Kumbe FBI na Polisi walikuwa planted sehemu hiyo na Edgar Hoover ili wamlinde muuaji mpaka atakapo tekeleza mauuaji ya Rais wa nchi!!

Ukisoma maelezo ya kina ya muuaji huyo akikiri ukweli huo kabla hajafa mwaka juzi, ndiyo utaona kwamba Amerika wakati mwingine ni Taifa la ajabu sana - Yaani makamu wako wa Urais anashirikiana na wamiliki wa Military Industry Complex na ma Bankers kumuua Rais ili waendeleze vita vya VietNam na kuuza silaha!!
 
N
Kama Mungu anakujaalia Mtoto wa kiume, italeta raha kumuita majina kama Fidel au Castro. Sio Juma.


Ni kweli mkuu, Mimi mwanangu wakiume nimemuita Sankara.

Nimempa jina hilo kwasababu nilivutiwa Sana na harakati za aliyewahi kua Rais wa Burkina Faso hayati Thomas Sankara.
 
🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
4ee51765f6d8968c9789742deb52676f.jpg
pale unapogundua wabaya wako wanataka kukuua.[emoji1619]
 
Duh...kumbe Marehemu Che Guavara alishakaa hadi Dar! Shikamoo Mkuu.
Mkuu GENTAMYCINE na habari zako za Makumbusho kweli hizi habari hukuwa unafahamu?

Che Gueavara alikaa Tz kati ya mwaka 1964-65,aliingia kwa siri japo Serikali ya Tz ilijua ujio wake.Alikaa Ubalozi wa Cuba pale Upanga akipanga safari ya kwenda Zaire kuwasaidia kina Kabila kumuondoa Mobutu.

Safari yake kwenda Zaire(DRC) ilikuwa kwa njia ya gari,alisafiri siku kadhaa mpaka Kigoma na baadae kuvuka kwa mtumbwi ziwa Tanganyika kwa kuvushwa na wavuvi bila wao kumfahamu.

Aliishi ktk kijiji cha Kibamba kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika.Na alitumia jina bandia "code name" la Kiswahili,aliitwa "Tatu".

Baadae aliamua kuachana na Kabila baaada ya kukuta askari wa Kabila hawana nidhamu,kazi yao wakiteka vijiji na kuuwa watu wasio na hatia na kubaka kina mama.Walikuwa walevi hata nyakati za mapambano na wapenda ngono sana.Che akawaambia hawawezi kushinda vita kama "chakula" chao itakuwa ni pombe na wanawake.

Akaamua kuondoka,akaja Dsm,akanywa kahawa,akakaa siku kadhaa,na inasemwa alikuwa anakula chakula mara kadhaa kwenye mgahawa fulani pale Kkoo.

Aliporudi kwao,akaongoza mapinduzi ya Bolivia.Na mwisho utabiri wake wa pombe na wanawake kwa askari wa Kabila ukatimia,kwani Kabila hakumshinda Mobutu toka msituni,bali alifanikisha baada ya Mobutu kuzeeka na kukosa ushawishi.Huyu ndio Che rafiki wa Ruz Fidel Castro Le Commandet
 
El Comandante de'levis tunakusubiri

Japo sijui ni kweli Fidel alikuwa na taarifa za mipango ya kumuua Kennedy ,kuna aide wake Fiorentino Aspillaga wanasema huyu alikuwa kwenye jumba fulani la mawasiliano na alipewa kazi maalumu ya kufuatilia mawasiliano ya CIA na ile siku ya mauaji basi Fiorentino akapewa order asiendelee kufuatilia hayo mawasiliano ..na badala yake akusanye taarifa zozote kutoka Texas kumbuka Kennedy alipigwa risasi Dallas

Ingawa wakati Fidel anapewa taarifa za kupigwa risasi Kenedy wakati akiwa kwenye beach house yake wakila chakula cha mchana alijua kwa vyovyote lazima atahusishwa na mauaji ya Kennedy hivyo hakuwa na uoga wowote kwa sababu siku zote za maisha yake alikuwa kwenye hatari pamoja na hayo alipata hofu kwamba kumuua raisi wa Marekani sio jambo dogo ,Marekani inagusa karibia dunia nzima hivyo kupotelewa kwa raisi sio tu kutaathiri Cuba bali dunia nzima

Ila pia wanahisi Castro alihusika kwa sababu huyu Oswald aliyempiga risasi Kennedy kuna wakati aliomba visa ya kwenda Cuba kwenye embassy yao iliyopo Mexico akanyimwa visa basi kwa hasira akaropoka atampiga Kennedy risasi ...na inaaminika ubalozi huo wa Mexico ulikuwa center ya ujasusi ya Cuba hivyo chochote kinachofanyika pale Castro lazima anajua
fuatilia 'the magic bullet' aliyopgwa kenedy,kenedy hakupgwa risasi moja na wala oswald hahusiki
 
Umetupa habari nyeti ambayo hatukuijua ,huyu Fidel alikuwa jasusi la kimataifa hizi njama za kumuuwa zilifanywa kwa ustadi mkubwa lakini watu wake walimsaidia yeye kuwa salama.
KGB itakua walikua wakimpga tafu,kumbuka ussr walikuwa na makombora cuba kwa ajili ya kukata ngebe za marekani
 
Mwanangu wa kwanza nimempa jina fidel Castro.
Mwanangu wa pili nimempa jina Ghadafi.

Mwanangu wa tatu nimempa jina Thomas sankara.
Mwanamapinduzi halisi. Waambie wawasome hao, ili wajue kwa nini wanaitwa majina hayo.
 
Tatizo ndani ya CIA kumejazana mashushushu kibao wa Castro ambao hata kulipwa hawalipi lakini ni waumini sana wa ideology ya Castro na Cuba. Wazee na sasa wajukuuu. Hii ni problem kubwa sana Langley
 
nimejifunza mengi sanaaaaaa huu uzi ila nin SWALI
kuna movie yeyote imeshawahi tungengenezwa juu ya maisha ya fidel au che guevera?

nitarudi kuchek jibu naona mb zinakata broooo
 
Huyu mtu nampenda kuliko navyojipenda mwenyewe. Huwa nikikaa kumsoma mpaka machozi yananitoka. Kwangu mimi ni mtu ambaye ataishi daima kwenye fikra zangu siku zote za maisha yangu.
umemsoma kwenye kitabu gani mkuu na sisi tumegee kidogo
 
Back
Top Bottom