Masikini UKAWA

Masikini UKAWA

Ukawa wanataka kuwaeleza nini wananchi wasichokijua? ila wanajua kuwa walichaguliwa kutengeneza katiba bungeni wala siyo uzurura majukwaani
 
- Juzi nilikutana na mbunge mmoja wa Chadema kwenye viwanja nikamtajia ukawa akaniomba sana na kunishi nisiseme kwa watu wasisikie maana ukawa sasa ni tatizo sana kwa wananchi, sikuamini alichokuwa anakisema kumbe na wao wameshaelewa kuwa wanayoyafanya sasa hata wananchi hawafurahii!!

Le Mutuz System
Cheap propaganda,from an old baphoon...
 
Kina Nape,
Wanadhania ushindi wa 2/3 upande wa "bara" kura ya maoni, hivyo kufanya bao 1-0 ndio ushindi wa msimao wao. Wanadhania kura ya maoni itaangalia wingi wa kura (grand total) kama uchaguzi wa rais wa Muungano. Hawajui kwamba ushindi kamili utahitaji pia washinde 1-0 upande wa zanzibar yani 2/3 pia kuungwa mkono upande ule. Hilo halitatokea, upande wa zanzibar mtapigwa 1-0 serikali tatu hivyo matokeo kuwa 1-1. Na hawajui madhara ya matokeo haya ni nini kwa CCM na muungano kwa ujumla. Mbaya zaidi, hawajui matokeo yatakuwa haya haya hata kama:

1. Polisi watafanikiwa kuzuia mikutano yote ya UKAWA mpaka siku ya kura ya maoni.

2. Hata kama chadema itakufa kesho na kupotea kabisa katika siasa za Tanzania.

Hoja ya Tanganyika ilianzia humo humo CCM, tena ikiletwa na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa (Aboud Jumbe) 1983. Hapakuwa na chadema wala ukawa. Na nchi ilikuwa chini ya chama kimoja (CCM).

Hoja ya Tanganyika ikaendelea na tume mbalimbali zilizoteuliwa na marais. Hapakuwa na chadema wala ukawa.

G55 - kundi la wabunge, wote walikuwa ni CCM. Na hapakuwa na ukawa wala vyama vingine vya siasa nchini. Rais wa Jamhuri ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM wakati ule (Mwinyi), makamu mwenyekiti na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais (Malecela), katibu mkuu ccm taifa (Kolimba), wote waliridhia serikali tatu. Malecela kama kiongozi wa serikali bungeni, bunge 100 pct CCM, akafanikisha hoja ya Tanganyika ipite. Waziri wa Sheria na Katiba wakati ule (Samuel sitta), akaanza mchakato wa kura ya maoni kabla ya Nyerere kuingilia.

Mwalimu angekuwa hai leo, asingeizuia Tanganyika kwani aliamini katika ccm imara, ccm yenye ushawishi mkubwa, ccm inayolinda katiba ya nchi. Leo znz wamevunja katiba ya nchi, leo ccm sio imara tena na wala haina ushawishi mkubwa tena, kwani upinzani umeshamiri. Chini ya mazingira haya, katiba ya nchi haiwezi tena kuwa ni sera ya chama cha siasa.

Mwalimu aliwahi sema kwamba "yapo ya maana na yapo ya kijinga aliyofanya katika uongozi wake". Hakika, hili la serikali mbili lilikuwa ni la kijinga (kwa kuazima maneno yake). Na akaenda mbali na kusema kwamba anashangaa viongozi waliomfuata, badala ya kuachana na ya kijinga na kuendeleza ya maana, wao wanaacha ya maana na kuendeleza ya kijinga.
Nape Nnauye, acheni kuendeleza yale ya kijinga kama serikali mbili nyakati hizi. Endelezeni ya maana - boresheni azimio la arusha liendane na mahitaji ya leo, sio kuboresha serikali mbili. Hilo ni la kijinga kabisa.

Kwa maelezo haya, nadhani ni dhahiri kwa nape kwamba kwa kushambulia UKAWA, Chadema, "he's barking at the wrong tree".

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

cc nape nnauye

Jisikie aibu kwa hoja hizi. Hivi ni kwanini vijana wengi wa ccm mnakosa hoja linapokuja jambo la kutetea maslah ya taifa? Hamuwezi hata kidogo kujilinganisha na vijana wa upande wa pili mkaelimika. Kijana popote alipo inasadikiwa ni mwenye akiri zinazochemka na kufanya kazi kwa wepesi sana.

Sasa mbona tunaona tofauti kwa wenzetu wa ccm kwanini mnataka tuendelee kuishi kwa mawazo ya wazee tena mawazo mnayo yarhadidia ni yale yasiyo na tija kwa taifa mawazo ya kujenga nchi ninyi mnayatupa hii ni nini hasa?

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
niliwahi kusema nikiwa kigoma kuwa ukawa ni kaburi la vyama vya upinzani nchini! Sasa nimeangalia bunge asub hii na kuona hao waliokuwa wakiaminiwa kama ni ukawa wamo bungeni. Huu ni msiba mkubwa kwa ukawa. Sasa wamebaki chadema,nccr na cuf tena si wote!

Kimbieni msiba huu mkubwa. Cuf na nccr mnaingizwa mkenge na chadema ambayo inaishi kwa matumaini kwasasa! Fumbueni macho!
Hongera olouch!



mizambwa
inaniuma sana!!!
 
- Juzi nilikutana na mbunge mmoja wa Chadema kwenye viwanja nikamtajia ukawa akaniomba sana na kunishi nisiseme kwa watu wasisikie maana ukawa sasa ni tatizo sana kwa wananchi, sikuamini alichokuwa anakisema kumbe na wao wameshaelewa kuwa wanayoyafanya sasa hata wananchi hawafurahii!!

Le Mutuz System
Kweli masisiem ni kisima cha umbeya na unafiki haijalishi mwanamme wote ni kama wanawake.
 
Chama cha CUF ndiyo KING PIN wa hii katiba mpya, no wonder Sitta amekwenda ZNZ kuwaangukia CUF. UKAWA wanawahitaji CUF ili kukwamisha katiba mpya ya ki-CCM. On the other hand CCM wanawahitaji CUF ili kupitisha katiba mpya ya ki-CCM. Hivyo basi CUF wameshika MPINI wakati UKAWA na CCM wameshika MAKALI. Kwa wale mliowahi kucheza karata CUF wamelamba DUME, UKAWA na CCM wamelamba MAJIKE, wanasubiri mmoja wao aolewa na CUF.
 
Chama cha CUF ndiyo KING PIN wa hii katiba mpya, no wonder Sitta amekwenda ZNZ kuwaangukia CUF. UKAWA wanawahitaji CUF ili kukwamisha katiba mpya ya ki-CCM. On the other hand CCM wanawahitaji CUF ili kupitisha katiba mpya ya ki-CCM. Hivyo basi CUF wameshika MPINI wakati UKAWA na CCM wameshika MAKALI. Wote (UKAWA NA CCM) wanasubiri huruma ya CUF. Kwa wale mliowahi kucheza karata, CUF wamelamba DUME, UKAWA na CCM wamelamba MAJIKE, wanasubiri mmoja wao aolewe na CUF.
 
Nape wale madiwani wawili Wa shinyanga Kara ya mwasele,na Kata ya ngokolo uliowapa Hindi batili(fake) wakihame CDMA na kujiunga ccm wanakutafuta.

Cheque zilibounce benki,nape acha utapeli Wa kisiasa,uliwadanganya kwa m 5 cash na Hundi fake ya 25 m,wakavua gwanda wakavaa gamba ...kwenda Benki wakaambiwa hiyo ac haina pesa ya kutosha....kwa salsa wamehama mji,wanakutafuta wamesema wakikukamata ama zako ama zao
 
Ukawa bora wangebaki Dodoma maana ni karibu na Milembe hosp.
 
Nape huwa ananipa shida sana kuwaza,pengine si mwanadamu.....mmmh...vichwa vya habari vyake,point anazoandika.
 
Niliwahi kusema nikiwa Kigoma kuwa UKAWA ni kaburi la vyama vya upinzani nchini! Sasa nimeangalia bunge asub hii na kuona hao waliokuwa wakiaminiwa kama ni UKAWA wamo bungeni. Huu ni msiba mkubwa kwa UKAWA. Sasa wamebaki Chadema,nccr na cuf tena SI WOTE!

Kimbieni msiba huu mkubwa. Cuf na nccr mnaingizwa mkenge na Chadema ambayo inaishi kwa matumaini kwasasa! Fumbueni macho!
Hongera Olouch!
+

we nepi ni majanga.unaropoka hujijui kuwa mwisho wako kisiasa ni November 2015.tutakusahau kwa ujumla wako labda ujiandae mapema kurudi CCJ.we ukawa nani kakuambia ni ya chadema mbulula mkubwa
 
Ukawa wanataka kuwaeleza nini wananchi wasichokijua? ila wanajua kuwa walichaguliwa kutengeneza katiba bungeni wala siyo uzurura majukwaani

Hakuna Mbunge aliywchaguliwa na Wananchi kwenda Kutengeneza Katiba Abadani. Wabunge waliteuliwa na Raisi kuwa wajumbe wa Katiba kupitia Ubunge wao. Ila sisi hatukuwatuma shughuli hiyo na ndio maana tunasema hili Bunge ni Batili, Wajumbe wote wanatakiwa watoke huku Mtaani na Ikiwezekana wasio hawa wanasiasa.
 
Hawa ukawa tushawajua sana hawana jipya tena la kutueleza wakalale nyumbani kwao huku mitaani hata wasitie mguu kabisa.
Usiseme hukumitaani ila utaje mtaa walk maana co Mitaa yote inachukia ukawa
 
Chemshabongo ya siku: chagua jibu lililosahihi kuliko yote (mshindi atapata zawadi nono)

NAPE ni
a) Kiazi kikuu
b) Kiazi kitamu
c) Kiazi mviringo
 
Cha kusikitisha ni kuwa huyu aliyepost hii kitu ni katibu mwenyezi TAIFA wa chama tawala!
...unajiuliza hawa watu wamepenyaje hadi kushika hizi nafasi nyeti katika nchi yoyote!
 
Upinzani ukifa kama ccm wanavyoomba (japo ni dua la kuku) mizania ya siasa haitakuwepo na hivyo taifa litakosa a balanced opinion. Watawala watabweteka na matokeo yake huduma za kijamii zitazorota na kupelekea social unrest.

Namkumbusha Nape kwamba ccm inaitwa chama-tawala kwakuwa kuna vyama vya upinzani kama ambavyo chama tawala Moshi ni chadema na ccm ni upinzani na maendeleo yapo.
 
- I hope huu muungano utadumu maana tunayoyasikia huku mtaani watabaki Chadema peke yao,!!

Le Mutuz System

Mashujaa wa kweli hawatakiwi kuwa wengi, CDM wakibakia peke yao nitawaona wanaume kweli kweli!! Ila nje kuna support ya wananchi wengi ambao sumu ya mafisadi haijawaaffect.
 
If we are to find a child in this forum, I believe you are a dumbest kid here.
This of course is drawn from your 'Childish comments', relative to your age.

ptuuuuuuu.....


ukawa movement is childish not this forum mrs/mr
 
Back
Top Bottom